Kuna Mvua kubwa sana Arusha. Mikoa mingine hali ipoje?

Kuna mvua Kubwa sana inanyesha hapa usiku huu Nipo ndani lakini nahisi ni ya mawe,

Hata usingizi hauji kutokana na hofu.

Mvua ni kubwa kwa kweli kama itakuwa na madhara kesho tutapata taarifa rasmi.
Chato tangu tar 17.3.2021 hatujaona mvua.
 
Yaani Kidimbwi palijaa bwanaaa. Aaanh. Mpaka asubuhi bahari shwari. Hat kaupepo hakakuwepo.
Na sasaiv nimetoka kwenye ibada shwari kabisa na dar es salaama yangu. I love you dsm
Ila acha JoBo aondoke tu watu wa Dar mmeshindikana walai,
Watu wamefanya bonge la party na wengine kwenda huko huko baharini, eti wanamsubiri JoBo, wavuvi walienda kutega nyavu zao kama kawaida,
Naipenda Tanzania.
 
Mitaa ya bunju kuna manyunyu tu, hata ukitoka hayana kuloweshana..
 
Sijawasiliana na watu wa huko

Hapa moshi tuliingia makubaliano na mvua kwamba itakua inaanza saa nne kamili usiku na kuisha kabla hakujapambazuka. Kwakweli naona makubaliano yetu yanazingatiwa na pande zote mbili na hakujatokea tatizo lolote kubwa mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom