Kuna muda huwa siwaelewi Watanzania hasa kwa tabia zao za kupenda Kukurupuka na Unafiki walizobarikiwa nazo

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Yaani leo Klabu Bingwa na Timu iliyobarikiwa Vingi na Mwenyezi Mungu ambayo kama huishabikii utakuwa na Roho ya Kishetani na Kichawi ya Simba SC imemualika Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara Mzee Abdulrahman Kinana kuwa Mgeni Rasmi itakapocheza na Orlando Pirates FC Saa 1 Kamili Usiku katika CAFCC tayari Kelele za Wapuuzi na Wanafiki zimeshaanza.

Hivi kuna Mtu asiyejua kuwa Klabu ya Yanga kwa 85% inajinasibisha na inahusishwa moja kwa moja na Chama Cha Cha Mapinduzi ( CCM ) na hata wana CCM wameshasikika sana Wakitamba hivyo?

Kama kweli nyie Wapuuzi na Wanafiki mna Uchungu sana na mnataka Haki halafu hamtaki hivi Vilabu Vikubwa na Vikongwe nchini vijihusishe na Vyama vya Siasa ( Siasa nchini ) mbona hatujawahi kuona mkiikemea Yanga SC kuwa Mali ya CCM na inasemekana hata Rangi za Klabu hiyo ziliigwa kutoka Chama Cha Mapinduzi?

Angalieni sasa mlivyo Wapuuzi na Wanafiki leo mnashupaza Mishingo yenu kwa Mzee Kinana ( Makamu Mwenyekiti CCM Bara ) kualikwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mechi ya Simba SC na Orlando Pirates FC lakini hivi Majuzi tu Mheshimiwa Rais Samia ( Mwenyekiti CCM Taifa ) alipopiga Simu katika Hafla iliyoandaliwa na Yanga SC na hadi kutoa ( Kuchangia ) Fedha Shilingi Milioni 15 wote mlinyamaza, mlifurahia na wengi Wenu Kumpongeza mno tu.

Na wengi wenu Walalamikaji Wapuuzi na Wanafiki hamjajua Akili Kubwa na ya Kimkakati iliyotumika na Simba SC katika Kumualika Leo Kinana kwani tayari wameona ni kama vile CCM ( yenye Serikali na Dola ) inaanza Kuibeba Yanga SC kwa namna moja au nyingine hivyo Simba SC nao wamekuwa Wajanja kwa kuona wasikae nyuma au Wasijitenge sana kisha huko mbeleni Wakasahaulika kuwa na Wao Dotto wanastahili Kukumbatiwa na CCM ( Serikali ) kama ambavyo Kulwa ( Yanga SC ) anafanyiwa.

Ila nami MINOCYCLINE nauliza hivi tukiachana na yote tuambieni Ukweli kwa Sasa Tanzania kuna Chama Imara cha Kisiasa kuliko CCM? Yaani nyie Wapuuzi na Wanafiki hamjui au hamjajua kuwa kwa Tanzania hii yetu na Mfumo wake wa Kisiasa kujiweka mbali na CCM ni sawa na Masikini Kumkwepa, Kumsusia na Kumnunia Tajiri aliye tayari kukubadilishia Ustawi wa Maisha yako?

Nawapongeza mno Klabu ya Simba kwa hiki walichokifanya cha Kumualika Mzee Kinana ( Makamu Mwenyekiti CCM Bara ) kwani wenye Akili Kubwa tumeshawaelewa ni wapi wanakulenga ila Wapuuzi na Wanafiki hawaelewi na wanachojua tu ni Kukurupuka na kuanza Kuulaumu Uongozi wa Simba SC kwa Uamuzi wake huu.

Mnakataa na mmechukia Mzee Kinana kuwa Mgeni Rasmi kwani mmeambiwa kuwa anaenda Kuhutubia na Kuomba Kura kwa Mkapa? Simba SC wanaalika Viongozi ambao ni Mashabiki wake na Kinana ni mwana Simba SC kindakindaki je, mlitaka aalikwe Freeman Alkaeli Mbowe ambaye kila Mtu anajua ni mwana Yanga SC lia lia?

Halafu je, mmeshaingia Akilini mwa Viongozi wa Simba SC na wakawaambia kuwa huko mbeleni katika Mechi zao mbalimbali za Ndani na Kimataifa hawatowaita hao Viongozi wenu wengine wa Vyama vya Upinzani ambao mngependa nao Waalikwe Slku moja kama ilivyokuwa kwa Mzee Kinana ( Makamu wa CCM Bara ) leo?

Kwahiyo Yanga SC kuwa na Vinasaba vyote vya Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) hadi Waandamizi kama akina Rais Mstaafu Kikwete, Waziri wa Fedha Nchemba na Waziri wa Kazi Maalum Mzee Mkuchika hadi akina Wabunge Tarimba na Ridhiwani kuwa ni sehemu ya Yanga SC kwenu ni sawa, ila leo Simba SC tu Kumualika Mzee Kinana ( Makamu Mwenyekiti CCM Bara ) kuwa Mgeni Rasmi katika Mechi yao Kwenu ndiyo imekuwa Nongwa na Mmechukia? Wapuuzi na Wanafiki wakubwa nyie.

Mnaacha kuiombea Klabu ya Simba ifanye vizuri leo ili iendelee Kuitangaza vyema Tanzania Kimataifa hasa katika Medani za Soka mmekalia tu Kushupaa katika Vitu vya Kitoto kabisa ambavyo kwa wenye Akili Kubwa na Waona Mbali wala isingekuwa na Mjadala wowote mpaka sasa mnataka Kuiwekea Kisununu Klabu yetu pendwa na Barikiwa ya Simba SC.

Mmenikera kweli ngoja niishie tu hapa.
 
Back
Top Bottom