Kuna siku tutaangalia alama ya Kila Rais aliyotuachia katika uongozi wake na hapo tutaelewa maono ya kila mmoja alipokuwa Rais yaliishia wapi.

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,542
3,451
Hakuna jambo la maana kama kuacha alama ya kudumu inayoleta faida katika maisha ya wengi.

Leo tunamuenzi Baba wa Taifa tukiiangalia misingi ya utangamano wa Kitaifa.
Nina uhakika tunamkumbuka kwa alama nzuri tunayoyaona na kushuhudia matunda yake.

Nimekuwa nikipipita eneo la Ubungo (junction) mara kwa mara ila leo nikiwa na rafiki yangu niliangalia ujenzi unaoendelea nikaiona alama inayochorwa chini ya utawala wa Rais wa wamu ya tano alama ambayo itasaidia kizazi kwa muda mrefu kuliko watu wangekula na kunywa vizuri leo na kuusahau mustakabali mzima wa kesho.

Naiona sura mpya kabisa ya Tanzania naona alama kubwa sana itakayodumu na kukumbukwa na kizazi hiki chute na kitakachofuata.

Naona matumizi ya kodi katika uhalisia wake na siyo tu nadharia ya matumizi ya kodi,alana hii inanipa matumaini mapya na kuamshwa ari na kasi ya kuwa mzalendo.

Nawaona Wakinamamama wajawazito na watoto wakitabasamu vijijini kutokana na uwepo wa huduma za afya ambazo licha ya changamoto nyingi bado maisha ya wengi yameokolewa.

Nawaona watoto wakipata elimu ya msingi na bure jambo ambalo limetunguzia mzigo mkubwa Wazazi na Walezi wa Watoto hao, simaanishi kama jambo hili lina kikamilifu wa asilimia mia moja ila naona nuru ya matumaini.

Nawaona Watoto wa miaka (0-5) miaka ambayo kiwango cha vifo ni kikubwa kuliko miaka mingine yote wakipewa huduma chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kwa hili sitoshangaa Serikali ikisema "HAWA NI WATU WANGU"kwa sababu imewalea vizuri na imewaandaa vyema.

Safari hii haiongozwi na Malaika ila inaongozwa na wanadamu wanaojitahidi kufikia ukamilifu na kwa msingi huo yapo madhaifu lakini hayazidi jitihada na nia njema.
 
Elimu bila Malipo, je imafanikisha ufaulu kwa wanafunzi au imeleta tija gani kwa stakeholders wote was Elimu?(mwalimu, mzazi na mwanafunzi)
Je ni bora kujenga Majengo mazuri ya kutolea huduma za afya wakati hakuna dawa na matabibu wa kutosha?
Juhudi zipo hatukatai lakini inabidi aangalie pande zote
 
Misingi hii iliwekwa tatizo nani aliweza kusimamia fedha kila MTU alikuwa mpigaji na jpm alijua kuziba mianya. Hivi kumwekea kila mteule wa jpm MTU wa kuangalia kufuatilia mpaka nyumbani anaishije mchezo, hii nchi ingepata akina magu 3 Japan I tufuate nini mifumo ya malipo serekalini kwa control number imesaidia Sana
.
 
Back
Top Bottom