Kuna mtu alivuma na aliisumbua CCM kama Lowassa?2020 Sioni Kada yoyote au kivuli cha kumsumbua Rais Magufuli

Mwingine nilimfahamu kupitia jina la "Kadafi" bila hivyo nisingemfahamu!
 
Natamani Sana CCM wasimpitishe MAGUFULI 2020. Ndio itakuwa mwisho wa chama kinachoitwa CCM TZ.
Magufuli akienda chama chochote anachukua nchi kwakishindo. Hakuna mpumbavu wa kuwaamini tena CCM. Kwa Sasa CCM wanatembelea nyota ya MAGUFULI. Kumbuka 2015 ilikuwa chagua MAGUFULI si CCM. na ndio pona yao. CCM HAWAAMINIKI KTK JAMII.
 
Tatizo lako ndugu yangu unadharau mwamko wa wananchi (wapinzani) dhidi ya CCM. Yaani umeshindwa kabisa kutambua waliomkosesha urais huyo Lowassa sio CCM bali ni wapinzani.

Tambua kuwa majority ya Wana CCM wakati huo ni kundi la wanamtandao ambao walishapangana Lowassa aje kuwa rais baada ya swahiba wake JK kumaliza muda wake. Lakini kelele za ufisadi wa Lowassa kutoka kwa wapinzani ziliwaamsha wapigakura dhidi ya CCM. Kelele hizi za wapinzani zilihatarisha ushindi wa ccm.

Kwakuwa walioshika mpini walijali zaidi hatma ya chama chao, iliwabidi wasaliti makubaliano ya kupokezana urais kiswahiba ili kunusuru ushindi kwa chama dhidi ya wapinzani ndipo wakamkata Lowassa.

Huyu Magufuli ingawa alisimamishwa kuokoa ushindi wa chama, bado hakuweza kukipa chama ushindi wa kishindo licha ya kuaminika hata na wapinzani kuwa "katapila/jembe". Kitakwimu, Ukweli ni kwamba Magufuli ndiye mgombea urais wa ccm aliyekipa ushindi mwembamba chama hicho kuliko wote waliowahi kugombea.

Jambo la muhimu na la kuzingatia ni kwamba, katika uchaguzi wa 2015, kutokana na kuwa underground katika medani za urais, Magufuli hakupata changamoto za mashambulizi ya kisiasa. Leo Magufuli siyo underground Tena; watu wanamjua vizuri na kuna mambo mengi mabaya yaliyotekea katika uongozi wake ambavyo yatatumiwa na wapinzani kumshambulia kisiasa. Kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi na kupambana na ufisadi pekee yake inaweza isisaidie kupata Kura za kutosha kwa wapiga Kura walioathirika na maamuzi yake ya "kuwanyoosha" na "kuelimisha wananchi kwa meno"
 
Back
Top Bottom