Kuna sababu ya kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa tanzania bara?

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Hivi sasa Zanzibar inaongozwa na serikali ya umoja wa Kitaifa kati ya Chama cha Mapinduzi , CCM na Chama cha Wananchi , CUF. Je kuna sababu ya msingi kuwa na serikali ya aina hiyo Tanzania bara?
Toa maoni yako.
 
Wewe maoni yako ni yepi? Unapoleta hoja jaribu kuipa nyama kwa kuitetea au kuikosoa. Ukiacha skeleton kama hii utaambulia matusi tu mdogo wangu.
 
Hivi sasa Zanzibar inaongozwa na serikali ya umoja wa Kitaifa kati ya Chama cha Mapinduzi , CCM na Chama cha Wananchi , CUF. Je kuna sababu ya msingi kuwa na serikali ya aina hiyo Tanzania bara?
Toa maoni yako.

Kichekesho hicho tena. Jamani mimi ninavyoelewa ni kwamba Zanzibar ni lazima kuwe na serikali ya umoja wa kitaifa kwa vile katika matokeo ya uchaguzi, CCM na CUF walikuwa wanazidiana kwa idadi ndogo sana ya wabunge na hata katika kura za urais tofauti ya kura ilikuwa ni ndogo sana kwa takribani chaguzi nyingi. Kwa Tanzania bara mambo ni tofauti kabisa . Kwa urais CCM ilishinda kwa asilimia 61% wakati mpinzani wake wa karibu akipata asilimia 22% . Aidha CCM walikuwa na wabunge zaidi ya 200 wakati wapinzani wao, CHADEMA walikuwa na wabunge chini ya 50. Kwa mawazo yangu ni kwamba Tanzania bara Serikali ya umoja wa kitaifa haina nafasi kwa sasa , na nadhani sijui kama niko sahii , Katiba hairuhusu serikali ya aina hii, labda liingizwe kwenye mjadala wa katiba mpya ili kwa baadaye kama kuna ulazima wa kuwa serikali ya mseto, basi katiba iwe inaruhusu.
 
Back
Top Bottom