G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Kwanza kabisa naomba nieleze kuwa baada ya kupata taarifa hizi za ghafla za kuhama Julius Mtatiro nilijiuliza sana kwanini? Baadaye nikagundua kuwa Mtatiro ameongea jambo moja la msingi sana kuwa "Sina jukwaa la kufanyia siasa kwa sasa" Hilo limemfanya ajione kuwa anapotea kisiasa akiwa bado kijana mdogo, uhuru wake umeminywa, hana jinsi. Anahitaji kujikuza kisiasa amebanwa mbavu na sasa hana jinsi.
Sasa basi hawa wanasiasa wanaohama upinzani wengi wao wamebanwa mbavu, wakitupiwa visenti kidogo tu wanayeyuka. Hata kina Tundu Lissu walipotaka kujinasua wakiwa huku upinzani waliishia kutwangwa risasi mchana kweupe tena hakuna kesi wala kuhoji na mbaya zaidi wala kuombea!
Hili linaonyesha wazi kuwa Rais Magufuli ni dikteta mbaya sana! Dikteta anayeiua Tanzania iliyokuwa imeanza kustawi kisiasa na Tanzania ya kuhoji! Huyu ni dikteta mbaya.
Naomba nimwambie wazi wazi Rais kuwa yeye alipatikana kirahisi sana kuwa mgombea wa CCM baada ya mtangulizi wake mzee JK kuruhusu serikali yake ichambuliwe, ikosolewe, ianikwe! Watuhumiwa wa ufisadi waliwekwa wazi, bunge liliwahoji na kupiga kelele hadharani. Hapa ndipo wanasiasa watarajiwa wa urais walianza kuonekana wachafu ndipo Magufuli akaibuka mbali na yeye kupewa uchafu wake. JK angekuwa mbinafsi kama alivyo Magufuli basi Urais angeusikia na kuuona maili milioni 100 kutoka alipo.
Sasa tunaona bunge halihoji tena, halipo huru, wanasiasa wanakosa majukwaa ya kisiasa huku chama dola kikitamalaki hapa kina Mtatiro lazima waibuke kama hawataweza kugangamala. Aibu ni kuwa leo Mtatiro anapokewa na yule yule aliyemsema kuwa ananunua wanaume wenzake! Asiogope kwani aibu ya upande huu kwa sasa ni dhaifu, aangalie tumbo lake. Zile siasa zake za face book na Twitter anaenda kuzitazama sijui tasemaje?
Sasa basi niitaadharishe hii CCM manunuzi kuwa walioenda huko wanaenda kutokana na kukosa namna. Huyu mtawala leo yupo kesho hayupo! Namna itarudi. CCM hii itavunjika vunjika, itapata shida sana.Kutakuwa na mparanganyiko mkubwa hapo mbele, najua wapo watakaobisha sasa ila tuombe uzima muda ambao si mrefu utakuja!
Hivi Kafulila, Mtatiro, Machali na wengine wanaunga mkono juhudi gani? Za rais kuonekana TBC kila mara? Maana aliyepita alikuwa hana huo muda! Za haya makelele tunayoyasikia kila mtendaji na kelele zake? Maana aliyepita alikuwa hana huo muda.
Nadhani gesi ya Mtwara ingegundulika kipindi cha Magufuli basi tusingelala maana wangehama kwa angalau kigezo kuwa "Amegundua gesi" "Wenzake walikuwa wanaikalia tu" Maana kama mtu anahama eti anasema kuwa Rais ameleta umeme wa Stiglers? Kweli? Eti amenunua ndege? Zinarejesha fedha zetu? Maana tulinunua kwa fedha zetu! Sasa kipi? Na hizo ndege angepewa bure si ndo tungewaomba wakenya wahamie Tanzania kuunga mkono juhudi?
Lakini pia tunapata funzo sasa kuwa watanzania wengi sana hawajaweza kujisimamia, kama hawa ambao wanaonekana afadhali wako tayari kujiacha utupu, vipi kwa wale kajamba nani? Tunapata ujumbe kuwa Tanzania bado haijawa na wanasiasa wengi waliokomaa. Ni aibu mtu anahama chama na hata kuuacha ubunge eti kwenda kuunga mkono Rais kujenga barabara! Aibu aibu! Lakini haya yote ni baada ya mbinu za kidikteta kutumika.