Kuna mwanasiasa alipiga sana kelele kuhusu tume huru ya uchaguzi

SHIGOTTO

Senior Member
Sep 4, 2018
156
280
Za leo ndugu wapenzi, leo napenda kuwakumbusha kuwa madai ya tume huru ya uchaguzi yalianza toka enzi za Marehemu Rev. Christopher Mtikila lakini tukamuona ni mtu anaye piga kelele za kisiasa.

Leo nimesoma kwenye gazeti Mzee Lowasa na jioni hii Chairman Mbowe wote wanasema bila tume huru ya uchaguzi hakuna jipya. Wito wangu isiwe tukaishia hapo ni wakati sasa wa kuidai hiyo tume huru, lakini tukishaipata tuiangalie muundo wake kwa kuwa isije tokea kama yanayotokea sasa hivi kwa (wabunge na madiwani) kununuliwa. Napenda kuwakilisha.
 
Tatizo sio tume huru tu, hata Katiba tulionayo ni mbovu sana dunia nzima. Ina mpa madaraka makubwa mtu Mmoja badala ya wananchi wenyewe. Katiba mpya ndio utakuwa mwarobaini wa yote hayo
 
Mimi nilimuelewa tangu 1995,lakini wanasiasa weti sijui wna tattizo gani,hawaelewi hili jambo
 
Tume iko huru huyo mbowe na wabunge wa vyama vingine wametangazwa na time IPI kama sio hiihii ,acheni ulimbukeni magufuli chapa kazi mungu akupe maisha marefu sana
 
Katiba Mpya nayo ni muhimu sana,Tusipoamka wananchi Na kudai hivyo vitu tukategemea mbowe au lowassa tunajidanganya.Sijui ndio moshi wa mwenge ndio umetufanya tumelala hivi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom