Kuna nini kwenye bei za bidhaa kama mafuta? Vipi mlipo wana JF bei zikoje.?

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,927
6,465
Wanajukwaa nawasalimu.

Mimi niko mkoani Arusha na kuna mkwamo mkubwa sana wa upatikanaji wa Mafuta ya kula/Kupikia.

Na ukiyapata dukani bei ni mkasi. Ile Singida ya Elfu 16 kwasasa inapatikana kwa taabu na bei yake imepanda mpaka elfu 25. Vipi huko kwenu mlipo hali ikoje? Hii ndiyo Tanzania mpya?

Mbona serikali iko kimya sana kwenye hili? Naomba tushirikishane angalau serikali iingilie kati maana hali ni mbaya huku vyombo rasmi vya habari vikiwa kimya huku wananchi wakiteseka.

Naomba kuwasilisha
 
Lita5 ya futa la alizeti 18500 hapo bei ya Kitetoni sijui Dar itakua sh ngapi
Hali mbaya
 
Lita5 ya futa la alizeti 18500 hapo bei ya kitetoni sijui dar itakua sh ngapi
Hali mbaya
Huku Arusha hata kuyapata mpaka utoe oda. Tunaona giza zaidi kuliko matumaini ya mwanga
 
Kipindi hichi obvious mafuta lazima yaadimike

Ni msimu wa kupanda alizeti siyo kuvuna.
 
Mbaazi Ukikosa Maua Husingizia Jua
Wakati Huu Watasema Mabeberu Hao
Mpaka Sasa Hivi Hatujapata Ufumbuzi Wa Bei Kuwa Juu Hasa Saruji, Utajua Mengine Ni Ujanjaujanja Tu
Ukiona bei iko juu, ujue supply ni ndogo kuliko demand. Hata waweke watu ndani haisaidii. Watafute ufumbuzi tu wa kuongeza cement kwenye soko
 
Ukiona bei iko juu, ujue supply ni ndogo kuliko demand. Hata waweke watu ndani haisaidii. Watafute ufumbuzi tu wa kuongeza cement kwenye soko
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu!!!
 
Back
Top Bottom