Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 15,795
- 28,453
Kutokana na takwimu zilizo katika website ya TAMISEMI (PORALG - Local Government Revenue Collection Dashboard) ni kweli kama alivyo sema Rais Magufuli, Mkoa wa Dodoma kwa ujumla unaongoza kwa mapato kwenye huu mwaka wa fedha kwa makusanyo ya kuanzia tarehe 01/07/2018 hadi jana 31/07/2018 yani makusanyo ya mwezi moja tu. Makusanyo haya ni kwa vile vyanzo vya mapato ya halmashauri sio Serikali kuu.
Kwa kutumia takwimu hizo hizo za TAMISEMI ndio maana ninasema Rais amedanganywa aidha na Waziri wake au yeyote aliyempa taarifa hizo.
Makusanyo ya Dodoma yamejumuisha makusanyo ya Halmashauri zote 8 ni Tshs.3,670,314,500.69 (PORALG - Local Government Revenue Collection Dashboard)
na mapato kwa Mkoa wa Dar es Salaam yenye Halmashauri 6 yameonyeshwa ni Tshs.733,608,741.82 (PORALG - Local Government Revenue Collection Dashboard) kitu ambacho sio kweli kwani hayo ni mapato ya Halmashauri 2 tu yani Kigamboni na Ubungo ndio yamewekwa kwenye mfumo.
Hivyo kwa takwimu hizo, Rais Magufuli amedanganywa hata kama alikuwa anazungumzia mwaka wa fedha ulioisha 2017/2018 bado Dodoma haijafikia DSM

Last edited by a moderator: