Kuna nini kati ya CHADEMA, Marekani, Ujerumani, Ubelgiji, Amnesty International na Kenya dhidi ya Usalama wa Tanzania?

Wakuu,

Hili ni bandiko la swali ili kupata uelewa mpana kuhusiana na taswira mpya wanasiasa wa Tanzania na washirika wao wanavyoonesha katika siku za hivi karibuni.

Je, kuna uhusiano gani wa ziada nje ya utaratibu wa kawaida kwa nchi tajwa hapo juu na shirika mojawapo la haki za binadamu na chama kinzani chenye viongozi machachari zenye harakati hasi?

Je, sio muda muafaka kurejea mfumo wa usalama wa nchi na kurekebisha baadhi ya mambo ili kudhibiti mbinu chafu za kijasusi zinazoendelea hivi sasa kwa kutumia watu kutoka miongoni mwa waTanzania wenyewe ama kwa kujitambua au bila kuelewa kutokana na uerevu unaotumika kupandikiza hadaa kwa ulaghai uliobobea (mercenary hoodwink approach)?

Wajuvi wa masuala ya kijasusi tufumbueni macho tubaini mwelekeo ulio sahihi kwa mustakabali wa Taifa.
Mwelekeo sahihi ni ciciem kuondoka madarakani bila hivyo wapenda demokrasia na haki za binadamu watazidisha kutugonga rungu hasa hasa kwa hii regime ya awamu ya tano.
Awamu hii ni wakiukaji wakubwa was misingi ya utawala was sheria na kuheshimu haki za binadamu. Hii awamu haina tofauti yeyote na uliokuwa utawala was busgiri was Sudan.
 
Nchi ulizotaja na shirika la Amnesty wapo busy kutugawa kwenye makundi kulingana nafasi zetu kiuchumi ili waweze kututawala. Kwamba kunapokuwa na kundi kubwa la watu maskini, ni rahisi kutumia kundi hili kuondoa uongozi uliopo na kupandikiza "puppets" ambao watatekeleza matakwa ya wale waliowaweka.
 
Back
Top Bottom