kuna na CVs kubwa haimaanishi utakuwa good kwenye uongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kuna na CVs kubwa haimaanishi utakuwa good kwenye uongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FredKavishe, Mar 19, 2012.

 1. F

  FredKavishe Verified User

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuna tabia ya wana jf kwenye jukwaa la siasa mtu katika serikal o upizani akiropoka kitu wanakimbilia kucheki CV yangu na kuanza kumjudge kutoka na CV huo sio ugreat thinker.
  Tukubaliane kuna viongozi wengi kwenye serikali wana CV za kutisha je wao ndo wametufikisha wapi
  1.Andrew Chege
  Ni mwanasheria aliyebobea je alisaini mikataba mingapi mibovu kipindi akiwa mwanasheria mkuu
  2.Edward lowassa
  Ni msomi mzuri je alituma vimemo vingapi tanesco waikubali richmond
  3.Ben mkapa
  Ni msomi je si ndo huyu alifanya biashara ikulu
  Kwa hyo mifano michache tu ukiangalia CVs za viongozi wengi utazamia hutaamini madudu wanayofanya
  Je wale mawaziri ambao hawatakiwi wizara ya afya mama Nkya na mponda CV zao zinatisha je wanaweza kuongoza la hasha hawawezi??

  Katika dunia ya Uongozi CV inakua kama nyongoza na sio kumjudge mtu kupata kazi sehemu fulani.
  Uongozi mzuri hauhitaji master wala phd kuweza kulead watu mtu anaweza akawa na Diploma tu but akawa kiongozi mzuri sana kuliko mwenye Phd

  Tatzo la viongozi wetu wanaingia kwenye uongozi kuarchive vitu.hata siku moja mtu anayetaka kitu kwenye uongozi wa umma hawezi kufanya kitu kizuri.

  Nakumbuka CDM kwenye uchaguzi mkuu walisimamisha mgombea mweza mwenye elimu ya darasa la saba watu wakawa wanahoji eti kwanini wanasimamisha mtu mwenye elimu ndogo.uongozi haungalii elimu
  Kuongoza ni kuweza kuwatoa watu kutoka hapa kuwapeleka sehemu nyingine salama
  Tatizo la watz wengi hatujui kuwa kwenye uongozi mfano waziri hana maamuzi mengi makubwa kama katibu wake mkuu.

  CV ya mtu haiwezi hata siku moja ikamfanya akawa kiongozi bora utendaji wake wa kazi ndo utamfanya na ufuatiliaje wake.
  Tuna mapro madr waliobobea nchi hii je tujiulize wametusaidia nini pamoja kuwa na vyeti vyao vya kuvutia kama dhahabu.
  Wengi wanahishia kukaa mahofisini kupiga porojo za wanasiasa na kuacha utaalamu wao kukimbilia siasa.

  Sasa wana jf mtu akiboronga kitu ni vyema tuangalie je aliingia kwenye siasa kupata nn na sio kujudge kupitia CVs zao ambao ni mapambo tu
  Kwangu mimi ujuzi wako ndo utanifanya niamini wewe ni mtendaji na sio CV kubwa wakati hujui kitu na hii ishu imeamia kwenye ajira CV ndo inamata mtu ana GPA ya 4.8 anapewa kazi anafanya madudu tu ofisi sababu yale mambo alikreamu tu akiwa shule
  CV isijadali uwezo wa mtu.kuna watu wana certificate but wana uwezo wa kuongoza kuliko wenye PHD

  Hivi tuchukulie mfano CV ya makamo wa raisi Bilali mtaalumu wa nyuklia hivi huyu angebaki kwenye field yake ya nyuklia taifa si lingepata mambo meng toka kwake sana kajiingiza kwenye siasa anashindwa kutumia kitu alichosomeshwa kwa kodi zetu

  Uongozi ni karibia ambayo mtu anakua nayo toka utotoni.uongozi sio CV kubwa hapana uongozi ni kuweza kuwaongoza wale ulipewa unaweza ukawa hujasoma lakini ukawa kiongozi mzuri kuliko hata jk.

  Na suala la kuangalia mawaziri kwenye katiba ijayo wasiwe wabunge hii itapunguza malamiko kwa mawaziri
  Napendekeza mawaziri watokee kwenye wizara usika upitishwe mchakato wa kugombea nafasi hyo kwa watu walioko wizarani ndo wachaguliwe sio mtu kawa mbunge tu hana uzoefu wowote na wizara ya kazi anapewa cheo

  CV ni mapambo tu ujuzi wako wa kazi ndo utaipamba cv yako.
  Unatakiwa ujue kukifanya kile ulichokisomea na sio kuwa dr wakati hujui hata kuboost uchumi wetu

  Mm kijana
  Majanikv
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Umeeleweka, bahati mbaya kwenye dunia ya leo tunayoiishi makaratasi ndo kipimo, huwezi kukwepa!
   
 3. F

  FredKavishe Verified User

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kosa kubwa sana na litaendelea kutugharimu mpaka basiii
   
 4. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Unajua taaruma nyingine huwa watu wanazikuuza saana lakini sorry to say ni za kinadharia zaidi, nawajua watu wengi katika nchi hii waliosoma nu phy siyo kuwa ni vichwa saana kama watu wanavyo fikiri jamani!
   
Loading...