Kuna nini kati ya KAYUNI na Kaseja???

MTWA

JF-Expert Member
Aug 5, 2009
1,166
166
Hivi juzi vioo ngozi wa TFFkupitia kwa S. Kayuni walitangaza kuwa Kaseja na mzungu wa Yanga wanafungiwa mechi tatu kwa kutosalimiana na mgeni rasmi- Mkuu wa mKOA wa Mwanza A. kandoro.

Lakini baada ya kufuatilia wamekuta kumbe Kaseja alisalimiana na mkuu wa mkoa huyo. Baada ya hayo wakasema kuwa hakusalimiana na wachezaji wa yanga. halafu adhabu ileile.

sasa haieleweki mbona wao hawajiadhibu kwa kudanganya?
halafu umakini wao upoje, kama unaweza kumwadhibu mtu kabla ya kujua kosa halisi la mtu? au ni visa tu?
Mimi binafsi hainiingii akilini kuwa wanapata wapi taarifa hizi hadi wazichanganye hivi?
Na inalkuwaje makosa yanahama lakini adhabu inabaki?
Au walishapanga tu kumpa adhabu hii! Mimi nahisis hata Maximo hakuwa yeye ila ni hawa jamaa? au mnasemaje! mimi naingia hasira na hili soka la bongo mbona la fitina?
Au tuendelee kushabikia Arsenal, Real Madrid, na hizo Juve tu.
 
Kayuni katika utawala wa michezo is a "dummy"!

Hakuna sheria ya kimichezo inayosema kuwa kutopeana mkono na opponent wako ni "KOSA". Handshaking is a sign of "sportmanship and respect" among players in the context of football/soccer.
 
Lakini mimi naona Kayuni hafai hata umonita, kwa sababu hata wajinga hawezi kuwaongoza, hawezi kubabaika namna hii halafu eti anakuwa na msimamo wa kuadhibu mtu
 
Ndio maana anavaa suspenders na mkanda wa suruali at the same time
basi inaonesha kuwa hana aibu halafu kuna kila dalili ya kuwa yeye ni KIHIYO, yaani nina wasiwasi sana na uongozi wake.
Na viongozi wenzake wapo wapi, Na simba si wakate rufaa?
 
Ndio maana anavaa suspenders na mkanda wa suruali at the same time

maximo-8.jpg


Akiwa na mbaya orijino wa Kaseja....labda anaendeleza chuki
 
maximo-8.jpg


Akiwa na mbaya orijino wa Kaseja....labda anaendeleza chuki
Sasa inakuwaje mtu anafanya yasiyo ya kisoka kabisa, nauliza tena hana aibu maana leo hata wasiojua soka wamehoji adhabu ya aina hii
Anatuharibia
 
Alafu wamempendekeza afanyiwe usaili wa kuwa katibu mkuu wa TFF subirini viroja zaidi ya hivi kamati ile ya nithamu ilikua chini ya El - maamry ipo wapi, maana hizi kazi nyingine ni proffession za watu
 
Nilipomwambia kuwa hatuvaagi mkanda na suspenders akavua mkanda....ni boreer kishenzi huyu jamaa

001.jp_1.jpg
Kama alifanya hili asilokuwa na uhakika nalo, nina wasiwasi nahili nalo hajui ila anafanya fanya tu ilimradi aonekane yupo,
Inabidi atimuliwe
 
Ile picha hakuna uthibitisho kwamba ni ya kweli huenda ikawa imetengenezwa,KASEJA alikuwa wapi siku zote kupeleleka hiyo picha kama kielelezo?
 
Kayuni kateleza aliposema kaseja hakumsalimia kandoro, ila hili la kukwepa kusalimia wachezaji wa yanga ni lakweli, na hili litasaidia kuondoa haya maimani potofu ya kishirikina, kwa mujibu wa vyombo vingi vya habari , inasemekana huyu jamaa ndio mtindo wake kila wanapokutana na watani wao wa jadi, huu ni ujinga adhabu yake inafaa sana ila kayuni nae bonzo
 
Kwani huyu mtu atangoka lini hapo TFF?maana anatupotezea muddy kabisa:bowl:!

Atang'oka siku Tenga atakapokoma kuwa rais wa TFF.

Sina kumbukumbu,hivi Bridges alipewa adhabu yoyote baada ya kukataa kumpa mkono JT?
 
Sasa inakuwaje mtu anafanya yasiyo ya kisoka kabisa, nauliza tena hana aibu maana leo hata wasiojua soka wamehoji adhabu ya aina hii
Anatuharibia
Na FIFA nayo eti inataka aina hii ya "Vimeo"ndiyo iongoze soka,mkitimua Vimeo kama hivi mnafungiwa!!!
 
Ile picha hakuna uthibitisho kwamba ni ya kweli huenda ikawa imetengenezwa,KASEJA alikuwa wapi siku zote kupeleleka hiyo picha kama kielelezo?

Siku zote lini? Simamia ukweli bwana,wewe ni mtu wa soka(au ni ile ya England pekee!!). Kandoro kasema alisalimiana na Kaseja je naye kauli yake imetengenezwa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom