Kuna tatizo gani uchaguzi usifanyike Jumapili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna tatizo gani uchaguzi usifanyike Jumapili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paschal Matubi, Sep 19, 2010.

 1. P

  Paschal Matubi Member

  #1
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  *****
  CHANZO: TANZANIA DAIMA
  TAREHE: SUNDAY, SEPTEMBER 19, 2010
  MWANDISHI: Joseph Misango Magata
  *****

  Juzijuzi maaskofu wakatoliki na waprotestant waliunda umoja uitwao Jukwaa la Wakristo. Kisha wakaomba uchaguzi wa rais na wabunge usifanyike Jumapili wakizingatia athari kwa wakristo.

  Ukazuka mjadala. Ni siku gani ambayo si ya kuabudu? Ombi likakataliwa, tarehe ikabaki ileile, Jumapili ya mwisho ya Oktoba. Maadam kukataliwa kule hakuondoi athari zile, basi ni vigumu kudhani hoja hii sasa isahaulike.

  Nimekuwa nikitafakari wazo ambalo sijui kama linawezekana kwa wenzetu waprotestant lakini tuone linavyowezekana kwetu wakatoliki.

  Mpangilio wa misa za Jumapili za Kanisa Katoliki hutofautiana sehemu hadi sehemu. Ukubwa wa kanisa, wingi na tabia ya waumini hufanya misa ziwe zaidi ya moja. Hivyo misa hutajwa kwa namba, misa ya kwanza, ya pili, au ya nne.

  Ukiuliza ya kwanza inaanza muda gani, kwa mazoea utaambiwa ni ile inayoanza jua linapochomoza. Wengine huianza saa 12:00 na wengine hata saa 01:30 asubuhi. Je, hizi ndizo saa maalum za kuanza misa za Jumapili? Kama sivyo, je, ni muda gani wa kuzianza?

  Tunajua tarehe hubadilika saa 06:00 usiku. Hivyo misa ikianza dakika hii basi hiyo ni ya Jumapili.

  Hata asiye mkristo anazifahamu zile misa za usiku unaotangulia Krismas na Pasaka ambazo kwa kiingereza huitwa "Vigil" na hivyo ni vizuri litumike neno "Mkesha" badala ya neno "Vijilia" (Rejea: Misale ya Waumini, 2004, uk. 49 na 253). Nchi zingine misa hizi huanzwa saa 06:00 usiku.

  Kalenda (liturjia) ya wakatoliki kwa siku ya Oktoba 31 haina tukio kama vile Pasaka au Krismas. Sanasana siku hiyo ni ya Mtakatifu Wolfgang (Askofu) wa Swabia,Ujerumani. Hivyo mwaka huu iko kama Jumapili zingine isipokuwa imeongezewa pilika za kufunga mwezi wa Rozari.

  Tarehe hiyo ingekuwa ni sherehe (solemnity) kama ilivyo Krismas basi wengine wangeamua kujipunguzia athari zile kwa kushiriki misa ya "mkesha" ili asubuhi wawahi foleni za vituoni hata kabla ya saa 02:00.

  Sasa tuone vigezo rasmi. Kifungu namba 2180 cha Katekism ya Kanisa Katoliki kinasema hivi: siku ya Jumapili na sikukuu za lazima, muumini anawajibika kushiriki misa inayoendeshwa "siku yenyewe" au "jioni kabla ya siku yenyewe".

  "Siku yenyewe" ni tarehe halisi ya siku, mfano Oktoba 31 ni Jumapili na ndiyo "siku yenyewe". "Jioni kabla ya siku yenyewe" ni jioni inayoitangulia Jumapili hii yaani jioni ya Oktoba 30 ambayo ni Jumamosi. Kifungu hiki kimerudiwa hata kwenye Sheria za Kanisa au Canon Laws {Can. 1248 (1)}.

  Hivyo, jioni ya Jumamosi inaweza kutumika kwa misa ya Jumapili. Wasabato huianza Sabato yao Ijumaa jioni. Wakatoliki kwa sababu zilezile nao tumeona misa zao za Jumapili huadhimishwa tangu Jumamosi jioni.

  Sina haja ya kuzama kwenye sababu zilizofanya Kanisa liitukuze Jumapili badala ya Jumamosi. Zimefafanuliwa kwa milleniam mbili sasa. Anayezihitaji ni bora asome barua (Apostolic letter) ya Papa John Paul II aliyoitoa siku ya Pentekoste ya mwaka 1998 iitwayo Dies Domini kwenye tovuti ya Vatican (www.vatican.va).

  Je, hiyo Jumamosi, ni jioni ya saa ngapi zinapoanza misa za Jumapili? Neno "afternoon" limetafsiriwa kuwa ni tangu saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 {Oxford Advanced Learner"s Dictionary, New 7th Edition, 2008}. Kiingereza si kigezo vinginevyo misa hizi zingeanza baada ya saa 12:00.

  Papa Pius XII alitoa maelekezo (Apostolic Constitution) Januari 06, 1953 yaitwayo Christus Dominus. Sehemu ya maelekezo hayo iitwayo Constitution, Rule VI:12 aliamuru kwamba misa inayolazimika kufanyika siku kama Jumamosi isifanyike baada ya saa 10:00 jioni. Hayo yalitolewa kwenye gazeti la Kanisa yaani AAS 45, (1953) 14-24 na yapo kwenye tovuti ifuatayo {www.ewtn.com/library/PAPALDOC/P12CHDOM.HTM}.

  Hivyo misa yoyote hata ijumuishe ibada ya ndoa, ikianza Jumamosi saa 10:00 jioni basi ni misa ya Jumapili. Mazoea yaweza kufanya usahau au usijue kwamba misa ya kwanza ya Jumapili inaweza kuanza Jumamosi saa 10:00 jioni.

  Nchi zinazozingatia misa hizi waumini wake wanajua zinaitwa Anticipated Mass. Huko ukiuliza misa ya kwanza Jumapili inaanza saa ngapi, hata mtoto atakujibu ni Jumamosi saa 10:00 jioni.

  Jimbo Katoliki la Denver, Marekani wana ratiba maalumu mtandaoni ya hizi misa za Jumapili zinazofanyika Jumamosi jioni {www.archden.org/index.cfm/ID/4/servID/4}. Ukisoma ratiba ile utaona kwamba misa hizi huanza saa 10:00 jioni hadi saa 11:30 jioni.

  Papa John Paul II alifariki Jumamosi , Aprili 02, 2005. Mwandishi wa Newsweek aitwaye George Weigel anasimulia Papa alivyoshirikishwa misa iitwayo Divine Mercy Sunday, saa chache kabla ya kifo chake. Ni misa aliyoagiza iadhimishwe kila Jumapili ya Pili ya Pasaka. Japo alifariki jioni saa 3:37 kikanisa tunasema alifariki baada ya kusali ya misa ya Jumapili {Rejea: Pope Benedict XVI And The Future of The Catholic Church, ISBN-13: 9780066213316, uk 76}.

  Uadhimishaji wa Jumapili unamega masaa nane kutoka kwenye Jumamosi. Hivyo Jumamosi isiyo sikukuu basi inabaki na masaa 16 wakati Jumapili yanakuwa masaa 32. Siku zingine yanabaki masaa yaleyale 24 iwapo haziitangulii sikukuu ya lazima (Solemnity) kama vile Krismas {Rejea: Sheria za Kanisa: Can. 202(1)}.

  Sheria ya Kanisa (Can. 1247) inamkumbusha mkatoliki asiishie tu kushiriki misa za Jumapili na sikukuu za lazima halafu akimbilie shughuli zingine maana pia inamtaka apumzike. Ndipo mgongano ulipo na serikali nyingi au waajiri wengi duniani. Swali linaibuka, je, apumzike kuanzia ile saa 10:00 jioni ya Jumamosi?

  Swali hili liliifanya Vatican isisitize kwamba ukishiriki misa Jumamosi jioni basi umeshashiriki misa ya Jumapili. Lakini kupumzika iwe tu ni kwenye tarehe yenyewe ya Jumapili {Rejea: Comm 12 (1980) 359}.

  Msomaji, ambaye leo ndiyo anayajua haya asijione mgeni pekee. Mitandao (blogs) ya kikatoliki huulizwa sana muda wa kuianza Jumapili na majibu yanatolewa kwa ufasaha. Tuliojijengea tabia ya kuhoji au kudadisi utandawazi umetuongezea majirani na marafiki wengi duniani huko mitandaoni wenye hamu ya kufafanua kila swali bila kukwepa ama kutumia majibu ya mkato.

  Tarehe ya uchaguzi imebaki ileile ambayo haikuwa pendekezo la maaskofu wale wanaozingatia athari zile. Lakini tumeuona uwezekano wa kuitumia Jumamosi kuanzia saa 10:00 jioni kuwe na misa ya Jumapili (Anticipated Mass).

  Kumbe, Kanisa Katoliki linaweza kupunguza athari zile kwa kuitumia siku moja kabla ya uchaguzi ambayo ni Jumamosi. Ni pale litakapoamua kwamba Jumamosi hiyo iwepo misa maalumu (intention) kwa ajili ya uchaguzi unaofanyika kesho yake na misa hiyo ianze saa 10:00 jioni.

  Ikifanyika hivyo nchini kote watakaoishiriki watanufaika kulala wakiwaza kuamka mapema na kuwahi foleni za njiani na misururu ya kujipanga vituoni kunakopigwa kura.

  Vilevile, kanisa linaweza kutumia misa hii kama marudio (revision) ya kuuhimiza ule waraka wake wa mwaka jana unaopendwa na waadilifu lakini unachukiwa na waovu tu. Ikibidi kuukumbushia vifungu vinavyogusa upigaji kura kesho yake, iwe kama wanafunzi wanavyopekua kurasa siku moja kabla ya mtihani.

  Ikifanyika hivyo majimboni na parokia zote nchini zilizoenea mijini na vijijini, basi ushawishi wa mwisho saa chache kabla ya uchaguzi utakuwa ni wa kanisa. Nafasi ya malumbano haitakuwapo kwani muda huo linasubiriwa giza liishe tujipange vituoni.

  Baadhi ya taarifa za anga (Celestial Information) zinatabiri kwamba jioni hiyo Jumamosi, Oktoba 30 sehemu za Mtwara zilizo mashariki zaidi hapa nchini (latitudi 10.35, longitudi 40.44), jua litazama saa 12:19 jioni (Rejea: www.dawnsun.net/astro/suncalc). Hivyo, hata walioko Mtwara wanaweza kumaliza misa na kufika nyumbani kabla ya giza la usiku.

  Ikitangazwa mapema, basi yawezekana mahudhurio jioni hiyo yatafurahisha kwani uzoefu wa Jumatano ya Majivu, Alhamisi Kuu au Ijumaa Kuu utazingatiwa vilevile na hoja kwamba siku mbili tu zijazo kuna misa zingine za jioni hapo Novemba 01 na Novemba 02.

  Kama nilichoeleza kinawezekana kwa walutheri, waanglikana, wapentekoste na wengine, basi hainufaishi kuendelea kuwawaza waliokataa kubadili tarehe, ni bora utumike uwezekano huu.

   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mzee hii mada ilijadiliwa kwa kirefu nyuma hapa JF ikaonekana wakiridhishwa wakatoliki na walutheri kwa kuondolewa jumapili, basi waislamu nao watadai ijumaa isiwe siku ya uchaguzi, wayahudi na wasabato watadai ijumamosi isiwe siku ya uchaguzi na waprotestant watasema tusipige kura kabisa maana wiki nzima wanasali. Sasa sijui tutaenda wapi mzee!!!

  Mie nadhani iachwe tu hii kwani tarehe hiyo imepangwa itafanyika according to tarehe na nadhani jumapili ni siku ya mapumziko kwa watanzania basi tuambieni lini siku nyengine ya mapumziko ambayo utawapata watanzania hawafanyi kazi??? Binafsi naona watu wanakosa cha kufikiri ni mtazamo wangu tu!!!
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Sioni tatizo uchaguzi kufanyika jumapili ingawa kuna mantiki yatokanayo na ukweli kuwa jumapili siyo siku ya kazi kiserikali; kwa hiyo kupiga kura siku ya jumapili ni kama kufanya ovataimu na hivyo wafanyakazi wa vituo vya kupigia kura watalipwa zaidi ya kiwango chao cha kawaida.
   
 4. M

  Mdanganywa JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 542
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Tulijadili huko nyuma lakini kwa uelewa finyu wa wakati ule hakuna kati yetu aliyekuja na pendekezo la kama huyu jamaa. Mimi namkubali kwa sababu hajasema siku ibadilishwe ila kasema wakristo wana fursa ya kubadili utaratibu wao kama siku ile inawakera.

