Kuna muda unaweza jisahau kumbe ACT Wazalendo ndio chama kikuu cha Upinzani kwa mizania ya uwakilishi maeneo mbalimbali kiuongozi

Kuna Muda nasahau kabisa nikidhani CHADEMA ndo chama kikuu cha Upinzani ndo mpaka nikumbushwe kwamba ni ACT,

Labda Chadema wakiwakubali wale 19 ndo itakuwa Chama kikuu cha Upinzani!

Isiwe Tabu sana tupiganie kushika madaraka kabisa


Britanicca
Malipo ya elfu 7 yamekung'oa ubongo ! mkidhulumiwa mnakuja kulialia hapa hapa jf ! umasikini ni fedheha sana !
 
Kimakaratasi CHADEMA ni chama kikubwa zaidi of course kura za Lissu plus majimboni wanawaacha ACT zaidi ya kura 1.8m sasa unasemaje ACT ndio main opposition?

Unadai kujigawa zaidi.... Hvi ni chama gani zaidi ya CHADEMA chenye uwezo wa kusimamisha Mwenyekiti wa mtaa/kijiji walau 90% ya Tanzania? ACT tu ina wanachama laki 1 hao wagombea itawatoa wapi???

Bado hakuna mbadala wa CHADEMA ndio maana licha ya kuporwa majimbo yote bado tu ina wabunge 20!! Even though haiwatambui
Usihangaike na waliolipwa kuja jf kupiga uongo
 
Mkuu britanicca , naunga mkono hoja, ACT ndio chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Chadema ilikuwa ni zamani, sasa it's the past, kwa mambo yote ni ACT
P
We jamaa una roho ngumu sana ! kura za maoni uliambulia sifuri yenye masikio , hivi bado hukati tamaa tu ?
 
Mnaelewa maana ya chama kikuu cha upinzani nyie ?
Muulize kamanda zirro anafahamu chama kikuu cha upinzani ni kipi.
 
Mkuu britanicca , naunga mkono hoja, ACT ndio chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Chadema ilikuwa ni zamani, sasa it's the past, kwa mambo yote ni ACT
P
Mnachombeza ili waingie ulingoni muone wanavyokamatwa, Chadema wasiposhiriki uchaguzi polisi hawaonekani na matamko yao hatuyasikii wala mazoezi yao hayafanyiki.
 
Chama kikuu cha upinzani katika eneo lipi?

Kama ni bungeni its impossible kulingana na namba ndogo ya wabunge wa ACT.

Kama ni mtaani chama cha upinzani kwa sasa ni CCM.

Chama tawala mtaani ni CDM.
Na hii ndio sababu akili ya mleta mada inajua chama kikuu Tanzania ni Chadema, sio chama kikuu cha upinzani.
 
Wana uwezo mkubwa sana wa prnpaganda; angalia wanavofanya siasa issue ya wabunge wa viti maalim wakati wenyewe hawajakamisha mchakato wa kuwafukuza.
Issue ya katiba utafkiri wako serious kumbe wanajua hawawez kupata katiba wakati ukawa wana 10% ya wabunge wa kuisemea, kuipigia kura na kuandika katiba, ccm wana 90% unawashawishi vip?
Issue ya chaguzi kisingizio ni tume huru wanashindwa vby badala ya kujitathmini wanakuja na simple reason, tume ya mahera, wakurupenz na policcm. Toka awamu ya tano wamekuwa wanakwepa chaguz za marudio mpaka ule wa tamisemi 2019. Ni mabingwa propbganda. Ndio maana tunafikiri eti ni chama kikuu
Hao wabunge 19 wenyewe siku hizi wanajijua hawako upande huo ndio maana hata uwakilishi wao ni Kama kuku wenye mdondo ie halima au esta siku hizi hata kusimama kuchangia bungeni hawana ile hamasa waliokuwa nayo wakiwa wanatambulika ni wabunge wa chama flani kiujumla suala la kufukuza mwanachama ni suala la chama husika sio la serikali Sasa serikali na bunge wanawang'ang'ania hao wabunge ili ionekane Kuna uwakilishi wa wabunge wa chadema bungeni bila kujali maslahi ya umma ila ni kwa maslahi ya CCM.
Kuhusu tume ya uchaguzi hiyo ni worse maana haiko kusimamia uhalali wa mchakato wa uchaguzi ila yenyewe ndio inachagua nani ashinde, sanduku la kura ni kiini macho tu ie uchaguzi wa Jimbo la konde Zanzibar miezi mitatu iliyopita CCM walishinda kwa kishindo, Sasa mambo yakageuka ACT wakatishia kujitoa kwenye SUK basi CCM wakamshinikiza mgombea wao aliyeshinda kujiuzulu ili kuistiri SUK juzi tumeona uchaguzi wa marudio ACT eti naye kashinda kwa kishindo, hapo haihitaji sayansi au utafiti maalumu kujua kura ya kwenye sanduku haiamui nani mshindi ila kinachoamua ni kikundi Cha watu (tume ya Uchaguzi) na ndivyo inavyokua kwenye chaguzi zote pia hata hao CCM wenyewe chaguzi zao za ndani tu zimejaa figisu na fitina asilimia kubwa wagombea wao hawakubaliki na wapiga kura kwa kuwa ahadi zao hazitekelezeki wanashinda kwa rushwa, sasa kwa mazingira hayo utasemaje Kuna tume ya huru uchaguzi.
Kuhusu suala la katiba mpya ni suala la muda tu kwa sababu wanaotaka katiba mpya sio Chadema au CCM ila ni wananchi hata tume za kijaji kadhaa zilishatoa taarifa kudhibitisha Hilo ie tume za jaji nyalali na warioba zote zilionyesha Tanzania inahitaji katiba mpya kutokana na kwanza namna katiba iliyopo ilivyopatikana na pia mabadiliko mbalimbali yaliyotokea kwa kipindi chote toka ilivyotungwa ie katiba ya mwaka 1977 ilitungwa na kupitishwa na kikundi Cha watu wachache bila kuzingatia maoni ya wananchi na pia kwa kipindi kile ilitungwa kwa kuzingatia mfumo wa chama kimoja na mfumo wa uchumi wa kijamaa kwamba vyanzo vyote vikuu vya uchumi kumilikiwa na umma/serikali kwaiyo kwa hali ya Sasa mabadiliko ya katiba hayaepukiki wanayachelewesha tu kutokana kuongezeka kwa idadi watu na uelewa wao, kuingia mfumo wa vyama vingi na mabadiliko ya kiuchumi maana Sasa tupo kwenye uchumi mchanganyiko ambao serikali na binafsi wote wanamiliki vyenzo za uzalishaji mali na uchumi kwa msingi huo katiba mpya ni lazima kuendana na mabadiliko hayo na yajayo.
 
Moja ya athari kubwa taifa iliyoachiwa na mwendazake ni kujenga taifa la watu waoga, wanafiki na wanaofikiri kwa kutumia tumbo badala ya kichwa na silaha kuu ikiwa ni kujipendekeza, bahati mbaya kasumba hii haijali umri, hali, elimu wala uzoefu wa mtu na heshima aliyowahi kujijengea kwenye jamii.
 
Wote muliochangia niwapongeze,na mimi nachangia hivi....
Zaidi ya nusu ya watanzania hatuna maji saafi.
Itatuchukuwa miaka mingi kwenda kwenye next level.
Wengi wetu hatujui kama tunakwenda au tunarudi.
Tumche Mungu,kwani kufanya hivyo ndiyo chanzo cha maarifa.
 
Kuna Muda nasahau kabisa nikidhani CHADEMA ndo chama kikuu cha Upinzani ndo mpaka nikumbushwe kwamba ni ACT,

Labda Chadema wakiwakubali wale 19 ndo itakuwa Chama kikuu cha Upinzani!

Isiwe Tabu sana tupiganie kushika madaraka kabisa


Britannica
Mkuu kuna vigezo vingi ambavyo wapaswa uvitue,kikubwa ni uwiano wa kura za Uraisi, kuna vidogo kama wanachama, matawi yao, na hata madiwani. Kule tunakokaa ACT ni nadra kuona hata bendera yake. Nashanga hata Paschal Mayalla hajui.
 
Kuna Muda nasahau kabisa nikidhani CHADEMA ndo chama kikuu cha Upinzani ndo mpaka nikumbushwe kwamba ni ACT,

Labda Chadema wakiwakubali wale 19 ndo itakuwa Chama kikuu cha Upinzani!

Isiwe Tabu sana tupiganie kushika madaraka kabisa


Britanicca
Kwani Chama kikuu cha Upinzani Kina pimwaje mpaka kiitwe hivyo?
 
Chama kikuu cha upinzani katika eneo lipi?

Kama ni bungeni its impossible kulingana na namba ndogo ya wabunge wa ACT.

Kama ni mtaani chama cha upinzani kwa sasa ni CCM.

Chama tawala mtaani ni CDM.
Mtaa gani huo? Ufipa?
 
mazoea yana taabu.
P
PASCHAL, come to your sense na uwe mkweli mbele ya nafsi yako na Mungu wako, Kama bado una Imani kwa Mungu.

Hivi kukiwa na mabondia wawili mmoja kafungwa mkono mmoja asiweze kuutumia na mwingine anatumia mikono yote miwili, hapo unategea nani ashinde?

Je, ushindi huo Ni fair?

Je unawezaje kumbagaza huyo aliyeshindwa kupambana kwa kuwa tu hakupata ushindi bila kuzingatia kuwa alionewa kwa kutumia mkono mmoja wakati mpinzani wake anatumia mikono yote miwili?

Uwanja wa Siasa hauko Sawa, CHADEMA wanashikwa mkono wasiweze kupambana ipasavyo. Elewa hilo!
 
Kuna Muda nasahau kabisa nikidhani CHADEMA ndo chama kikuu cha Upinzani ndo mpaka nikumbushwe kwamba ni ACT Wazalendo.

Labda CHADEMA wakiwakubali wale 19 ndo itakuwa Chama kikuu cha Upinzani.

Isiwe Tabu sana tupiganie kushika madaraka kabisa.


Britanicca
Hahahhh Mkuu Britanica umenikumbusha jambo msingi sana... Ujue tunajisahaulisha kusudi hili jambo
 
Kwani Chama kikuu cha Upinzani Kina pimwaje mpaka kiitwe hivyo?
Chama chenye wabunge wengi wa upinzani ndio chama kikuu cha upinzan. Na ikatokea ikatokea ccm wameshinda urais halafu labda ACT ikawa na wabunge wengi 50% + na hakuna serikali mseto au za umoja wa kitaifa hapo act watatoa waziri mkuu na kuunda serikali (baraza la mawaziri) na rais atapunguziwa madaraka na kubaki kuwa ceremonial.
Hivo utagundua kuwa idadi ya wabunge ndio muhimu sio jumla ya kura wabunge wala kura za mtu kama Lisu
 
Wana uwezo mkubwa sana wa prnpaganda; angalia wanavofanya siasa issue ya wabunge wa viti maalim wakati wenyewe hawajakamisha mchakato wa kuwafukuza.
Issue ya katiba utafkiri wako serious kumbe wanajua hawawez kupata katiba wakati ukawa wana 10% ya wabunge wa kuisemea, kuipigia kura na kuandika katiba, ccm wana 90% unawashawishi vip?
Issue ya chaguzi kisingizio ni tume huru wanashindwa vby badala ya kujitathmini wanakuja na simple reason, tume ya mahera, wakurupenz na policcm. Toka awamu ya tano wamekuwa wanakwepa chaguz za marudio mpaka ule wa tamisemi 2019. Ni mabingwa propbganda. Ndio maana tunafikiri eti ni chama kikuu
Chadema inawatesa sana
 
Suala la kufukuza mwanachama ni suala la chama husika sio la serikali Sasa serikali na bunge wanawang'ang'ania hao wabunge ili ionekane Kuna uwakilishi wa wabunge wa chadema bungeni bila kujali maslahi ya umma ila ni kwa maslahi ya CCM.

Katiba za vyama zinaridhiwa na Msajili kwanza yaani Serikali. Aidha haki za wanachama zinalindwa pia na Katiba na Sheria za Nchi na SIO suala Chama pekee. Kumbuka Hamad Rashid alifukuzwa CUF lakin Mahakama ilimlinda na akabaki Mbunge, hata Zito Kabwe wa Chadema alibaki na ubunge ingawa chama chake WALITAKA KUMFUKUZA.
Leo hii mnatudanganya eti mmewafukuza wakati Rufaa yao haijasikizwa. Mimi binafsi niliwahi kufukuzwa kazi nikapewa nafasi ya kukata Rufaa Hukumu ya kufukuzwa ilisimama mpaka baada ya kusikilizwa kwa Rufaa.
Niliposhindwa Rufaa nilifukuzwa kazi, nikaenda Mahakamni nikashinda.
Hata hao covid19.., kwanza Rufaa yao haijasikilizwa je wakishinda Rufaa au wakaenda Mahakamani kama Zito au Hamad Rashid itakuwaje
 
Mkuu britanicca , naunga mkono hoja, ACT ndio chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kwa sasa. Chadema ilikuwa ni zamani, sasa it's the past, imebaki historia tuu, and soon inakwenda 6ft under, tunaisahau!. Kwa sasa mambo yote ni ACT Wazalendo.
P
Kiuhalisia ACT ni chama kikuu cha upinzani Zanzibar. Kule bara hakuna upinzani kwa mizania ile kuna mbwembwe tu,huwezi.sema.bara upinzani una kajimbo kamoja ndio useme wanacount. Let's be realistic.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom