Kuna nini kati ya CHADEMA, Marekani, Ujerumani, Ubelgiji, Amnesty International na Kenya dhidi ya Usalama wa Tanzania?

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,036
3,479
Wakuu,

Hili ni bandiko la swali ili kupata uelewa mpana kuhusiana na taswira mpya wanasiasa wa Tanzania na washirika wao wanavyoonesha katika siku za hivi karibuni.

Je, kuna uhusiano gani wa ziada nje ya utaratibu wa kawaida kwa nchi tajwa hapo juu na shirika mojawapo la haki za binadamu na chama kinzani chenye viongozi machachari zenye harakati hasi?

Je, sio muda muafaka kurejea mfumo wa usalama wa nchi na kurekebisha baadhi ya mambo ili kudhibiti mbinu chafu za kijasusi zinazoendelea hivi sasa kwa kutumia watu kutoka miongoni mwa waTanzania wenyewe ama kwa kujitambua au bila kuelewa kutokana na uerevu unaotumika kupandikiza hadaa kwa ulaghai uliobobea (mercenary hoodwink approach)?

Wajuvi wa masuala ya kijasusi tufumbueni macho tubaini mwelekeo ulio sahihi kwa mustakabali wa Taifa.
 
Mkianza kupiga watu risasi kisa uchu wa madaraka ni lazima watafute watetezi kutoka nje, mawazo aliuawa, hakuna aliekamatwa, Benni Saanane bila shaka ni mfu, Lissu kapigwa risasi za kutosha, hakuna aliekamatwa. Kama yote yanatokea hayo, kwanini wasitafute watu wa kuwahifadhi nje?
 
Historia ni mwalimu hizo Nchi zote zilizomsindikiza Lissu hazijawahi na hazitowahi kuwa Rafiki wa Afrika
Zinanufaika hadi Kesho kutwa na Afrika kwa kuwaondoa viongozi wa kiafrika wenye Uzalendo na waafrika
Kwa kuwatumia waafrika Kama Lissu kufanikisha matakwa yao.
 
Historia NI mwalimu hizo Nchi zote zilizomsindikiza Lissu hazijawahi na hazitowahi kuwa Rafiki WA Afrika
Zinanufaika Hadi Kesho kutwa na Africa kwa kuwaondoa viongozi WA kiafrika wenye Uzalendo na waafrika
Kwa kuwatumia waafrika Kama Lissu kufanikisha matakwa yao
Historia ni mwalimu mzuri, viongozi wa Afrika tangu Mkwawa, Mirambo nk hadi Mugabe, M7 na jiwe hawajawahi kujali wananchi wala maslahi ya wananchi wao. Huwa wanaangalia matumbo yao
 
Historia NI mwalimu hizo Nchi zote zilizomsindikiza Lissu hazijawahi na hazitowahi kuwa Rafiki WA Afrika
Zinanufaika Hadi Kesho kutwa na Africa kwa kuwaondoa viongozi WA kiafrika wenye Uzalendo na waafrika
Kwa kuwatumia waafrika Kama Lissu kufanikisha matakwa yao
Duh, Mkuu hivi ndivyo maana ya mtiririko wa matukio haya?

Basi nakuelewa mkuu kwa mchango wako.....kumbe!!
 
Baada ya maandamano kushindwa, ni rasmi sasa, hao uliowataja, ndio watasaidia kuyabusti maandamano yakianzia kwao huko hadi Ufipa na mwisho wa siku yanapokelewa na Mbowe na kuishia hapo bila faida yoyote.
 
You must be crazy, ebu ongelea political environment Tanzania. Mauaji yanayotokea hapa, politically motivated ones unayasemeaje! Adui wangu siyo ngozi, adui wangu ni yule anayenidhulumu haki yangu. Nikipata jirani akanisaidia kupata haki yangu nitamtumia
 
Back
Top Bottom