  Bwana mzee uwe unasoma hadi mwisho. Au ndiyo ule uvivu wa kusoma kama si uvivu wa kuelewa?
   
 5. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  nawashauri wasipige kura
   
 6. KATIZAJI

  KATIZAJI Member

  #6
  Sep 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 58
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mwaka 2005 uchaguzi ulifanyika siku ya jumatano na ilitangazwa kuwa ni 'public holiday'. Kwa watu wote wenye uwezo wa kupiga kura walipata nafasi nzuri ya kwenda kupiga kura na kurudi majumbani kupumzika na kusubiri matokeo. Hii niliipenda sana.

  Tukumbuke kwamba kupiga kura ya haki ya kila raia aliyetimiza umri wa kupiga kura na uhuru wa kuabudu ni haki ya kila mtanzania. Jumapili ni siku maalum kwa wakristo kuabudu kama ilivyo ijumaa kwa waislamu na jumamosi kwa wasabato.

  Napendekeza ichaguliwe siku yoyote katikati ya juma na iwe rasmi kwa ajili ya uchaguzi. Siku hiyo iwe ni mapumziko kwa wafanyakazi ili wapate nafasi ya kupiga kura kwa utulivu na kutafakari mustakabali wa nchi yetu.
   
 7. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wanajamvi mie siwaelewi hawa walio madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 viongozi wa makanisa walilamika juu ya tarehe na siku za jumapili ambazo serikali hupanga kwa ajiri ya upigaji wa kura ambapo huingiliana na ibada.

  Ndipo serikali ikakiri udhaifu huo na kudai kutafuta siku kati ya Jumatatu na Alhamis kuwa siku ya kupiga kura.

  Lakini nashangaa mpaka leo wanaendelea na tabia yao sijui mpaka raia wagome ndo warekebishe naona kwa serikali hii "sikivu" hawasikii
   
 8. Mandla Jr.

  Mandla Jr. JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2014
  Joined: Dec 15, 2013
  Messages: 3,101
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wanabodi,

  Kama kuna kitu nataka kiingizwe kwenye Katiba mpya basi ni siku ya Uchaguzi Mkuu au Chaguzi ndogo kufanyika siku ambazo sio ya weekend.

  Kama Jumamosi na Jumapili. Kuna kila sababu uchaguzi ukafanyika siku za kawaida ili kuwapa nafasi wananchi wengi kupata nafasi ya kushiriki.

  Kwanini uchaguzi ufanyike jumapili?

  Hivi hili liko sawa kweli?

  Mandla.
   
 9. Mandla Jr.

  Mandla Jr. JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2014
  Joined: Dec 15, 2013
  Messages: 3,101
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Je, Katiba ya sasa inalazimisha hivyo au ni Tume ya uchaguzi inataka hivyo???
   
 10. Kibwebwe

  Kibwebwe JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2014
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 797
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  mkuu kuna kitu unataka kuongea funguka uwanja ni wako tukusaidie
   
 11. mzenjiboy

  mzenjiboy JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2014
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 834
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi ukiwa siku ya kazi watu wengine watakosa kuhudhuria au wapewe ruhusa kazini, jambo ambalo ni hasara kwa serikali na mashirika.

  Ama weekend watu wote wapo free.
   
 12. ipogolo

  ipogolo JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2014
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 4,053
  Likes Received: 2,934
  Trophy Points: 280
  jumapili n sawa kufanyika uchaguzi.
  ukisema ichaguliwe siku za jumatatu-alhamisi utawakwaza wengi.
  mathalani uchaguzi mdogo wa chalinze ungefanyika siku za j3/alhamisi itabidi ofisi za serikali zifungwe. je wananchi wasio wa eneo la uchaguzi nao wasipate huduma za kiserikali chalinze?
   
 13. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2014
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  ni siku ambayo watu wengi hawaendi kazini
   
 14. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2015
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Juzi Jumapili 11.1.2015, maelfu ya waumini wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) linaloongozwa na Askofu Mkuu Zachary Kakobe, walivaa TShirt zenye maandishi “UCHAGUZI USIFANYIKE JUMAPILI”, katika ibada maalum ya maombi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Katika maombi hayo maalum yaliyofanyika katika Kanisa hilo lililoko barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar-Es-Salaam; Askofu Kakobe aliwaongoza waumini hao kumshukuru Mungu kwa ajili ya roho ya usikivu iliyomwingia Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyetangaza katika hotuba yake ya Mwaka Mpya kwamba Kura ya Maoni kuhusu Katiba pendekezwa itafanyika ALHAMISI 30.4.2015.

  Katika maombi hayo, Askofu Kakobe alisema kwamba kwa miaka mingi, kilio cha Wakristo wengi kimekuwa kwamba siku ya kupiga kura isiwe siku ya Jumapili inayoingilia haki ya Kikatiba ya kupiga kura na uhuru wa kuabudu kwa Wakristo usiotakiwa kuingiliwa na mamlaka ya nchi, kama inavyoainishwa katika Katiba, Ibara ya 5 (1) na Ibara ya 19 (2); hivyo hawana budi kumshukuru Mungu kwa jinsi ambavyo Serikali ilivyosikia kilio chao, kwa kutangaza kwamba Kura ya maoni itafanyika Siku ya Alhamisi, badala ya siku iliyozoeleka ya Jumapili.


  Kwa msingi huohuo, waumini hao walimwomba Mungu katika maombi hayo kwamba, Serikali izidi kuwa na usikivu na hivyo kutangaza siku ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ambayo haitakuwa Jumapili, wala Jumamosi wala Ijumaa; ambazo ni siku za kuabudu kwa waumini wa madhehebu yote ya Wakristo, Wasabato na Waislamu; ili Wakristo na Watanzania wote kwa ujumla wapate kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura. Askofu Kakobe alisema kwamba imekuwa kawaida kwa wanasiasa kujiuliza kwa nini watu wengi hawajitokezi siku ya kupiga kura, bila kuwaza juu ya kujenga mazingira ya kuwawezesha watu wote kupiga kura, kwa kuifanya siku ya kura kutokuwa siku ya Ibada.


  Askofu Kakobe alitoa mifano ya nchi zinazotuzunguka ambazo hufanya Uchaguzi wao Mkuu kuwa siku ambayo siyo siku ya Ijumaa, Jumamosi au Jumapili; ili watu wengi wajitokeze kupiga kura, kwa mfano Zambia ambayo itakuwa na Uchaguzi siku ya JUMANNE 20.1.2015, baada ya Rais wao aliyechaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa JUMANNE 20.9.2011, kufariki. Vilevile alitaja siku za Uchaguzi Mkuu uliopita wa nchi nyingine kama ifuatavyo: Malawi (JUMANNE 20.5.2014); Zimbabwe (JUMATANO 31.7.2013); Kenya (JUMATATU 4.3.2013); Uganda (JUMATATU 18.2.2011); Rwanda (JUMATATU 9.8.2010); Burundi (JUMATATU 28.6.2010); na Afrika Kusini (JUMATANO 7.5.2014); na baada ya kutaja mifano hiyo, aliwaongoza waumini kumwomba Mungu ili kwamba Serikali iwe na usikivu katika jambo hili pia, na kutangaza Siku ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu wa 2015 katika nchi yetu Tanzania, kuwa siku yoyote ambayo siyo Jumapili, Jumamosi, wala Ijumaa; na kuifanya siku hiyo kuwa siku ya mapumziko maalum yenye kazi moja tu kuu, ya kupiga kura.

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 15. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2015
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,678
  Likes Received: 30,819
  Trophy Points: 280
  amen...
   
 16. H

  Hatugombani JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2015
  Joined: Jun 15, 2013
  Messages: 757
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  ameen!!
   
 17. liwaya

  liwaya JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2015
  Joined: Jan 20, 2014
  Messages: 759
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 60
  Si juzi ila jana
   
 18. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2015
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ujumbe umefika, tusubiri wezi wa kura na majibu yao. Tena ungetengewa siku mbili ili kama kunakulinda kura na kulala kituoni kesho yake watu wawe off.
   
 19. shaks001

  shaks001 JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2015
  Joined: Feb 6, 2014
  Messages: 1,256
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Na tunaosali jumanne,j5 na j3 inakuwaje?
   
 20. MUSSA ALLAN

  MUSSA ALLAN JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2015
  Joined: Oct 13, 2013
  Messages: 18,964
  Likes Received: 7,718
  Trophy Points: 280
  Tisheti moja iliuzwa kwa bei gani?

  Hapo ni biashara kama kawaida.
   
Loading...