Blasio Kachuchu
Senior Member
- Sep 7, 2016
- 152
- 111
Wakati serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya viwanda kufanikisha ajenda yake ya Tanzania ya viwanda, bado kuna dalili za sekta hiyo badala la kukua na kuwainua Watanzania baadhi ya makampuni yana muelekeo wa kuwakandamiza wafanyakazi wake Watanzania na kunufaisha raia wa kigeni.
Moja ya kampuni kubwa nchini ambayo hivi sasa inawanyima fursa wafanyakazi wake wazawa, wasomi na wenye uzoefu wa kazi na kukumbatia wageni ni Tanzania Breweries Limited (TBL), chini ya kampuni ya ABInBev.
Kampuni imefikia hatua ya kuajiri raia kutoka Afrika Kusini kuongoza vitengo vya Logistic, Mauzo na Masoko, wakati kuna Watanzania wengi wengi ujuzi na uzoefu wa fani hizo. Jambo la kujiuliza raia wa kigeni ambaye hata hajui jiografia ya nchi hii atawezaje kusimamia uuzaji wa bia katika mikoa, wilayani mpaka vijijini ambako wapo watumiaji wa bidhaa za kampuni?
Mbona kuna makampuni mengi nchini kama Azam, MO, viwanda vya soda nk. unakuta bidhaa zake zinapatikana mpaka vijijini na kazi ya usambazaji na masoko inafanywa na watanzania?na hata TBL inao wenye ujezi. Suala la kuuza bia ndilo waswahili wanaonekana hawana uwezo, wageni wanaotambua maeneo kwa kutumia ramani za Google ndio watajua? au kuna ajenda ya siri ya kuua viwanda na kutorosha fedha nje ya nchi kwa urahisi?
Baadhi ya wafanyakazi wa kigeni TBL, ambao wamekabidhiwa jukumu la kuongoza vitengo wakati watanzania wenye sifa na ujuzi wa kufanya kazi hizo ni Lise Kruger (Afrika ya Kusini)-Logistic Director, Doreen Tumureebile (Afrika ya Kusini)-Mkurugenzi wa Mauzo,na Uendelezaji wa Masoko,Bruno Zambrano, amekuwa akifanya kazi kama Mkuu wa Kitengo cha fedha japo amekuwa akitambulishwa kama Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara .Pia yuko Mkurugenzi wa Masoko , Neil Hobkirk, ambaye amekuwa akifika nchini mara kwa mara kama mtalii kufuatilia masuala ya masoko kama vile hapa nchini hakuna mtu kwa kufanya kazi hizo.
Swali la kujiuliza wageni kama hawa ambao wanakuja kufanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania nani anawapatia vibali vya kufanya kazi nchini?.Uhamiaji mko wapo? NBAA mkoa wapi?
Wakati umefika wa Serikali kuwa macho na wawekezaji ambao wanaangalia zaidi maslahi yao na kukandamiza watanzania, na kuwakatisha tamaa sambamba na kuua taaluma zao.
Baadhi ya wawekezaji wanakuja na kivuli cha uwekezaji wakati wanafanya ulaghai na kunufaika na raslimali walizozikuta, mfano mwekezaji anayeendesha kiwanda hiki tangu aingie nchini amekuwa akiongelea suala la kujenga kiwanda cha bia mkoani Dodoma, lakini hadi sasa hakuna chochote kinachoendelea.