Alex Fredrick
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 679
- 1,337
Joto la Uchaguzi 2015 lilikuwa kubwa sana ndani ya Chama Tawala,Vigogo wengi walipewa nafasi ya kuukwaa Urais kupitia CCM lakini Edward Lowassa ndiye alikuwa Tishio kubwa
Lowassa alikuwa gumzo sio tu CCM bali hata kwenye vyama wa upinzani kiasi kwamba walipoteza Agenda zao za msingi kusikiliza Upepo ulivyokuwa unavuma CCM
Ukiacha Ukwasi wake mkubwa aliokuwa nao yeye pamoja na rafki zake lakini pia hata Mwenyekiti wake JK alikuwa hafui dafu kwa Lowassa kimkakati na kila kitu
Pamoja na hayo yote lakini mwisho wa siku Lowassa alikatwa na Kikao cha Kamati kuu kwa hoja dhaifu kwamba ana nakisi ya Uadilifu
Yeye pamoja rfk zake wote waliomuunga mkono hawakuamini kwa kile kilichotokea siku alipokatwa
Uchaguzi wa 2020 ndani ya Chama Tawala sioni Kada yoyote ambaye anaweza kuchuana na Rais Magufuli
Sioni Kada yoyote ndani ya CCM mwenye record ya uchapaji kazi mithili ya Rais Magufuli ukiachalia mbali tabia yake ya kuthubutu au maamuzi magumu ambapo hatukuzoea kuyaona huko nyuma
Na Kada yoyote ambaye anataka kuchuana na Rais Magufuli tunaomba atupe record yake alivyokuwa Kiongozi serikalini au kwenye Chama
Wengi wanaotaka Urais wanasukumwa na Visasi tu basi na sio kuja kutatua changamoto za Wananchi
Tanzania karibia miongo mitatu tumepitia changamoto nyingi hasa Rushwa kila eneo na Viongozi kutowajibika na zaidi wananachi ndio walikuwa wanawatumikia Viongozi na sio Viongozi kutumika kwa Wananchi
Pia tuliona baadhi ya Viongozi wakitengeneza watoto wao na rafiki zao kuendelea kututawala milele,Yaani tulikuwa tunaelekea kwenye Taifa la Kifalme
Rais Magufuli amekata minyororo yote hiyo na ndio sababu ya msingi ambapo wenzie hawampendi kwa maana ZAMA za ulaji Buriani ndani ya CCM
Ndani ya miaka kumi ya Rais Magufuli naamini Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa kwenye medani zote,Kimsingi tumpe muda amalize ngwe zake mbili na ndio tuanze kuhukumu
Alex Fredrick
Dar es salaam