Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,702
- 36,121
Habari!
Katika pilikapilika za hapa na kule nilifika ofisi moja ya umma (Shirika la umma). Watumishi wamejaa madeni sio poa, mtumishi anadaiwa na Bank mpaka tatu, au benki moja kuna deni juu ya deni.
Hapo kuna mikopo ya wakopesha pesa kwa riba, yaani pesa za mkononi. Akipata posho analipa deni anakopa tena.
Nilimuhoji mmoja wa watumishi ambaye huwakopesha wenzake alisema karibu watumishi wote wana madeni ya namna hiyo.
Yeye mtaji wake ni mdogo, hivyo alinishauri nifungue ofisi ya kukopesha karibu na ofisi yao endapo nitakuwa na mtaji mkubwa. Alinihakikishia kuwa nitafanikiwa kiuchumi haraka.
Ni wakati sasa wataalamu wa uchumi kutoa semina elekezi za lazima kwa watumishi wa umma.
Tatizo sio MISHAHARA midogo tu bali tatizo hasa ni ukosefu wa elimu muhimu ya fedha.