Kuna nini kwenye madeni haya ya nchi za Kiafrika? Badala ya kupungua ndio Kwaanza yanaongezeka

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,504
3,499
Kuna nini kwenye mikopo hii ambayo nchi zetu hizi za Afrika huwa zinakopa/ kopeshwa?

Zinajitahidi karibu Kila mwezi kurejesha mikopo hiyo, miaka na miaka, lakini badala ya kupungua, ndio Kwanza yanaongezeka!!

Lakini Je, shida iko wapi? Uwekezaji unaotokana na mikopo hiyo ndiyo hupelekea tusiondoke kwenye madeni hayo ama ni usimamizi mbovu wa mikopo na matumizi hiyo, au kuna shetani gani kwenye mikopo kutoka Kwa nchi za kibepari??

Fedha zao ni za kimapepo? Kwamba haziwezi kuzinufaisha nchi zetu na Miradi inayotokana na mikopo hiyo haiwezi kutuletea faida?

Kuna nchi ambazo mpaka muda huu zipo kwenye hatari ya mfilisi, kutokana na mikopo kufikia kwenye kiwango cha nchi husika kushindwa kuirejesha Kwa mjibu wa masharti ya mikopo hiyo

Je, kuna nchi yoyote labda balani Afrika, Kwa kupitia mikopo kutoka ughaibuni imewahi kujikomboa na hatimaye kujiletea maendeleo makubwa?

Kama haipo, Je kuna nini kwenye hii mikopo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom