Kuna siri gani kati ya mti mtu aliojinyongea na uchawi?

Msomi hewa

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
768
1,066
Wakuu habari za mda huu

Napenda kuchukua fursa hii adhimu ya kuwa mwanachama JF kujadili jambo pamoja na nyie wanajamii wenzangu.

Kuna siri gani kati ya wachawi na Mti uliotumika kujinyongea Mtu.

Kumekuwa na tetesi (kama si taarifa) kuwa mara nyingi sehemu alipojinyongea mtu utakuta matawi ya mti yule yamekatwa,

Jambo hili nimelifuatilia kwa mda kitambo ila majibu yake hayaridhishi,

Karibuni wenye ujuvi wa mambo haya.
 
Mtwara niliwahi sikiia hii habari, kuna sehemu gari iligonga mti na MTU/ watu walifariki hapo hapo. Watu mpk Leo wanachimba udongo kwa ajili ya mambo yao ya kishirikina. Nilishangaa sana na ndio kwanza niliona huko.
 
Unapoamua kujiua ni ujinga uliopitiliza.....wachawi uwa wanajua ulipojitolea roho na kumwaga damu....utakuwa umeacha damu yako na bahati tele.....hawawezi chimbua ule mti kuupeleka kwao....so wanapambana na matawi mpaka ukauke!
 
Huku kwetu kuna baba mmoja alijinyonga kwenye mti wa mwembe walishakata hiyo sehem mpk nikajiuliza ina kaz gan na sio mti tuu hata kamba aliyojinyongea mtu ni shida ,ngoja nisubir majibu
 
Unapoamua kujiua ni ujinga uliopitiliza.....wachawi uwa wanajua ulipojitolea roho na kumwaga damu....utakuwa umeacha damu yako na bahati tele.....hawawezi chimbua ule mti kuupeleka kwao....so wanapambana na matawi mpaka ukauke!
Kujinyonga so ujinga ni hali tu ya misukosuko inapozidi uwezo wa akili ya mtu ambayo inaweza kumkuta mtu yeyote ishu ni kumuomba mungu tu atuepushe! Simlaumu aliyejinyonga ila namuonea huruma tu
 
Hata waganga wakienyeji huzihitaji sana issue kama hizo siyo wachawi tu.
 
Kaswali kako ungekaelekeza kwanza kwa polisi make wakisikia raia kajinyonga wanakimbilia kuchukua kamba na hawairudishi kwa wafiwa eti ushahidi!!
 
Kujinyonga so ujinga ni hali tu ya misukosuko inapozidi uwezo wa akili ya mtu ambayo inaweza kumkuta mtu yeyote ishu ni kumuomba mungu tu atuepushe! Simlaumu aliyejinyonga ila namuonea huruma tu
Unapokaribisha mawazo ya kushindwa kulikabili jambo lililokukatiza shetani hukuletea roho ya kifo katika hali ya kutamani kujiua. Kama huna ulinzi au hujawahi kuwa na muongozo mzuri katika uhusiano wako na Mungu, roho hiyo hukujaa na wewe mwenyewe unaanza kuandaa mazingira y kulitimiza hilo jambo kadri hiyo roho ikuongozavyo. Once such a thought clicks your mind, what you need to do is to rebuke it and start fighting against the problem your facing respectively
 
Wana tumia.kuulia watu.hata mchanga wa sehemu MTU alipo gongwa akafa ni Mali.
 
Sikutegemea kuikuta humu maana juzi tu nilipouliza nilielezewa vizuri japo sikwa kina.

Majibu:
Kamba pamoja na mti huwa vinatumika kwa uchawi na inasemekana kuwa (watu wa ziwani wanalifahamu hiki) ukipata kipande kidogo tu hasa kwa wavuvi wa samaki unapokifunga katika nyavu ya kuvulia samaki huwa samaki wanakuwa wengi sana,pia hata kwa wafanya biashara unapoipata kamba au kipande cha huo mti basi huwa na uwezo wa kuwa na wateja wengi sana katika biashara yake.

(Kulingana na maelezo niliyopewa)

Naomba nishie hapo nisije haribu madili ya watu.
 
Wakuu habari za mda huu

Napenda kuchukua fursa hii adhimu ya kuwa mwanachama JF kujadili jambo pamoja na nyie wanajamii wenzangu.

Kuna siri gani kati ya wachawi na Mti uliotumika kujinyongea Mtu.

Kumekuwa na tetesi (kama si taarifa) kuwa mara nyingi sehemu alipojinyongea mtu utakuta matawi ya mti yule yamekatwa,

Jambo hili nimelifuatilia kwa mda kitambo ila majibu yake hayaridhishi,

Karibuni wenye ujuvi wa mambo haya.
Kamba alojinyongea mtu akafa hiyo ndo dili..!
Kuna dawa ikichanganywa inakuwa limbwata kali ambapo mkeo au mchepuko akikutengenezea ikatokea siku amekukataa lazima ujinyonge!
Pia kingine ni jiwe lililoua mtu,
Mfano mwizi kakimbizwa akaanguka kisha watu kuanza kushambulia wengine kwa mawe
sasa ikitokea akapigwa jiwe kichwani na kufa hapohapo hilo jiwe ni bonge la dili ila siwezi kusema leo ipo siku ntafafanua!
1. Jiwe lililoua
2.Nyumba au mti uliopigwa radi
3. Maiti ya mtoto mchanga chini ya siku 7
4.Nguo iliyodondoshwa na ndege
5.Fuvu la kichwa cha mwehu
6.kipande cha sanda ilotumika
7. Maji yaliyooshewa maiti
N.K
 
Sikutegemea kuikuta humu maana juzi tu nilipouliza nilielezewa vizuri japo sikwa kina.

Majibu:
Kamba pamoja na mti huwa vinatumika kwa uchawi na inasemekana kuwa (watu wa ziwani wanalifahamu hiki) ukipata kipande kidogo tu hasa kwa wavuvi wa samaki unapokifunga katika nyavu ya kuvulia samaki huwa samaki wanakuwa wengi sana,pia hata kwa wafanya biashara unapoipata kamba au kipande cha huo mti basi huwa na uwezo wa kuwa na wateja wengi sana katika biashara yake.

(Kulingana na maelezo niliyopewa)

Naomba nishie hapo nisije haribu madili ya watu.
yawezekana mie nilisikia kamba inatumika kwa wawindaji kutegea na wanapata kweli kwenye mitego yao.

pia mti ambao mama amejifungua hapo nao hukobolewa magamba na matawi kwa kazi zao za kishirikina.
 
Kamba alojinyongea mtu akafa hiyo ndo dili..!
Kuna dawa ikichanganywa inakuwa limbwata kali ambapo mkeo au mchepuko akikutengenezea ikatokea siku amekukataa lazima ujinyonge!
Pia kingine ni jiwe lililoua mtu,
Mfano mwizi kakimbizwa akaanguka kisha watu kuanza kushambulia wengine kwa mawe
sasa ikitokea akapigwa jiwe kichwani na kufa hapohapo hilo jiwe ni bonge la dili ila siwezi kusema leo ipo siku ntafafanua!
1. Jiwe lililoua
2.Nyumba au mti uliopigwa radi
3. Maiti ya mtoto mchanga chini ya siku 7
4.Nguo iliyodondoshwa na ndege
5.Fuvu la kichwa cha mwehu
6.kipande cha sanda ilotumika
7. Maji yaliyooshewa maiti
N.K
Shetani anapenda vitu used/mitumba!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom