Kuna sababu ya wajasiriamali kuunganisha nguvu zetu pamoja

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,375
3,654
Habari za humu JF,

Hali ya maisha kwa Wajasiriamali walio wengi Tanzania hayakidhi viwango vya malengo yao mengi waliyojiwekea hivyo wajasiriamali hawa wadogo wadogo wanakua wapo vile vile na miradi yao miaka nenda miaka rudi bila kupiga hatua mbele zaidi.

Ukiuliza maendeleo ya miradi ya wajasiriamali hawa kamwe hawakosi jibu kwa sababu imezoeleka ujasiriamali ni kama kiswahili fulani kireeefu hivi, Maneno mengi vitendo ziro.

Nawaasa wajasiamali kufikiri zaidi juu ya kuunganisha mitaji yao ili iwe na nguvu katika Soko.
Kwa mfano wakitokea wajasiamali( 100)Wakaunganisha nguvuzao kila mmoja ajiunge na 2M tunaona kwamba hawa watakua na mtaji wa M200.

Huu mtaji wa M200 mnaweza kufungua Biashara moja yenye nguvu katika soko na mkapata kutoa ajira kwa vijana wengine zaidi ya 100-utajiri wa mabilioni ndani ya muda mfupi kuliko kila mmoja kwenda katika soko na mtaji wa M2 hapa tunapoteza tuunganishe nguvu na wengine wenye nia ya kujikomboa kuifanya kesho iliyo nzuri.

Ukingia katika mitandao utashuhudia vijana wa rika la kati wanalalama kuhusu kupata mitaji na kukosa ajira lakini katika hayo hakuna ambae anaewaza kuunganisha nguvu zake na wengine ili wawe na nguvu soko la mitaji.

Vijana sasa ni wakati wa kuamka tuunganishe nguvu zetu tuzifuate ndoto zetu.

Nakaribisha Mawazo yenu.
 
Wazo zuri Ila linahtaji upembuz yakinifu hasa kwenye uaminifu na kulinda mitaji ya watu , sambamba na hlo niwepo na wazo la mradi wenye Tija , hapa wizara pia zinahusika kuainisha maeneo ya uwekezaji. Tatizo viongozi wetu wameunga unga Elimu, hawana lolote Zaid ya kuangalia Nani anapata wapi kiurahsi ili tumgonge nyundo.
 
Lakini mkuu si wote wako hivyo, Kuna wale wenye nia hasa hasa hawa hawawezi kuwa kama hao unaowaelezea istoshe mkifanikiwa kufanya biashara ni lazima mfuate taratibu za mikataba ili kusiwepo udanganyifu.
Eti eeeh haya nakutakia mafanikio mema
 
Wazo zuri Ila linahtaji upembuz yakinifu hasa kwenye uaminifu na kulinda mitaji ya watu , sambamba na hlo niwepo na wazo la mradi wenye Tija , hapa wizara pia zinahusika kuainisha maeneo ya uwekezaji. Tatizo viongozi wetu wameunga unga Elimu, hawana lolote Zaid ya kuangalia Nani anapata wapi kiurahsi ili tumgonge nyundo.
Watu wataoweza kufanya hivyo ndio watakaofanikiwa mapema zaidi kuliko kila mmoja wetu aende sokoni na bidhaa pungufu wakati wakiungana wanaweza kufanya zaidya hapo.
 
Umeona hadi mabenki yanaungana ili kuongeza nguvu kutokana na hali mbaya ya uchumi.....wenye biashara zinazofanana wanaweza ungana kutengeneza kampuni moja kubwa kufanya biashara hiyo hiyo ....vikundi vingi vya wabongo vilivyoundwa asilimia kubwa vilishakufa kutokana na userious mdogo,kutapeliana na sababu kedekede ,na vingine vilivyopo vimebaki kukopeshana na havina miradi...vipo vichache vyenye project's but vingi ni majanga
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom