Kuna ndoa na harusi, wengi mnapenda harusi sijui kwanini

belionea

JF-Expert Member
Mar 17, 2014
1,052
914
Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi!

Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza Ndoa picha inayowajia ni Suti kali, Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, Mashosti kuingia ukumbini naWimbo wa Alingo,Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall..

Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia??Umewahi kuwaza Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno yaMama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?? Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi. Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika.

Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo... Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako??? Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?? Sidhani... Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,Unatamani Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi????-
 
ujumbe mnono sana nimekupenda bure,,,, barikiwa sana,,,,,atakae ponda huyo anaugua akili si mzima!!!
 
ujumbe mnono sana nimekupenda bure,,,, barikiwa sana,,,,,atakae ponda huyo anaugua akili si mzima!!!
 
ujumbe mnono sana nimekupenda bure,,,, barikiwa sana,,,,,atakae ponda huyo anaugua akili si mzima!!!
 
ujumbe mnono sana nimekupenda bure,,,, barikiwa sana,,,,,atakae ponda huyo anaugua akili si mzima!!!
 
Umeongea point ,one of my friends ana imaginations hadi namshangaa,anawaza kwenda honeymoon visiwani sijui wapi .Na hivi akiona harusi za wa-naija na arabs ndo anazidi kupagawa
 
Kuna mwanaume wa ndoa na mwanaume wa showoff wadada wengi kwa sasa hawataki mwanaume wa ndoa wanatafuta mwanaume wa showoff...
 
Hakuna umegusa mule mule aisee watu wanawaza sherehe tu hawazi majukumu baada ya hapo ndo maana michepuko inazidi kuongezeka mtu anafunga ndoa kesho Leo analala na mchepuko habari sana
 
It seems essential, in relationships and marriage, that we concentrate only on what is most significant and important unfortunately wedding is not one of them...
 
Back
Top Bottom