Kuna raha gani mnaipata kwenye bia/pombe?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,672
Ijumaa nilikuwa kwenye bar moja inaitwa TAXIDO, Nikiwa mwenye mawazo
tele niliona hiyo kama ni sehemu Muafaka ya kupunguza mawazo kwani kila
Ijumaa huwa kuna LIVE BAND zinapiga hapo na nyimbo zao nyingi huwa
zilipendwa.

Nikiwa hapo niliagiza Nyama choma ya mbuzi ambayo ilikaushwa vizuri kwenye
moto na wataalamu wa kuchoma nyama, niliwekewa pilipili ya kutosha ndimu na
Kachumbari iliyotengenezwa kwa ustadi mkubwa sana nikashushia kwa Soda.

Katika kaa yangu ya hapo niligundua wanywaji wa Bia/pombe walikuwa na
Furaha sana, yaani wengi walichangamka tofauti na nilivyowaona wakati wanaingia.
Halafu ni watu naona kama wanajiamini katika mazungumzo ya mipango yao.

Naomba nifahamishwe Uzuri unaopatikana kwenye Bia kabla sijakata shauri ya kuanza
kunywa. Kiukweli natamani Ijumaa Ijayo nianze angalau na Bia tano au ile Chupa
ndogo ya Konyagi.

Vipi kuna ubaya wowote kuanza unywaji wakati nishakuwa Mtu mzima hivi?
 
Ijumaa nilikuwa kwenye bar moja inaitwa TAXIDO, Nikiwa mwenye mawazo
tele niliona hiyo kama ni sehemu Muafaka ya kupunguza mawazo kwani kila
Ijumaa huwa kuna LIVE BAND zinapiga hapo na nyimbo zao nyingi huwa
zilipendwa.

Nikiwa hapo niliagiza Nyama choma ya mbuzi ambayo ilikaushwa vizuri kwenye
moto na wataalamu wa kuchoma nyama, niliwekewa pilipili ya kutosha ndimu na
Kachumbari iliyotengenrzwa kwa ustadi mkubwa sana nikashushia kwa Soda.

Katika kaa yangu ya hapo niligundua wanywaji wa Bia/pombe walikuwa na
Furaha sana, yaani wengi walichangamka tofauti na nilivyowaona wakati wanaingia.
Halafu ni watu naona kama wanajiamini katika mazungumzo ya mipango yao.

Naomba nifahamishwe Uzuri unaopatikana kwenye Bia kabla sijakata shauri ya kuanza
kunywa. Kiukweli natamani Ijumaa Ijayo nianze angalau na Bia tano au ile Chupa
ndogo ya Konyagi.

Vipi kuna ubaya wowote kuanza unywaji wakati nishakuwa Mtu mzima hivi?
Hahahahaaaaa usituzuge, kwa namna ulivyoandika wewe ni wakala wa kilaji aisee!

Ila beti ya kwanza nime salivate!....mbaya zaidi mwishoni ukatupia tumaneno twa kujazia mate mdomoni kwamba utaanza na tubia tutano tu! ......wewe jamaaa ni mzoefu maeneo ya kilaji na hata hapo TAXIDO
 
Ha ha ha ha Hapana Mkuu kama bia Tano ni nyingi nifafanuliea maana siku ile kuna meza ilikaa
njemba fulani na wadada nahisi walimaliza Kreti 2.
 
Maandiko yote ya dini uislam na ukristo yamekataza ulevi.....Pombe ni mpango wa Shetani kuitawala dunia...Tito ni nabii wa shetani
Ok nimekuelewa Mkuu, Baba yangu Mkubwa alikuwa Padre wa Kanisa katoliki Jimbo
Fulani na alikuwa anapiga pombe vizuri, sijui kama alikuwa anafanya hivyo kimakosa
au...... Sina la kusema naye ni Binadamu labda alikuwa anakosea angekuwa hai ningemuuliza.
 
Back
Top Bottom