Kuna tabia naiona kwa Waathirika wengi wa VVU/ UKIMWI katika Hospitali kadhaa Dar. Je, kana faida gani?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,876
Sijajua kwa Mikoa mingine bali kwa Mkoa niliopo wa ‘ Wajanja ‘ na ambao Mimi GENTAMYCINE ndiyo nasema Mji Mkuu wa Tanzania (na siyo Dodoma ) kuna ‘ Kajitabia ‘ ka Kipuuzi nimeanza Kukaona na naona kanaanza Kuota Mizizi ambapo utakuta Muathirika wa VVU/ UKIMWI anaishi Mbagala lakini cha Kushangaza anaenda Kuchukua Dawa zake (ARV) Hospitali ya Bunju.

Kama haitoshi kuna ‘ Kajitabia ‘ kengine ka Kipuuzi ambapo utakuwa Waathirika hao hao wa VVU/ UKIMWI wakienda Kuchukua hizo Dawa zao za (ARV) wakifika katika Hospitali wanacheza Dili na Manesi ambapo Wao huwa hawaingii ndani Kuzichukua bali huwaagiza hao Manesi wawachukulie na wanaweletea nje na ‘ Kusepa ‘ zao mazima.

Je, tabia hii ina faida gani hasa katika vita dhidi ya Maambukizi haya ya VVU/ UKIMWI kwa Tanzania na Kizazi chake?
 
Mkuu hii habit haijaanza jana wala juzi. Na haijanza hivi karibuni bali ipo kitambo tu.

Hil sio kosa la wahusika au waathirika bali ni ni jukum la hizo taasisi kubain residency ya watu wanao wahudumia wanatoka wap na wawe na namna ya kujiridhisha kuhusu taarifa hizo za makazi ya wagonjwa wao (kama kwel wanawajali, maana serikal inamkono mrefu reffering to wenyevit wa vitongoji a.k.a nyumba 10 ambao wangeweza ktumika vizur kusaidia hil kama nia ipo)

Pia sio tatizo mtu kutoka mbagala kuchukua dawa Bunju as long as anakidhi na kufuata vigezo wanavyo vitaka.katika person level of privacy, hii inahusika.if am not comfortable kuchukua dawa kituo A kwann nisiende Kituo B ambako nitakua free even kuelezea progress ya afya yangu.

Mwisho, kila kitu kina manufaa yake (na changamoto pia) .lakin tabia hii ww unayoiona kama ya ajab, kwa wagonjwa ina manufaa ya ku conserve privacy yao.Pia husaidia kuondoa unyanyapaa.
 
Kuna dada mmoja tunatoka sehem moja ni swaiba wangu sana kuna siku moja tukawa tunaongelea maswala ya mtaa wetu huko mwanza jinsi vijana wengi walivo kufa ..idadi kubwa walikua wamekufa kwa ngoma yule dada na mm tuliwateta sana na kuona kua wale walikufa kwa matendo yao maovu bila kujua .

Huyu Mungu mwacheni tu mdogo wa huyu dada alikua anasoma chuo kimoja huko Dar alirudi akiwa na hali mbaya kiafya dada mtu ndo akawa anamuuguza kumbe yule binti alikua amewaficha kua anaumwa UKIMWI dada mtu alimuuguza mdogo wake kwa upendo akijua tu mdogo atapona kuja kugundua dogo ana vidonge anatumia. dada mtu ndo akahamaki akaenda kupima si akakutwa kaambukizwa .Tangu siku hiyo anakuja kuniambia sitakuja kukaa kumkashifu wala kusema mtu anae umwa ugonjwa wowote na kujiona mm km ni mwamba ...Na Mungu anisamehe sana maana sikujua km nilikua nakosea sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GENTAMYCINE, post: 33758059,

“Sio tatzo kuchukua dawa mbali na unapoishi,tatizo ni kuchukua dawa kwa njia za panya ni ngumu kujua kama dawa zinakusaidia au zinakuletea nabadiliko hasi mana kila visit kuna parameters zinatakiwa zifatiliwe kuhusu mgonjwa ambapo hutuwezesha kuamua aendelee na regime husika ya dawa au abadilishiwe pia kusort viral resistance kutokana na poor drag adherence pamoja na hayo lazma kucheki uzima wa ini, figo na moyo na mana vikizingua hivi tiba yaweza kuwa sumu ukamuua mgonjwa.Tusijifiche kias cha kutoweza kupata updates zinazoweza kutupa ujasiri na maarifa ya kuishi na hao wadidu mwili na tusiwadhuru wengine.
 
Sijajua kwa Mikoa mingine bali kwa Mkoa niliopo wa ‘ Wajanja ‘ na ambao Mimi GENTAMYCINE ndiyo nasema Mji Mkuu wa Tanzania (na siyo Dodoma ) kuna ‘ Kajitabia ‘ ka Kipuuzi nimeanza Kukaona na naona kanaanza Kuota Mizizi ambapo utakuta Muathirika wa VVU/ UKIMWI anaishi Mbagala lakini cha Kushangaza anaenda Kuchukua Dawa zake (ARV) Hospitali ya Bunju.

Kama haitoshi kuna ‘ Kajitabia ‘ kengine ka Kipuuzi ambapo utakuwa Waathirika hao hao wa VVU/ UKIMWI wakienda Kuchukua hizo Dawa zao za (ARV) wakifika katika Hospitali wanacheza Dili na Manesi ambapo Wao huwa hawaingii ndani Kuzichukua bali huwaagiza hao Manesi wawachukulie na wanaweletea nje na ‘ Kusepa ‘ zao mazima.

Je, tabia hii ina faida gani hasa katika vita dhidi ya Maambukizi haya ya VVU/ UKIMWI kwa Tanzania na Kizazi chake?
Tatizo ni unyanyapaa, jamii bado haijapokea vizuri elimu kuhusu Ukimwi. Tupunguze kuwanyooshea wenzetu vidole tuwaonyeshe upendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom