Kulupango
JF-Expert Member
- Mar 19, 2020
- 288
- 534
Kila ifikapo sikukuu ya Eid, iwe Eid ya kuchinja (Udhu-hiya) au Eid ya baada ya Ramadhani (Eidil - Fitir). BAKWATA hualika viongozi wa Serikali kuja kwenye baraza la Eid, cha ajabu zaidi sio kwa kiongozi mualikwa wala Mashekhe mada kubwa huwa ni kuzungumzia AMANI.
Sasa najiuliza waisilamu ndio watu wa vurugu kwenye nchi hii mpaka kila sherehe yao kuzungumze mada ya amani na tafaruku za nchi?
kwanini sikukuu ya kuchinja yasitolewe mawaidha ya Kisa cha kuchinja kutoka kwa Baba wa Imani Nabii Ibrahimu. Badala yake wanaalikwa viongozi kuja kuzungumza mambo ya Amani na kutolewa mifano ya nchi zilizo athiriwa na vita? Mbona sherehe za Pasaka na X-Mas hatuoni mada hizi za Amani zikizungumzwa?
Niwaombe viongozi wa BAKWATA, tumechoka na hizi taratibu zenu za kuja kuzungumza mambo ya Amani badala ya kuzungumza mafunzo husika ya siku hiyo. Hata kwenye mashindano ya visomo vya QUR'AN uwanja wa Taifa, anakuja kiongozi anazungumza mambo ya Amani. (sijui kuna tatizo gani hapa)
Na vipi mtu asiye muisilamu akawa mgeni rasmi kwenye mambo ya imani?. Yani kwa mfano sisi tupo kwenye sherehe ya pasaka kisha utuletee kiongozi wa serekali ambae ni muisilamu aje kuwa mgeni rasmi kwenye imani yetu ya kikristo, ilihali hafahamu chochote kuhusiana na pasaka.
Niombe viongozi wa serekali wasihusishwe kwenye shughuli za imani ya dini kama ''wageni rasmi'' kwasababu serekali haina dini. Na wakihusishwa basi wahudhurie kama watu wa kawaida. TUMECHOKA