Kuna tatizo gani Umoja wa Vijana wa CCM

malang0

JF-Expert Member
Apr 7, 2021
440
518

Miaka ya huko nyuma Umoja huu wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ulisifika sana kwa kuandaa viongozi bora , wenye weledi na uongozi, wenye maarifa, uzalendo na nchi yao, wachapa kazi na wenye misingi ya haki, utu na maadili ya kutosha mfano wa ni pamoja na Waziri Mwandamizi wa siku nyingi anayehudumu Wizara ya Ardhi Mh. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro waa sasa Martin Shigella.

Lakini miaka ya hivi karibuni Umoja huo umekuwa ukitoa viongozi wasio sifa wenye na mifano mmibaaya kwa Taifa, mf. mwaka 2014 Paulo Makonda aliyepikwa kwenye umoja huo alimpiga vibao Waziri Mkuu M staafu Jaji Joseph Sinde Warioba. Mwaka 2015 tukamwona aliyekuwa Mwenyekiti wa muda mrefu Dr.Emmanuel Nchimbi akipinga maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Chama na kuongoza kikundi wakiimba wana imani na Lowassa.

Alipoingia Magufuli kwenye uenyekiti wa chama na kumpa mpwa wake kuongoza umoja huo, Kheri James naye akatoka adharani na kutishia kuwandunga watu wa upinzani na sindano za sumu. Aliyekuwa Mwenyekiti wa umoja huo mkoa wa Arusha 2017, Lengai Ole Sabaya alishtakiwa kwa kesi ya forgery kujifanya usalama wa Taifa na sasa yupo Kisongo na kesi ya kuendesha genge la wahalifu.

Je nini kumetokea ktk UVCCM imeacha kupika viongozi wazuri na sasa kutengeneza wahalifu, wapiga deal na wachumia tumbo?
 
Uchaguzi ukiisha huwezi kuwaona UVCCM. Ila ukiipinga serikali kwa upotoshaji watakujibu. Ukigusa penyewe wananoti na kukaa kimya. Mambo yapo kidigitali
 
Kimsingi ccm imeshachoka kushindana kisiasa kwani imeshapoteza ushawishi kwa umma. Sasa hivi matumizi ya nguvu tu ndio silaha yao pekee kubaki madarakani kwa shuruti. Ukishaona chama kinatumia zaidi mabavu kukaa madarakani, basi ujue mwisho wa chama hicho uko karibu sana.
 
Naam Mkuu yule dhalimu magufuli aliwapa uwanja wa kuropoka chochote kile hadharani bila kujali athari za kauli zao kwa jamii yetu ya Watanzania. Ndiyo sababu Watanzania wengi tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kumchukua yule dhalimu maana nchi ilikokuwa inaelekea siko kabisa.
Watu walikosa aibu kabisa, imagine mtu anajitpa hadharani kuwa atawadunga sindano za sumu.

Hivi huwa hawakemewi?
 
Sijui nini kilitokea, nimesoma nae shule aliitwa Erick Ngambeki, nimekuja kumuona majukwani akiitwa Heri James sijui nini kilitokea, labda alibatizwa.
Hilo la erick ngambeki lilikuwa hali sound vizuri kama la heri james. Ni hivyo tu
 
Back
Top Bottom