CHIBA One
JF-Expert Member
- Nov 16, 2018
- 560
- 2,087
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na hili jambo kwa watumishi wa umma,
Mfano, Mtu amesoma ugavi, kwa level ya diploma, akaenda kusoma Mipango kwa level ya degree, anakuja kuandika barua ya kuomba "Recategorization" kwa mwajiri wake ili kama kuna nafasi pengine halmshauri kwenye idara ya mipango akae pale...kinachotokea ni kwamba kama kuna nafasi kwenye idara basi anaambiwa ataanza na mshahara kama mwajiriwa mpya..Mfano alikuwa ameshapanda daraja mpaka E, au F basi analazimika kuanza upya kwenye level D ya ngazi ya degree, mbona kama ni uonevu? Kwa nn asiendelee na mshahara wake wa awali?
Ndugu yangu mmoja yeye alikuwa mwalimu, akahamia halmashauri kama afisa utamaduni, akaenda kusoma degree ya UTUMISHI, kamaliza wakamuweka kukaimu utumishi kwa kuwa Afisa utumishi alienda kusoma.
Mwisho wa siku wamempa barua ya kurudi shuleni, ama la akae utumishi lakini arudi level D ya mshahara, ukizingatia kabakiza miaka 2 kustaafu.
Wizara husika inabidi liangalie sana hili kwa sababu, inakuwa kama hakuna faida kwa mtumishi wa umma kujiendeleza, kama mtu amefanya kazi miaa 20, anaamua akapate degree yake, akirudi kuomba kubadilishwa cheo anaambiwa utaanza na ngazi ya mshahara wa elimu yako maana yake nini? Kwa nini asiendelee na daraja la mshahara alilonalo?