Kuna nini katika salamu za pongezi kwa askofu mpya wa mwanza, mbona hazikusomwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna nini katika salamu za pongezi kwa askofu mpya wa mwanza, mbona hazikusomwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theophilius, Jan 9, 2011.

 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  katika hafla ya kumsimika askofu mpya wa jimbo la mwanza, waziri wasiri ameshindwa kusoma salamu za Rais na badala yake akakabidhi bahasha yenye hizo salamu kwa mhusika.

  kwa hakika hii ni stali mpya ya serikali ya awamu ya nne ya KASI ZAIDI... kwani ni nadra sana kwa mwakilishi wa Rais katika hafla au sherehe fulani kuamshwa na badala ya kusoma hotuba/salamu kwa niaba ya anayemwakilisha, kuona anaishia kukabidhi bahasha.

  ni jambo la kushangaza hususani kipindi hiki ambacho kuna madai kwamba KUNA UDINI. wengi walikuwa na shahuku ya kumsikia rais atasema nini, hata kama hakuweza kufika kama ilivyotarajiwa, mwakilishi alitarajiwa kusoma walaka/hotuba/salamu hizo kwa niaba ya rais

  Hii ni ishara gani, kwa Rais ambaye tangu alipoingia madarakani amekuwa ni nadra kutohudhuria sherehe, hafla au adhimisho muhimu bila kuajali aliyeaandaa labda kama ajaalikwa, kama ilivyotokea kwa sherehe za wafanyakazi!

  pengine kuna mwenye wazo juu ya hili!
   
 2. K

  Kieleweke Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na sijui kwa nini ametuma ujumbe wakati yeye mwenyewe yuko hapa Mwanza jana jioni tumeona msafara wake.

  Baadhi tulidhani amekuja kwenye usmikaji huu.
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Tumueleweje? mara ya mwisho alialikwa bukoba kusimika askofu wa lutheran akachelewa kufika..kiasi cha kushindwa kutembelea miradi aliyotakiwa kukagua.... kwenye shughuli ........na akaondoka mara tu ya kuongea na kuacha chakula alichoandaliwa na wenyeji wake...

  mara ya mwisho wakati wa msiba wa askofu mkuu mayala alichelewa ..lakini alifika..sasa kama jana ameshindwa kufika kufika na ukizingatia umuhimu wa shuhuli za kijamii zinazoendeshwa na kanisa ukanda wa ziwa kama chuo kikuu cha st augustine,chuo kikuu bugando...hospitali ya rufaa budando.....miradi ya maji na mingine ya kijamii ......basi inaonekana amenuna!!!!!!....lakini kweli itasimama kuwa kweli...hawa ndio waliomuunga mkono mwaka 2005...sasa kama akiambiwa ukweli anafikiri anachukiwa na asikuwe anasaidiwa ...basi!!
   
Loading...