Kuna NGO moja na BBC waliokuwa wakifuatilia sakata la Ben Saanane, Tundu Lissu na Azory Gwanda. Waliamriwa kuacha shughuli hiyo mara moja!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,874
Kumbe Rais Magufuli aliwachokoza sana EU? Kuna NGO moja kutoka EU ambayo iliamua kufuatilia sakata la kupotea Ben Saanane na Azory Gwanda pamoja na kushambuliwa Tundu Lissu kwa risasi lakini cha ajabu watu wa hiyo NGO waliamriwa kuondoka nchini haraka iwezekanavyo.

Pia zipo taarifa kuwa kituo cha BBC nacho kiliamua kufuatilia sakata hilo lakini kilipigwa marufuku na kupewa karipio kali. Nini tatizo?

Aidha habari zinasema kuwa NGO moja kutoka EU iliyokuwa ikifadhili program ya "Haki elimu" nayo ilifukuzwa nchini na shughuli zake zote kusitishwa.Nini tatizo?

Hayo yote tisa kumi NGO zilizokuwa zikishughulikia utafiti wa magonjwa yajulikanayo kama "tropical diseases" nazo ziliamriwa kusitisha shughuli zake nchini. Nini tatizo?

Kwa hakika serikali ya Rais Magufuli ina mengi ya kujibu!
 
Ni wajinga tu watakaodhani haya mataifa yamekurupuka.

Usisahau hata BalozI wa EU nae alikuwa harassed na huu utawala.

Narudia maneno yangu kuwa, "kwa sasa ni uzalendo kushurikiana na wanaoitwa mabeberu kuliko hawa watu wa awamu hii"

Na huyu mtu ajue tu,siku mambo yakiharibika/maji yakizidi unga,wafuasi wake wote wanaomzunguka na kumpa support leo hii,watamkana/watamkimbia kama walivyofanya wafuasi wa Yesu (wanafunzi wake) siku ile anakamatwa na Wayahudi kabla ya kuteswa.
 
Majizi chadema wakipewa hii nchi wanaiuza kwa wazungu .

Kila wakati wanajipendekeza kwa wazungu kama mazuzu na washamba fulani wasiojua historia ya wazungu kwenye nchi hii.
Kama walivyofanya kwenye mikataba ya madini na gas. CCM isingeingia madarakani 2015 nadhani chadema wangeimaliza nchi yetu pendwa ya tanzania kwani wametuibia toka wameanza kuongoza mwaka 1977 hadi ccm iliposhinda urais mwaka 2015
 
Kumbe Rais Magufuli aliwachokoza sana EU? Kuna NGO moja kutoka EU ambayo iliamua kufuatilia sakata la kupotea Ben Saanane na Azory Gwanda pamoja na kushambuliwa Tundu Lissu kwa risasi lakini cha ajabu watu wa hiyo NGO waliamriwa kuondoka nchini haraka iwezekanavyo.

Pia zipo taarifa kuwa kituo cha BBC nacho kiliamua kufuatilia sakata hilo lakini kilipigwa marufuku na kupewa karipio kali. Nini tatizo?

Aidha habari zinasema kuwa NGO moja kutoka EU iliyokuwa ikifadhili program ya "Haki elimu" nayo ilifukuzwa nchini na shughuli zake zote kusitishwa.Nini tatizo?

Hayo yote tisa kumi NGO zilizokuwa zikishughulikia utafiti wa magonjwa yajulikanayo kama "tropical diseases" nazo ziliamriwa kusitisha shughuli zake nchini. Nini tatizo?

Kwa hakika serikali ya Rais Magufuli ina mengi ya kujibu!
Hii propaganda nyepesi sana kajipapange upya .Serikali haichaki kirahisi hivyo
 
62 Reactions
Reply
Back
Top Bottom