Kuna mtu alivuma na aliisumbua CCM kama Lowassa?2020 Sioni Kada yoyote au kivuli cha kumsumbua Rais Magufuli

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
548
1,000
Joto la Uchaguzi 2015 lilikuwa kubwa sana ndani ya Chama Tawala,Vigogo wengi walipewa nafasi ya kuukwaa Urais kupitia CCM lakini Edward Lowassa ndiye alikuwa Tishio kubwa

Lowassa alikuwa gumzo sio tu CCM bali hata kwenye vyama wa upinzani kiasi kwamba walipoteza Agenda zao za msingi kusikiliza Upepo ulivyokuwa unavuma CCM

Ukiacha Ukwasi wake mkubwa aliokuwa nao yeye pamoja na rafki zake lakini pia hata Mwenyekiti wake JK alikuwa hafui dafu kwa Lowassa kimkakati na kila kitu

Pamoja na hayo yote lakini mwisho wa siku Lowassa alikatwa na Kikao cha Kamati kuu kwa hoja dhaifu kwamba ana nakisi ya Uadilifu

Yeye pamoja rfk zake wote waliomuunga mkono hawakuamini kwa kile kilichotokea siku alipokatwa

Uchaguzi wa 2020 ndani ya Chama Tawala sioni Kada yoyote ambaye anaweza kuchuana na Rais Magufuli

Sioni Kada yoyote ndani ya CCM mwenye record ya uchapaji kazi mithili ya Rais Magufuli ukiachalia mbali tabia yake ya kuthubutu au maamuzi magumu ambapo hatukuzoea kuyaona huko nyuma

Na Kada yoyote ambaye anataka kuchuana na Rais Magufuli tunaomba atupe record yake alivyokuwa Kiongozi serikalini au kwenye Chama

Wengi wanaotaka Urais wanasukumwa na Visasi tu basi na sio kuja kutatua changamoto za Wananchi

Tanzania karibia miongo mitatu tumepitia changamoto nyingi hasa Rushwa kila eneo na Viongozi kutowajibika na zaidi wananachi ndio walikuwa wanawatumikia Viongozi na sio Viongozi kutumika kwa Wananchi

Pia tuliona baadhi ya Viongozi wakitengeneza watoto wao na rafiki zao kuendelea kututawala milele,Yaani tulikuwa tunaelekea kwenye Taifa la Kifalme

Rais Magufuli amekata minyororo yote hiyo na ndio sababu ya msingi ambapo wenzie hawampendi kwa maana ZAMA za ulaji Buriani ndani ya CCM

Ndani ya miaka kumi ya Rais Magufuli naamini Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa kwenye medani zote,Kimsingi tumpe muda amalize ngwe zake mbili na ndio tuanze kuhukumu

Alex Fredrick
Dar es salaam
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
142,496
2,000
Unapokiangalia choo kilichojengwa vizuri na kufanyiwa nakshi zote za kuvutia unaweza kudhani hakuna kitu chema kama hicho.... Na unaweza kutoa sifa zote... Lakini utakapo tambua kuwa jina choo sio jengo bali kuna uhalisia mkubwa nyuma yake unaobeba dhima yote ya neno CHOO.. Lazima utakuwa na mtazamo tofauti na huu
 
mwasipenjele

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
774
500

Daaaaa
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
3,931
2,000
ccm ni kikundi fulani hivi cha watu walioishiwa utu na aibu..
Usiwaamini sana.. wanajua jinsi ya kumtumia yule adui almaarufu kama ujinga (wa watanzania).
Kwa makusudi kabisa wamewafanya wengi wawe wajinga na wajihisi walizaliwa ili kuwa wajinga..
Amini usiamini.. walimtengeneza Lyatonga, wakampoteza Salim A. Salim, wakamtengeneza Li-Pumba, wakamtisha Lowassa..
Hawashindwi kumtisha Magufuli.. na akikomaa nao ndo mwisho wake yeye na ccm!!
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
32,058
2,000
Lowasa hakuwa na kitisho chochote ndani ya ccm bali wapambe ndio walikuwa wanampigia debe ili wamlie hela zake. Nadhani alivyopanda jukwaani kwenye kampeni ndio ilionyesha dhahiri kwamba sifa zake zililetwa na wapambe waliokuwa wanafaidika na hela zake. Yeye zaidi ya kusema kipaombele chake ni "elimu, elimu, elimu" "mabadiliko Lowasa, Lowasa mabadiliko" alikuwa na jipya gani? Hiyo ndio hofu iliyokuwa inaogopwa na ccm?

Magufuli ndani ya ccm ndio anaweza kuwababaisha lakini nje ya ccm nguvu pekee ya uhakika ya ushindi wa Magufuli ni vyombo vya dola, na tume ya uchaguzi inayohofia madaraka yake. Labda wapinzani wafanye ile upuuzi wa kina Mbowe kuchukua kapi la ccm. Hapo hakuna porojo eti kwamba kiongozi wa upinzani kafanya nini maana huna la maana unaloweza kufanya kazi iwapo hujawa madarakani. Vinginevyo atakayeleta hiyo porojo watuambie Nyerere alijenga miradi mingapi kabla ya kupewa nchi na wakoloni.
 
omtiti

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
588
1,000
Unapokiangalia choo kilichojengwa vizuri na kufanyiwa nakshi zote za kuvutia unaweza kudhani hakuna kitu chema kama hicho.... Na unaweza kutoa sifa zote... Lakini utakapo tambua kuwa jina choo sio jengo bali kuna uhalisia mkubwa nyuma yake unaobeba dhima yote ya neno CHOO.. Lazima utakuwa na mtazamo tofauti na huu
Hivyo wewe ni choo!
 
Coolant

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
880
1,000
Unapokiangalia choo kilichojengwa vizuri na kufanyiwa nakshi zote za kuvutia unaweza kudhani hakuna kitu chema kama hicho.... Na unaweza kutoa sifa zote... Lakini utakapo tambua kuwa jina choo sio jengo bali kuna uhalisia mkubwa nyuma yake unaobeba dhima yote ya neno CHOO.. Lazima utakuwa na mtazamo tofauti na huu
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,303
2,000
Sasa kaka mkubwa unapotaka kuonesha mahaba usichanganye mambo

Kama unakubali Lowasa alikuwa tishio hasa kwa CCM na hata nje ya CCM lakini kamati kuu ilimkata na hakuamini, kwanini hutaki kukubali kuwa kamati kuu inaweza kumkata hata jamaa wa sasa na watu wasiamini!

Boss usiichukulie dhamana siasa! Itakufanya mtumwa alafu ikufanye kitu hautaamini
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,842
2,000
Unapokiangalia choo kilichojengwa vizuri na kufanyiwa nakshi zote za kuvutia unaweza kudhani hakuna kitu chema kama hicho.... Na unaweza kutoa sifa zote... Lakini utakapo tambua kuwa jina choo sio jengo bali kuna uhalisia mkubwa nyuma yake unaobeba dhima yote ya neno CHOO.. Lazima utakuwa na mtazamo tofauti na huu
Message nzuri sana hata kwa wale wanaoamini kwamba chadema (hii ya sasa) na kamanda anayesaliti nchi yake kwa mabeberu ndo hope yetu ya ukombozi. Wakitoka ndani ya hilo box lao ndo watauona ukweli kwamba ni afadhali kutoacha mbachao kwa msala unaopita.
 
Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
548
1,000
Nakuonyesha msuli wa Lowassa na hawa wingine ambao hawana record yoyote zaidi ya visasi eti ndo wapewe Nchi. Serious?
 
modavid

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
537
500
Unapokiangalia choo kilichojengwa vizuri na kufanyiwa nakshi zote za kuvutia unaweza kudhani hakuna kitu chema kama hicho.... Na unaweza kutoa sifa zote... Lakini utakapo tambua kuwa jina choo sio jengo bali kuna uhalisia mkubwa nyuma yake unaobeba dhima yote ya neno CHOO.. Lazima utakuwa na mtazamo tofauti na huu
Watakuelewa wachache
 
NJOLO

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
545
1,000
Tukitaka kitathimini uwezo na nguvu ya Kampuni yoyote katika biashara tunaangalia vitu viwili muhimu.
1. Uwezo wa rasilimali fedha Kifedha (Financial resource).
2. uwezo wa rasilimali watu. (Human resource).
Katika siasa ni hivyo hivyo.
Lowasa hakuwa na kitu cha ajabu cha kuwavutia watu isipokuwa uwezo mkubwa wa kifedha aliokuwa nao na rasilimali watu alioiandaa bila kumsahau yeye kuwa ni sehemu muhimu ya rasilimali hiyo (Human resource).
Kilichomkwamisha Lowasa kutokushinda ni hali yake ya afya ambayo ndiyo ilidhoofisha human resource muhimu katika malengo na madhumuni yake.
Sasa hivi vyama karibu vyote vya siasa ni dhaifu sana katika swala Zima la uwezo wa kifedha (financial resource).
Kwa vyovyote hata kama wana nguvu kazi nzuri kiasi gani, hawawezi kukishinda chama ambacho kiko vizuri katika uwezo wa kifedha na rasilimali watu na hasa kama wanainchi wanajua kua hakuna ufisadi katika uwezo huo wa kifedha.
Tukumpuke pia, kuwa uwezo wa kifedha wa Lowasa ulikuwa unatiliwa mashaka na watu wengi kuwa haukupatikana kihalali.
Hii nayo ilikuwa ni dosari kubwa iliyomnyima kura nyingi.
Kitendo cha mpinzani wake kupiga push up kwenye campaign zake ilikuwa inapeleka ujumbe kwa wapiga kura kuwa mpinzani wake mkuu ni mgonjwa na hawezi kupiga push up.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
142,496
2,000
Message nzuri sana hata kwa wale wanaoamini kwamba chadema (hii ya sasa) na kamanda anayesaliti nchi yake kwa mabeberu ndo hope yetu ya ukombozi. Wakitoka ndani ya hilo box lao ndo watauona ukweli kwamba ni afadhali kutoacha mbachao kwa msala unaopita.
Umepotoka na unapotosha... Kujisaidia porini na kujisaidia maliwatoni kipi bora... USIPOTOSHE
 
CCM MKAMBARANI

JF-Expert Member
Mar 15, 2017
781
500
CCM imeshakuwa safi na itashinda siku nyingi sana zijazo, japo ni kweli ushawishi wa CCm ulipungua lakini Rais Magufuli amesaidia kufufua jitihada za chama kuleta maendeleo.
 
Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
548
1,000
Tukitaka kitathimini uwezo na nguvu ya Kampuni yoyote katika biashara tunaangalia vitu viwili muhimu.
1. Uwezo wa rasilimali fedha Kifedha (Financial resource).
2. uwezo wa rasilimali watu. (Human resource).
Katika siasa ni hivyo hivyo.
Lowasa hakuwa na kitu cha ajabu cha kuwavutia watu isipokuwa uwezo mkubwa wa kifedha aliokuwa nao na rasilimali watu alioiandaa bila kumsahau yeye kuwa ni sehemu muhimu ya rasilimali hiyo (Human resource).
Kilichomkwamisha Lowasa kutokushinda ni hali yake ya afya ambayo ndiyo ilidhoofisha human resource muhimu katika malengo na madhumuni yake.
Sasa hivi vyama karibu vyote vya siasa ni dhaifu sana katika swala Zima la uwezo wa kifedha (financial resource).
Kwa vyovyote hata kama wana nguvu kazi nzuri kiasi gani, hawawezi kukishinda chama ambacho kiko vizuri katika uwezo wa kifedha na rasilimali watu na hasa kama wanainchi wanajua kua hakuna ufisadi katika uwezo huo wa kifedha.
Tukumpuke pia, kuwa uwezo wa kifedha wa Lowasa ulikuwa unatiliwa mashaka na watu wengi kuwa haukupatikana kihalali.
Hii nayo ilikuwa ni dosari kubwa iliyomnyima kura nyingi.
Kitendo cha mpinzani wake kupiga push up kwenye campaign zake ilikuwa inapeleka ujumbe kwa wapiga kura kuwa mpinzani wake mkuu ni mgonjwa na hawezi kupiga push up.
Hoja kubwa kwenye andiko ni kwamba sioni mtu au Kada sampuli ya Lowassa ambaye ana msuli wa kupimana na Rais Magufuli ndani CCM au nje ya CCM kwa maana Rais Magufuli anakete nyingi za kuendelea kuongoza Nchi pasi na mashaka yoyote
 
MKUYENGE

JF-Expert Member
Jun 26, 2019
4,153
2,000
Joto la Uchaguzi 2015 lilikuwa kubwa sana ndani ya Chama Tawala,Vigogo wengi walipewa nafasi ya kuukwaa Urais kupitia CCM lakini Edward Lowassa ndiye alikuwa Tishio kubwa

Lowassa alikuwa gumzo sio tu CCM bali hata kwenye vyama wa upinzani kiasi kwamba walipoteza Agenda zao za msingi kusikiliza Upepo ulivyokuwa unavuma CCM

Ukiacha Ukwasi wake mkubwa aliokuwa nao yeye pamoja na rafki zake lakini pia hata Mwenyekiti wake JK alikuwa hafui dafu kwa Lowassa kimkakati na kila kitu

Pamoja na hayo yote lakini mwisho wa siku Lowassa alikatwa na Kikao cha Kamati kuu kwa hoja dhaifu kwamba ana nakisi ya Uadilifu

Yeye pamoja rfk zake wote waliomuunga mkono hawakuamini kwa kile kilichotokea siku alipokatwa

Uchaguzi wa 2020 ndani ya Chama Tawala sioni Kada yoyote ambaye anaweza kuchuana na Rais Magufuli

Sioni Kada yoyote ndani ya CCM mwenye record ya uchapaji kazi mithili ya Rais Magufuli ukiachalia mbali tabia yake ya kuthubutu au maamuzi magumu ambapo hatukuzoea kuyaona huko nyuma

Na Kada yoyote ambaye anataka kuchuana na Rais Magufuli tunaomba atupe record yake alivyokuwa Kiongozi serikalini au kwenye Chama

Wengi wanaotaka Urais wanasukumwa na Visasi tu basi na sio kuja kutatua changamoto za Wananchi

Tanzania karibia miongo mitatu tumepitia changamoto nyingi hasa Rushwa kila eneo na Viongozi kutowajibika na zaidi wananachi ndio walikuwa wanawatumikia Viongozi na sio Viongozi kutumika kwa Wananchi

Pia tuliona baadhi ya Viongozi wakitengeneza watoto wao na rafiki zao kuendelea kututawala milele,Yaani tulikuwa tunaelekea kwenye Taifa la Kifalme

Rais Magufuli amekata minyororo yote hiyo na ndio sababu ya msingi ambapo wenzie hawampendi kwa maana ZAMA za ulaji Buriani ndani ya CCM

Ndani ya miaka kumi ya Rais Magufuli naamini Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa kwenye medani zote,Kimsingi tumpe muda amalize ngwe zake mbili na ndio tuanze kuhukumu

Alex Fredrick
Dar es salaam
KAZI NA BATA MEMBE
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom