Kuna mtu huwa anaelewa Kingereza cha Nigeria?

Kuna mtu huwa anaelewa Kingereza cha Nigeria?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
60,816
Reaction score
100,481
Hivi kuna mtu tofauti na raia wa Nigeria wenyewe huwa anaelewa English ya Nigeria? Mimi huwa sielewi Kingereza wanachozungumza Wa Nigeria hasa wa mtaani au wanamuziki na comedians wao wengi.
Screenshot_20260424-103158~2.jpg
 
Kuna press moja trump alikua anafanya na waandishi wa habar mwandishi mmoja wa kihindi akamuuliza swali trump akauliza ameongea Nini
Wanigeria na wahindi ni kazi sana kuwaelewa
Aisee nakumbuka miaka fulani ya nyuma nimesoma shule moja ya advance, sasa kulikuwa na mwalimu wa kihindi jinsia ke na alikuwa na sauti nyembamba halafu sauti kali, alivyoanza kufundisha economics paper one, nikawaambia wenzangu hapa tumefeli wote..lakn mwishowe tulimuelewa ijapo miezi miwili ya kwanza tulikuwa tumehenya!
 
I dey sabi, no wahala!
Lugha ya mtaani hiyo wanaita Nigerian pidgin
Kile unachosikia mara nyingi si English ya kawaida bali ni mchanganyiko English na lugha za asili kama Yoruba, Igbo, na nyinginezo.
Ina sarufi na msamiati wake tofauti kabisa,
Wetin - what
How far? - Mambo?
I dey fine - niko poa
No wahala - no problem
Sawa na vile Sheng ya Kenya au hata mtu wa Tz Bara hawezi kumuelewa vizuri wa Zbar ambao nao kuna wale wa Makunduchi hawawaelewi na kuna watu Dar pia ngumu kumuelewa mwenyeji aliyekulia Vingunguti, Manzese au Buguruni
 
Wahindi
Aisee nakumbuka miaka fulani ya nyuma nimesoma shule moja ya advance, sasa kulikuwa na mwalimu wa kihindi jinsia ke na alikuwa na sauti nyembamba halafu sauti kali, alivyoanza kufundisha economics paper one, nikawaambia wenzangu hapa tumefeli wote..lakn mwishowe tulimuelewa ijapo miezi miwili ya kwanza tulikuwa tumehenya!
Inaitaji moyo kwenye kuelewana haswa kama ni mgeni kwenye lafudh yao
 
I dey sabi, no wahala!
Lugha ya mtaani hiyo wanaita Nigerian pidgin
Kile unachosikia mara nyingi si English ya kawaida bali ni mchanganyiko English na lugha za asili kama Yoruba, Igbo, na nyinginezo.
Ina sarufi na msamiati wake tofauti kabisa,
Wetin - what
How far? - Mambo?
I dey fine - niko poa
No wahala - no problem
Sawa na vile Sheng ya Kenya au hata mtu wa Tz Bara hawezi kumuelewa vizuri wa Zbar ambao nao kuna wale wa Makunduchi hawawaelewi na kuna watu Dar pia kumuelewa mwenyeji aliyekulia Vingunguti, Manzese au Buguruni
Kiswahili cha Zanzibar kwa 90% kinaeleweka, Kuna maneno machache huwa yanaweza kuwa mapya lakini bado ni rahisi kuyaelewa ukivuta picha kidogo mfano skuli, tunguja, marikiti, ushanifahamu n.k
 
Pia kuna kiingereza cha waingereza wametofautiana hawa nao ni mzozo kuwaelewa.

Msikilize mwanamzuki Adele akiongea huelewi kitu
Waingereza tofauti yao ni accent zaidi, Adele akiongea kukiwa na subtitles utaelewa hao Wa Nigeria hata mfano Burna boy akiimba na subtitles bado kuelewa ni mtihani.
 
Hata wakenya kusema kweli kiswaenglish chao kinakera.

Ni shida yetu waafrika hiyo, utambulisho hatuna. Lugha zetu hatujui, na lugha za kikoloni pia hatujui, tunazichanganya.

Na hapa tz huo upumbavu umeanza, hasa kwa wanawake. Kiswahili hawajui, wanachanganya na kiingereza ambacho hawajui pia.
 
Back
Top Bottom