kuna sababu ya kufuatilia background ya wapenzi wetu?

Mapenzi kabla ya ndoa ni kama gari inapopita kwenye round-about, kila mtu ana-keep left. Hivyo ukitaka kujua idadi na aina ya magari yaliyokwisha pita kabla yako ni kutaka kuumiza kichwa bila sababu.
 
Kwa hivyo just fumba macho, ukipata mke mzuri (wa sura na tabia) utakuwa na furaha, lakini ukipata mke mbaya (wa sura na matendo) basi utageuka philosopher jambo ambalo pia ni kheri..........!
 
Hakuna ulazima wa kufuatilia, lakini kama mpenzi wako ataamua mwenyewe kukueleza unaweza ukamsikiliza kwa sababu inawezakufanya mapenzi yenu yakawa strong.
 
Yaani wewe unataka kujua flani ndo alikuwa anampitia mke wako duh! mzee hutaumia?
Kama mvumilivu basi muulize akutajie na wengine usikute walisha chomoka kwa miwaya.
 
sikushauri ufanye hivyo, pale mnapoanzana urafiki wa kimapenzi ndipo hapo hapo na wewe uanze kuchuja yako, ukisema ufatlie hata kama alicheza rafu mahali hataweza kukuambia ukweli! ki ujumla mtadanganyana, kwani wewe unaweza kumwambia kwamba wewe ni mwanamke wa 16 kwangu? hivyo hivyo na yeye atakueleza wewe ni wa pili wa kwanza walitengana coz alienda ULAYA kimasomo...lol
 
wewe SIPO naomba kujua jinsia zako.
inawezekana unatafuta Mume na sisi tunajua namna ya kukushauri VYEMA kabisa namna ya kujitutumua kufikia malengo.
Ila si unajua kwa kila twisheni hulipiwa na bure ghali?
 
mbona mnapenda kufatilia tu mambo ya mechi za hapo zamani.... kama ni background infor I would be more interested in any genetic disorders katika familia yake ambazo zaweza kuleta nuksi baadaye!!! ya nani kamla/kaliwa na nani yatafaidi nini????
 
Ndugu wana jamvi kuna sababu ya kujua mpenzi wako unayetaka kumuandaa kuwa my wife au my husband alikuwa anaishije kwenye maisha yake ya kimapenzi hapo nyuma. Tusaidiane maana nataka kuingia katika maisha ya ndoa lakini bado sijampata wa kumoyo.

NB: Wana JF inawezekana hii thread ilishajadiliwa hapo nyuma lakini TAFADHALINI tusaidiane tena kimawazo wanajamii wenzangu!!

USIJARIBU HILO NIPO..

La, kama unataka mchumba ambaye ni perfect, basi nenda kwa wale

jirani zako wamakonde, au fundi MHUNZI, AU MFINYANZI

akamchonge wa hivyo!! MIMI nina taaluma ya masuala ya ndoa

na jinsia, nitafute private nikushauri.

Kimsingi, wewe na mchumba wako mna uwezo wa juu kabisa wa

kuanzisha au kutunga maisha mapya mnayotaka kuyaishi...Lakini

suala la kufuatilia maisha ya nyuma Halipo!! Kinachotakiwa ni kuwa

AIDS-FREE!! Ndo maana hata makanisani wachumba wanatakiwa

kuleta vyeti vya Daktari vya vipimo vya UKIMWI, mambo mengine

hayajalishi... umenipata?

KARIBU KWENYE TAASISI HII NYETI...!!
 
Ndugu hupo, usimchunguze bata sijui baba/mama hutomla, muombe mola wako akujalie umpate mtakae randana.
 
Haifai kabisa na wala usithubutu. Wewe cha msingi ujue tu kuwa aidha umemkuta mkeo tayari kabanjuliwa au la. Na nina uhakika hutakuwa na **** za kutafuta mke bikira, labda kama nawe hujawahi kubanjua (bahati mbaya mwanamke hataweza kuthibitisha kama umewahi au la), inatosha. Hayo mengine, sijui nani alikuwa anafaidi, sijui nani alimbikiri mke wangu haitakusaidia lolote zaidi kukuongezea msongo wa mawazo.

Mimi nashauri hata suala la sijui mmoja kiamua kumsimulia mwingine mimi nadhani ni kulikataa mapema kabisa kwamba ajenda hiyo haifai na isipewe nafasi katika uhusiano wenu.
 
Ndugu kuwa mwangalifu kama una taka mwenza, mkubali mwenzako kitabia,umbile,matarajio yake uyakubali pia kama atakwambia,pokea ushauri toka kwa jamii inayokuzunguka baada ya kuwashirikisha juu ya mpendwa wako na la mwisho kama mna imani/dini ni vizuri mkafanana. Usisahau elimu,walau ajue kusoma vibao vya daladala.
 
Usimchunguze muulize point blank kuwa kama yupo ok na wewe na at least partner wake wa mwisho alimalizana naye kivipi kisha ishia hapo usitake kuwajua wote, by any means do not dig too far coz no one is perfect but at least one previous partner can tell you what type of a partner a.k.a mpenzi he/she is.

Methali zetu za kiswahili zinasema kuwa ukimchunguza sana bata........
 
Kama walivosema Nyamayao,Shishi na Penny we anzia hapo mnapofahamiana ya huko nyuma yaache yalivyo mtaishi kwa amani ukitaka kujua ya zamani utaumia na pia itadhihirisha hujiamini.
 
umeamua kweli kutomchimbua sana huyo mpendwa wako na mambo yamekuwa safi. Mmefunga ndoa vizuri.Kidudu mtu kakwambia mwenza wako alikuwa anagawa tigo kama hana akili vizuri au siku ya kujifungua kule Muhimbili ikagundulika alikuwa anatoa tigo na Nesi ndo anakwambia sokomeza tambala ili ajifungue salama utafanyaje?

Wanajamvi,ni kumwomba Mungu akujalie kupata mwenza safi.
 
sasa shida yote ya nini si bora usioe tuu...wanakuambua "what you don't know wouldn't hurt you"
 
Ndugu wana jamvi kuna sababu ya kujua mpenzi wako unayetaka kumuandaa kuwa my wife au my husband alikuwa anaishije kwenye maisha yake ya kimapenzi hapo nyuma. Tusaidiane maana nataka kuingia katika maisha ya ndoa lakini bado sijampata wa kumoyo.

NB: Wana JF inawezekana hii thread ilishajadiliwa hapo nyuma lakini TAFADHALINI tusaidiane tena kimawazo wanajamii wenzangu!!

Je una hamu ya kujua background ya mpenzi wako?; na
Je upo tayari kuoa bila kujua hiyo background?(can you live without the knowledge of this history?);na la muhimu,
Je, unao uwezo wa ku-probe na kupata hiyo background ya mwenza wako?

Ni kweli kuna mambo mengine kwa kuyajua kwake hayasaidii kujenga uhusiano wenu.Lakini yapo mambo kadhaa ambayo ni muhimu kuyafahamu kabla hujaaamua kuingia kwenye ndoa.


Nitatoa mifano michache (wengine wanaweza kuongezea!);
  • Mpenzi wako ameoa/ameolewa? alishawahi kuoa/kuolewa? ameachika? nk(Hili ni muhimu sana. Nimeshuhudia mara kadhaa wanawake wanaingia kwenye ndoa ya mitala bila kujua au mwanaume anaoa mke wa mtu!)
  • Je mpenzi wako ana mtoto/watoto? (Ni hatari sana kulijua hili baada ya kuingia kwenye ndoa)
  • Fahamu pia familia ya mwenzio (kaka, dada zake nk). Kuna wengine unaweza ambiwa ni dada kumbe ni wake wenza! nk nk
  • Ni vema ukajua elimu ya mwenza wako (kuna ndugu yangu mmoja alioa mwanamke asiyejua kusoma wala kuandika- yeye ali assume mwanake ni literate!. Hakujua hili mpaka walipofika madhabahuni!)
 
Ndugu wana jamvi kuna sababu ya kujua mpenzi wako unayetaka kumuandaa kuwa my wife au my husband alikuwa anaishije kwenye maisha yake ya kimapenzi hapo nyuma. Tusaidiane maana nataka kuingia katika maisha ya ndoa lakini bado sijampata wa kumoyo.

NB: Wana JF inawezekana hii thread ilishajadiliwa hapo nyuma lakini TAFADHALINI tusaidiane tena kimawazo wanajamii wenzangu!!

Ukimchunguza bata utashindwa kumla,la muhimu angalia FANTASY zenu zina owana.
 
Kuna watu wengine wana wivu wa ajabu sana. Kama unataka mke au mume ambaye ni bikira :) basi wapo kibao! we tangaza tu unataka bikira basi utapata maelfu ya watu kisha utafanya uchaguzi wako. Umchunguze mke/mume wako ili kujua katembea na watu wangapi ili iweje? halafu ukishajua itakusaidia nini? Bora ungesema woote mchunguze afya zenu ili kuhakikisha hamjangusa miwayawaya kabla ya kuingia kwenye ndoa yenu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom