Kuna saa unaweza usijisifie kuwa Mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna saa unaweza usijisifie kuwa Mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eeka Mangi, Nov 18, 2011.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kuna wakati mwingine huwa najisikia vibaya sana kujivunia Utanzania wangu! Kwenye macho ya wengi huwa tunaonekana watu wenye amani sana! Kiukweli sivyo!
  Nimeangalia ITV leo kule Meatu! Askari anapiga watu mabomu anawasha kibiriti kuchoma nyumba ya mtanzania mwenzake huku wamekamata AK47 as if wale ni waasi wa kivita! Yet we are saying nchi ya amani. Hivi wale Watanzania wamependa kukaa kule porini jamani. RC, DC na viongozi wa Shinyanga na Meatu wameenda kufanya nini kule? Kukaa maofisini na kucheza karata kwenye computer tu! Siku hawa wahanga wakiamua kukataa manyanyaso wanayoyapata toka serikali yao mtasema waasi?
  Tuwe na huruma na wenzetu.
  Iko siku moja hawa watu wataadhibiwa ama kukutana na gadhabu ya Mungu kwa kuwatesa viunbe wake
   
Loading...