Kuna siri gani kwenye chumvi?

Chumvi ya mshana jr imetusaidia sana.

mabaharia wanaozama baharini nao walisema kuna chumvichumvi, sijui ni kweli ?
 
Mods naomba mtauweka uzi huu kwenye jukwaa sahihi kama nimekosea.

2 Wafalme 2:19-22

Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. ndani yake.

Wakamletea. Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.

Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.




Leo katika pitapita zangu nikakutana na video moja tiktok kuna mdada anaongea habari za chumvi, story za kuogea chumvi na kadhalika. Na kuna watu wanashuhudia kabisa zimework out kwao.

Pia nikakumbuka zile story za kama mtu mtu ana mikosi wanamshauri akaoge maji ya baharini atoe mikosi. Huenda kuna ukweli. Mimi sijajua.

Nikalazimika kutafuta kwenye biblia story za chumvi na ndio nikakutana na hiyo ya 2 Wafalme 2:19-22. Sijajua kwenye vitabu vya dini zingine kama imezungumzwa wenzetu mtatusaidia.

Kwenye bible inaonesha kumbe chumvi ilikuwa inatumika toka miaka hiyo kuponya vitu as kama ilivyo kwenye hiyo story ya wafalme.

Kuna siri gani kwenye chumvi?

Kama una nondo za kuongezea unaweza kutiririka.

Jumapili njema.
Hiv karibuni nimeona mtu ameandika kuwa ukichukua kitunguu swaum kizima ukachanganya na chumvi hlf ukaweka chini ya mto mchawi hakusogelei
 
Hata magadi ni mazuri kuliko hata hyo chumvi, hutibu mambo mengi, ikiwemo tumbo, pia huondoa uchawi wa zongo, so ukichaganya magadi na hyo chumvi ya mabonge Matokeo yake ni makubwa zaidi, pia ukimwagia kwenye biashara inaondoa machawo yote mabaya na aliyeroga eneo lako atajua hajui huko aliko.
Mtu akioga maji aliyochanganya na chumvi plus sabuni ya magadi je?

Hapo inakuwaje?
 
Hivi mke wa Lutu alipogeuka nguzo ya chumvi ni nani aliyegeuka nyuma kuthibitisha kuwa aligeuka nguzo ya chumvi
Swali fikirishi ila ilithibitishwa na mumewe kwani walishaambiwa na malaika hilo jambo na katika safari yao akakosekana mmoja ambae ni lutu basi ikajulikana kuwa amekuwa chumvi sawa sawa na neno wa bwana mungu wetu nalo likatimia.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom