Kuna nini TBL? Ajira za wazawa mashakani

Blasio Kachuchu

Senior Member
Sep 7, 2016
152
111
Wakati serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya viwanda kufanikisha ajenda yake ya Tanzania ya viwanda, bado kuna dalili za sekta hiyo badala la kukua na kuwainua Watanzania baadhi ya makampuni yana muelekeo wa kuwakandamiza wafanyakazi wake Watanzania na kunufaisha raia wa kigeni.

Moja ya kampuni kubwa nchini ambayo hivi sasa inawanyima fursa wafanyakazi wake wazawa, wasomi na wenye uzoefu wa kazi na kukumbatia wageni ni Tanzania Breweries Limited (TBL), chini ya kampuni ya ABInBev.

Kampuni imefikia hatua ya kuajiri raia kutoka Afrika Kusini kuongoza vitengo vya Logistic, Mauzo na Masoko, wakati kuna Watanzania wengi wengi ujuzi na uzoefu wa fani hizo. Jambo la kujiuliza raia wa kigeni ambaye hata hajui jiografia ya nchi hii atawezaje kusimamia uuzaji wa bia katika mikoa, wilayani mpaka vijijini ambako wapo watumiaji wa bidhaa za kampuni?

Mbona kuna makampuni mengi nchini kama Azam, MO, viwanda vya soda nk. unakuta bidhaa zake zinapatikana mpaka vijijini na kazi ya usambazaji na masoko inafanywa na watanzania?na hata TBL inao wenye ujezi. Suala la kuuza bia ndilo waswahili wanaonekana hawana uwezo, wageni wanaotambua maeneo kwa kutumia ramani za Google ndio watajua? au kuna ajenda ya siri ya kuua viwanda na kutorosha fedha nje ya nchi kwa urahisi?

Baadhi ya wafanyakazi wa kigeni TBL, ambao wamekabidhiwa jukumu la kuongoza vitengo wakati watanzania wenye sifa na ujuzi wa kufanya kazi hizo ni Lise Kruger (Afrika ya Kusini)-Logistic Director, Doreen Tumureebile (Afrika ya Kusini)-Mkurugenzi wa Mauzo,na Uendelezaji wa Masoko,Bruno Zambrano, amekuwa akifanya kazi kama Mkuu wa Kitengo cha fedha japo amekuwa akitambulishwa kama Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara .Pia yuko Mkurugenzi wa Masoko , Neil Hobkirk, ambaye amekuwa akifika nchini mara kwa mara kama mtalii kufuatilia masuala ya masoko kama vile hapa nchini hakuna mtu kwa kufanya kazi hizo.

Swali la kujiuliza wageni kama hawa ambao wanakuja kufanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania nani anawapatia vibali vya kufanya kazi nchini?.Uhamiaji mko wapo? NBAA mkoa wapi?

Wakati umefika wa Serikali kuwa macho na wawekezaji ambao wanaangalia zaidi maslahi yao na kukandamiza watanzania, na kuwakatisha tamaa sambamba na kuua taaluma zao.

Baadhi ya wawekezaji wanakuja na kivuli cha uwekezaji wakati wanafanya ulaghai na kunufaika na raslimali walizozikuta, mfano mwekezaji anayeendesha kiwanda hiki tangu aingie nchini amekuwa akiongelea suala la kujenga kiwanda cha bia mkoani Dodoma, lakini hadi sasa hakuna chochote kinachoendelea.
 
Blasio Kachuchu,

Mkuu pole kwa yanayowakuta, badala ya kulalamika kuhusu hao jamaa kujenga kiwanda cha bia huko Dodoma, ilihali anawapa watu wa nje kazi badala ya wazawa, ni vyema mkajipanga nyie wazawa mkajenga hicho kiwanda cha bia, tena ikibidi mjenge hicho kiwanda na waziri wa viwanda ili atekeleze sera yao vizuri. Hao wazungu wanatajua hivyo sehemu nyeti wanawapa wenzao maana wanajali kazi. Nani ataajiri mtu kila mwezi anaenda kuzika, mara kupiga deal na uhuni wa aina hiyo? Fungueni cha kwenu wazawa mpige siasa na gawio mtoe serikalini.
 
Watanzania saa nyingine tumezidi,uvivu ,kutokujituma ,wizi nk.Ila sio wote bado kuna watu waadilifu na wachapa kazi.Sasa huwa najiuliza serikali huwa inatoaje "work permit" kwa watu wengi hivyo kwenye kiwamda kimoja.Kwanza kutokana na utandawazi ,TBL ingekuwa inwaweka watu hukohuko walipo kwa Kuwa wakuu wa vitengo na hapa nchini wakaweka watanzania kuwa chini yao bika kutakiwa kuja Tanzania.Wamerikani huo wanatumia hii system sana.
 
Sheria ya kubana hayo mambo ipo japo siikumbuki vizuri kuna nafasi chache ndio zinatakiwa zishikwe na wageni
Na hata hizo work permit zina mda nahisi sio zaidi ya miaka 3
 
Blasio Kachuchu, We are so keenly with industry developments,what we can say is HONGERA SANA RAIS MAGUFULI,we works only with targets as a normal situation to any one who wish or will to perform well,Hatutaweza kuwavumilia watu wasioweza kuendanda na kasi yetu/
Asante sana sana,majita fresh,kama kawa kama dawa.
 
Viwanda vya bia sasa hivi viko ktk ushindani wa hali ya juu.Sasa ktk kitengo cha Marketing lazima waweke watu wenye uwezo hasa,sidhani kama ni issue ya ubaguzi wa rangi au uzalendo.

Binafsi huwa naona katika watu ambao hawahitaji kulalamikia ajira ni watu wa Marketing.Kwasababu biashara nyingi zinahitaji kuuzwa/masoko,kama unauwezo wa kitafuta masoko/kuuza tayari una ajira.
 
Mkuu wachaga na wakaskazini wengine wamekuwa retrenched ama.

Katika shirika lilijaa bwashee ni TBL. Kuanzia management mpaka madereva trucks wote meku aisee.

Huu uzaifu upo Tanzania tuu. Hata Uganda huwezi kwenda kuwekeza halafu ukajaza wageni makaburu watanyimwa vibali.

Kuna njia nyingi za kuwabana wasijae ikiwemo kuverify vyeti vyao TCU, Succession plan, kupewa vibali vya mwaka mmojammoja na kuwanyima vibali. Lakini Kama wanaingilia mlango wa TIC halafu wawe na wings Kama wawekezaji wachina wanavyofanya Basi utaona mpaka storeman atakuja mkaburu.

This shows somebody at Ministry of labour hafanyikazi ipasavyo au anachukua bahaasha chini ya meza.
 
Wakati serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya viwanda kufanikisha ajenda yake ya Tanzania ya viwanda, bado kuna dalili za sekta hiyo badala la kukua na kuwainua Watanzania baadhi ya makampuni yana muelekeo wa kuwakandamiza wafanyakazi wake Watanzania na kunufaisha raia wa kigeni.

Moja ya kampuni kubwa nchini ambayo hivi sasa inawanyima fursa wafanyakazi wake wazawa, wasomi na wenye uzoefu wa kazi na kukumbatia wageni ni Tanzania Breweries Limited (TBL), chini ya kampuni ya ABInBev.

Kampuni imefikia hatua ya kuajiri raia kutoka Afrika Kusini kuongoza vitengo vya Logistic, Mauzo na Masoko, wakati kuna Watanzania wengi wengi ujuzi na uzoefu wa fani hizo. Jambo la kujiuliza raia wa kigeni ambaye hata hajui jiografia ya nchi hii atawezaje kusimamia uuzaji wa bia katika mikoa, wilayani mpaka vijijini ambako wapo watumiaji wa bidhaa za kampuni?

Mbona kuna makampuni mengi nchini kama Azam, MO, viwanda vya soda nk. unakuta bidhaa zake zinapatikana mpaka vijijini na kazi ya usambazaji na masoko inafanywa na watanzania?na hata TBL inao wenye ujezi. Suala la kuuza bia ndilo waswahili wanaonekana hawana uwezo, wageni wanaotambua maeneo kwa kutumia ramani za Google ndio watajua? au kuna ajenda ya siri ya kuua viwanda na kutorosha fedha nje ya nchi kwa urahisi?

Baadhi ya wafanyakazi wa kigeni TBL, ambao wamekabidhiwa jukumu la kuongoza vitengo wakati watanzania wenye sifa na ujuzi wa kufanya kazi hizo ni Lise Kruger (Afrika ya Kusini)-Logistic Director, Doreen Tumureebile (Afrika ya Kusini)-Mkurugenzi wa Mauzo,na Uendelezaji wa Masoko,Bruno Zambrano, amekuwa akifanya kazi kama Mkuu wa Kitengo cha fedha japo amekuwa akitambulishwa kama Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara .Pia yuko Mkurugenzi wa Masoko , Neil Hobkirk, ambaye amekuwa akifika nchini mara kwa mara kama mtalii kufuatilia masuala ya masoko kama vile hapa nchini hakuna mtu kwa kufanya kazi hizo.

Swali la kujiuliza wageni kama hawa ambao wanakuja kufanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania nani anawapatia vibali vya kufanya kazi nchini?.Uhamiaji mko wapo? NBAA mkoa wapi?

Wakati umefika wa Serikali kuwa macho na wawekezaji ambao wanaangalia zaidi maslahi yao na kukandamiza watanzania, na kuwakatisha tamaa sambamba na kuua taaluma zao.

Baadhi ya wawekezaji wanakuja na kivuli cha uwekezaji wakati wanafanya ulaghai na kunufaika na raslimali walizozikuta, mfano mwekezaji anayeendesha kiwanda hiki tangu aingie nchini amekuwa akiongelea suala la kujenga kiwanda cha bia mkoani Dodoma, lakini hadi sasa hakuna chochote kinachoendelea.
Idumu serikali ya awamu ya 5 chini ya Mtukufu Dr. John Pombe Joseph Magufuli
 
Masharti ya mgeni kupata work permit pamoja na kwamba ujuzi wake uwe haupatikani hapa nchini. Sasa kama ni kweli mtu wa Logistic na Marketing ni mgeni hapo siyo sawa. Nafikiri Idara ya Kazi watafanyiakazi malalamiko haya ikitiliwa maanani juzi tu Mwanajeshi ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kazi.

Kwa nafasi za directors, inaruhusiwa kampuni kuajiri nje
 
Back
Top Bottom