Kuna nini birthday ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli?

CHEF

JF-Expert Member
Nov 4, 2013
222
122
Ama hakika nimeona upendo wa ajabu kwa Watanzania walioonesha kwa Mhe. Rais maana wanasiasa hasa wapinzani wa Mheshimiwa Rais wananadi kwamba wananchi hawampendi mheshimiwa kutokana na kuongezeka kwa ugumu wa maisha, ila kwa hakika usemi huu nimegundua ni uzushi mkubwa.

Kwa ufupi naweza kusema ni unafiki na uzandiki wa wapinzani wa mheshimiwa; maana hizi shamra shamra nilizoziona za birthday ya Mheshimiwa Rais sijawahi kuziona ijapokuwa Mheshimiwa Rais sio hata mpenzi wa masuala ya birthday.

Yaani hata huku kijijini kwetu wakubwa kwa watoto wamejua kulikuwa na birthday ya Mheshimiwa, status za whatsapp kila nikichungulia wanaonizunguka naona HBD Mr president, na mimi niseme tu uishi miaka mingi Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli wananchi tunaupendo wa dhati sana dhidi yako .
 
Nafikiri ni kwa sababu ya mapenzi ya dhati
Ulipata kutembea kidogo miaka ya nyuma ukaenda Zimbabwe?
Uliwahi kufika huko msimu wa birthday ya Mugabe?
Basi kule sherehe yake ilikuwa kama ya kitaifa, na hata siku zote za maisha ya kawaida asilimia 90% Mugabe alikuwa "mungu" wao kama inavyotaka kuwa Tanzania.
Lakini baada ya shida kushindwa kuzoeleka jeshi likaamua kumuweka pembeni. Ajabu ni kuwa 90% ya RAIA ndio walioingia tena mitaani kushangilia. Hiyo ndio formula ya tawala za kibabe na kidikteta hasa kwa Afrika.
Tafakari.
 
Haitaweza kuwa hivyo Tanzania na UBASHIRI HUO USHINDWE KWA JINA LA YESU!
 
Ulipata kutembea kidogo miaka ya nyuma ukaenda Zimbabwe?
Uliwahi kufika huko msimu wa birthday ya Mugabe?
Basi kule sherehe yake ilikuwa kama ya kitaifa, na hata siku zote za maisha ya kawaida asilimia 90% Mugabe alikuwa "mungu" wao kama inavyotaka kuwa Tanzania.
Lakini baada ya shida kushindwa kuzoeleka jeshi likaamua kumuweka pembeni. Ajabu ni kuwa 90% ya RAIA ndio walioingia tena mitaani kushangilia. Hiyo ndio formula ya tawala za kibabe na kidikteta hasa kwa Afrika.
Tafakari.
Mkuu upendo haulazimishwi, mtu akipenda kinafiki utajua tuu! na hakuna upendo wa kweli kama wa mtoto, mtoto akipenda amependa na sio unafiki, Upendo niliouona kipindi hiki kwa mheshimiwa ni mpaka kwa watoto wadogo kabisa, sasa mkuu huu ni upendo wa kweli kabisa
 
Katimiza miaka 60 hivyo kwa tafsiri sahihi Magufuli saivi ni Babu kizee au kikongwe au Muhenga. Hivyo acha wajukuu zake tumtakie kheri ya siku yake ya kuzaliwa japo anatusomesha namba kweli kweli.
 
Hahahaa umesomeshwa namba ngapi mkuu
 
Ulipata kutembea kidogo miaka ya nyuma ukaenda Zimbabwe?
Uliwahi kufika huko msimu wa birthday ya Mugabe?
Basi kule sherehe yake ilikuwa kama ya kitaifa, na hata siku zote za maisha ya kawaida asilimia 90% Mugabe alikuwa "mungu" wao kama inavyotaka kuwa Tanzania.
Lakini baada ya shida kushindwa kuzoeleka jeshi likaamua kumuweka pembeni. Ajabu ni kuwa 90% ya RAIA ndio walioingia tena mitaani kushangilia. Hiyo ndio formula ya tawala za kibabe na kidikteta hasa kwa Afrika.
Tafakari.
Tutafakari nini sasa hapo, embu funguka vizuri kama mtt wa kiume
 
Lakini mtoto akionesha upendo, basi huo ni upendo wa kweli, mtoto hawezi kuficha baya na zuri, watoto wengi wameonesha upendo kwa mheshimiwa basi huo ni upendo wa kweli
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom