Kuna tafauti gani Mh Abuu Bakari kati ya Tanganyika ya zamani na Tanzania ya sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna tafauti gani Mh Abuu Bakari kati ya Tanganyika ya zamani na Tanzania ya sasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 29, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by amini // 29/06/2011 // Habari // No comments

  [​IMG]Tanganyika kabla ya Muungano, nembo ya Taifa.

  [​IMG]Tanganyika ya sasa simbuli(nembo) ni ile ile jee Wazanzibar si tuko ktk tumbo la Tanganyika kwa jina la ubatizo Tanzania?.

  Kama Mh AbuuBakari ni Mwana Sheria basi kuna vipengele vya sheria
  hakuvipitia vizuri? kwanza ni sheria na haki za mzulumiwa, ambao
  Wzanzibar kwa mujibu wa sheria ndio wazulumiwa wakupwa tokea mwanzo wa
  huo mfumo mzima na utaratibu wake wa Muungano.
  Haiwi ndowa ukitaka kuowa nilazima makubaliano ya wenye kuoa na kuolewa
  wakubaliane sio kulazimiswa tu, sasa wahusika wa Muungano ni wzanzibar
  wenyewe na hawakuulizwa na hivi sasa Mh AbuuBakari sijamfahamu alipo
  sema hata hio mswada wa maoni ya katiba mpya basi wananchi wataangaliwa
  maoni yao? alipo ulizwa na muwakilishi wa chake chake kuwa wananchi
  wakiamua kusema Muungano basi jee vipi Mh Abuu? Mh asema eti tutapima na
  hayo maoni nyenye jee vipi hayato hatarisha ulaji wetu ? maana mimi
  naona Mh kajibu utumbo?.
  Mara zaote hakuna mtoto kumzaaa mzee? sasa kati ya Wzanzibar na akina
  Abuu na wenzake ipi power? mimi naona Mh Abuu nimiongozi mwa watu wenye
  kuhitaji sifa kutoka Tanganyika na kuwakandamiza Wzanzibar.
  Maana kisheria Wzanzibar Muungano upo au haupo? Muungano mimi nahisi
  haupo maana huwezi kufanya ushirika na Kombo kecho ukambiwa umefanya
  ushirika na Nyange? uchirika ninao fahamu mimi ni makubaliano yani ni
  (agrement) hata ndoa basi zina Agrement M/mungu katuwekea(cheti cha
  ndoa) sasa na huu Muungano wetu unao Agrement kama ipo na nisikiavyo
  kuwa Agrement ni kati ya Tanganyika na Zanzibar? sasa kinacho
  tuchanganya Wzanzibar nikuwa leo twambiwa Tanganyika haipo ipo Tanzania
  From no where?.
  Sasa kweli Mh Abuu Muungano ni halali? na baado tuendelee kulinda na
  kuenzi? mimi nahisi Mh Abuu unamsadia Aduwi na Mradi wake wakuimaliza
  Zanzibar kwa jina la ubatizo Tanzania.
  Mh Abuu katika huo mkataba wa Muungano(Artcle of Union) kuna kipengele
  gani kilicho andika Tanzania? a.) b.) Kama Muungano kisheria ni halali?
  Jee ilipo vunjwa Tanganyika na Bunge la Tanganyika na Katiba ya
  Tanganyika ambae ndio mchirika wa Zanzibar Memba Baraza la Mabinduzi
  au Baraza la Uwakilishi la Sasa jee Mulishauriwa kisheria au vipi na
  kama mulishauriwa uko ushahidi wowote?
  C.) Kama hamukushauriwa jee Bado Muungano nihalali? na Kama nihalali
  jee mkataba wa Muungano umetaja Muungano huu sasa ni wa Tanzania na
  Zanzibar? Yani mkataba umefanyiwa marekebisha na Sulusi 3 za wahusika wa
  pande mbili za Muungano?
  Jengine ni kiungo cha Mkataba wa Muungano Arcle of Union? Raisi wa Watu
  wa Zanzibar ndio kiungo kikubwa cha Muungano kwa vile Rais kapigiwa kura
  na Wzanzibar ambae anawakilishi watu wake sasa kiungo cha Muungano hivi
  sasa kinacho wawakilisha Watu wa Zanzibar ktk Muungano ni kipi ikiwa
  Rasi wa Zanzibar states yake ktk Muungano ni Waziri asio na wizara
  maalum yani hata ofisi Bara hana ya Muungano na ni mjumbe wa baraza la
  mawaziri . Jee bado Muungano ni halali?.
  Na ikiwa tushukulie anae wakilicha Muungano ni Dr Bilali sheria gani na
  ridhaa gani ya kuwawakilisha wazanzibar? kama mimi siko ktk ccm/cuf au
  ktk chama chochote jee bilali kapata ridhaa gani kwangu mimi Mzanzibar
  aniwakilishe wakati mimi sio ccm wala sina chama?.
  Na kama Muungano Mh Abuu ni halali kisheria Yapi mambo yasio ya Muungano
  Bara na yanasimamiwa na katiba gani isio ya Muungano ikiwa Tanganyika
  ndio haipo? b.) Jee nivikaao vingapi vilivyo kwisha kaa Baraza au Bunge
  linalo jadili mambo na rasilimali za Tanganyika lililokaa kujadili
  mambo yao ya sio ya Muungano?.
  Na jee Mh Abuubakari SMZ na wajumbe wa Baraza la Uwakilishi na
  Wanasheria kwa vile Muungano ni halali Jee tumerizika kuwa na mshirika
  mpya Tanzania badala ya Tanganyika? na kwa zamira gani na nia gani kufaa
  kwa Tanganyika ikawa haitajwi wala kusikika tena kama Zanzibar lengo na
  mazumuni ni nini?.
  Au nikupata mwanya wa kuwa utaifa wa Zanzibar na kuwa na sera ya
  serekali 1 Tanzania lakini power tafauti? Hivi sasa kilisho badilika ktk
  Serekali ya Tanganyika ni jina tuu nisawa na Zaire ya zamani kuita
  Kongo lakini nembo za nchi nizile zile za awali za Tanganyika kama nembo
  ya Taifa ya Adam na Hawa? na Katiba ya Tanganyika ndio hii hii ya
  Tanzania kuna vipengele tu flani vimebadilishwa lakini haiizuru
  Tanganyika.
  Jee Mh Abuu na Wajumbe wa Baraza Mumerizika na mapungufu yote mazito na
  makubwa kuwa bado Muungano ni halali na tuwenzi na kuudumisha? kwa nini
  Tanganyika isiwepo kama kweli Muungano ni halali.
  Mimi nahisi Muungano umeshapoteza uhalali wake tokea kufa kwa Tanganyika
  na nyiyi viongozi au munao jita wana sheria kuna mpako wakutupeleka
  ovyo kutokana na maslahi yenu mulio wekeza Bara ya kibiashara, sisi
  hatuko tayari Wzanzibar kuza nchi kwa maslahi ya wafanya biashara waloko
  Bara au kusema ukivunjika Muungano watakwenda wapi? warudi nyumbani
  bado tunawahitajia , nibora kurudi nyumbani kuliko kubakia ugenini?.
  Zanzibar itajengwa na Wzanzibar wenywe wenye ari na uchungu wa nchi yao
  na kila Wzanzibar wakiondoka basi ndio hasara ya Zanzibar maana mipango
  ni kuingiza wakeni kwa wingi na kuua Uzawa wa ki-Kizanzibar, Zanzibar ni
  ndoko hata ukilinganicha na Mkoa wa Murogoro una watu wengi kuliko
  Zanzibar kwa hio kupotea kwa Identite ya Kizanzibar nimara moja tu.
  Haingii akilini kabisa kwa mtu mwenye akili timamu kuwa watu million 44
  kungana na watu million 1.2 hii sio halali ni zulma na uonevu mkubwa.
  Mungu ibariki Zanzibar na ujalie imani mzuri viongozi wetu wabadilike ili kuinusuru Zanzibar na kizazi chake kuangamia.
   
Loading...