Kuna nini nyuma ya huu mpango?

SIPIYU30

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,616
2,012
Nimefahamiana na dada mmoja,
Kila siku akawa ananitumia ujumbe mfupi kwenye simu yangu, i miss u, nikadhani kawaida. Baadaye akanitafuta facebook, Jambo moja alilogundua bila hata kuniuliza, nina watoto wawili ambao picha zao nimeweka facebook. Jana jioni akanitumia msg, kumbe una watoto wawili? nikajibu ndiyo.

Baadaye akanitumia message kuwa ana ombi moja kwangu. Nikadadisi ni ombi gani hilo? Akasema nataka mtoto unizalie, kama niko tayari tukapime then nimpe ujauzito basi, nikamwambia nina familia, akasema hataki ndoa, wala hataki mimi nimlee mtoto, anachotaka ni mimba tuuu. Kilichonishangaza hatujajadili mambo ya mapenzi, hatujajadili mambo ya kusema "i love you" sasa from "i miss you" to "nataka unipe mtoto" imenishangaza kidogo.

Nimeshindwa kumjibu lolote, kwani kuna agenda gani nyuma ya pazia?
Nimemhoji kwani huna mume? akasema ana mchumba lakini kwa kuwa hajamuoa bado, yeye ana maamuzi yake mwenyewe na maisha yake na haingiliwi na mtu.

Leo asubuhi nimefungua facebook, nimekuta ameweka comment kwenye picha za watoto wangu "hongera sana kwa watoto wazuri sana.."

Nimeshindwa kumwelewa, anataka kunitega kwa mimba ili baadaye avuruge ndoa yangu? au amevutiwa sana na watoto wangu kiasi cha yeye kutamani kuwa na watoto kama wangu, na hatima yake ni nini?
 
Acha tamaa wala haina haja hata ya kufikiria mtoto ni muunganiko ambao hautaweza kuukwepa milele
 
Peleka mbegu KAMANDA sasa unashindwa nini kuweka naye mkataba kwa mwanasheria. Huenda dogo akaja kuwa Presida baada ya kuing'oa CCM. Changamkia tenda. Kama analipa piga kazi kamanda
 
Pole sana uamuzi ni wako ila kumbuka mtoto Sio Nyumba utaiacha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Anadhani ukimzalisha atapata watoto wazuri kama hao anaowaona ktk picha? mawazo finyu sana hayo!
 
ukisikia jini madhara ndio huyo............akili za mbayuwayu changanya na za kwako,ukiuvaa huo mkenge utajuta maishani.
 
Nimeshindwa kumjibu lolote, kwani kuna agenda gani nyuma ya pazia?
Nimemhoji kwani huna mume? akasema ana mchumba lakini kwa kuwa hajamuoa bado, yeye ana maamuzi yake mwenyewe na maisha yake na haingiliwi na mtu.
Huna sababu ya kushindwa kumjibu lolote ikiwa hauna nia mbaya dhidi ya mkeo. Ni nini kinakufanya ushindwe kumkatalia?

Kilichonishangaza hatujajadili mambo ya mapenzi, hatujajadili mambo ya kusema "i love you" sasa from "i miss you" to "nataka unipe mtoto" imenishangaza kidogo.
Kama na wewe haujaanza kutaka kumsaliti mkeo, imekuaje uanze kujiuliza haya maswali hapo juu?

Kwanini utake mjadiliane kuhusu mapenzi?

Nimeshindwa kumwelewa, anataka kunitega kwa mimba ili baadaye avuruge ndoa yangu? au amevutiwa sana na watoto wangu kiasi cha yeye kutamani kuwa na watoto kama wangu, na hatima yake ni nini?

Acha kuumiza kichwa chako pasi na sababu. Kaa na mkeo mjenge familia yenu.

Kwani mwanaume ni wewe tu dunia nzima?
 
Mkuu usiingie kwenye huo mtego, hao ni makahaba tu, Ndoa ni agano takatifu, hivyo na liheshimiwe na watu wote including huyo kahaba anayekurubuni uingie naye kwenye ndoa isiyo rasmi.
 
Pumbavu tena pumbavu sana.....kaa na mkewe mpende zaa naye watoto hata kumi na nane kaa ni hitaji lako....ukazae nje mtoto akose maleizi na mapenzi ya baba wakati upo duniani...umpe mkewe pressure wakati yeye bado anatka kuishi kwa amani uache nyuma yako uanze nyumba ndogo....upunguze mkate wa familia yako kwaajili ya ushetani....mnyziuuuu!
 
usiingie kwenye huo mtego.tena usimdekeze mwambie short and clear kuwa haupo interest,salamu zake zozote usizijibu,mwisho atachoka mwenyewe.kama shida yake ni sperm,ipo hospitali dar unalipa unapewa sperm na wanaziingiza wenyewe.mchumba si anae,mwache na majanga yake.wadada wengine bwana,hawajijui wanataka nini katika maisha yao.
 
^^
Kama una uzoefu wa kugawa mbegu zako hilo ni dogo kwako.
Lakini kama unajua thamani ya mtoto vunja ngome za shetani.
^^
 
Nimefahamiana na dada mmoja,
Kila siku akawa ananitumia ujumbe mfupi kwenye simu yangu, i miss u, nikadhani kawaida. Baadaye akanitafuta facebook, Jambo moja alilogundua bila hata kuniuliza, nina watoto wawili ambao picha zao nimeweka facebook. Jana jioni akanitumia msg, kumbe una watoto wawili? nikajibu ndiyo.

Baadaye akanitumia message kuwa ana ombi moja kwangu. Nikadadisi ni ombi gani hilo? Akasema nataka mtoto unizalie, kama niko tayari tukapime then nimpe ujauzito basi, nikamwambia nina familia, akasema hataki ndoa, wala hataki mimi nimlee mtoto, anachotaka ni mimba tuuu. Kilichonishangaza hatujajadili mambo ya mapenzi, hatujajadili mambo ya kusema "i love you" sasa from "i miss you" to "nataka unipe mtoto" imenishangaza kidogo.

Nimeshindwa kumjibu lolote, kwani kuna agenda gani nyuma ya pazia?
Nimemhoji kwani huna mume? akasema ana mchumba lakini kwa kuwa hajamuoa bado, yeye ana maamuzi yake mwenyewe na maisha yake na haingiliwi na mtu.

Leo asubuhi nimefungua facebook, nimekuta ameweka comment kwenye picha za watoto wangu "hongera sana kwa watoto wazuri sana.."

Nimeshindwa kumwelewa, anataka kunitega kwa mimba ili baadaye avuruge ndoa yangu? au amevutiwa sana na watoto wangu kiasi cha yeye kutamani kuwa na watoto kama wangu, na hatima yake ni nini?

Anataka kuvuruga ndoa yako. kukuaribia maisha yako. kukuaribia maisha ya watoto wako. Huyo ni shetani, anakujua ila wewe haumjui na ana jambo lake. Yaani ujiaribie kwa ajiri ya lishetani la facebook?
 
Nachukiaga hakiri za kitoto, sasa wewe dume zima, unataka ushauriwe kwenye jambo dogo kama hilo??
Huyo rafiki yako anaetaka umzalie tayari ameshakupenda na anatumia gia ya kuzaa ili akuteke

kama unaipenda familia yako, katisha huo urafiki na huyo dada haraka sana coz anapoelekea ni kubaya ndugu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom