Kuna Mtanzania bado anaamini nchi hii ni masikini na inahitaji misaada zaidi kujikwamua?

Jk alipotoka madarakani aliacha deni la taifa
Likiwa trillion 43,akaingia jpm kipindi chake
Deni likapanda mpaka trillion 61

Ova

inaonesha hujui kitu ngoja tuweke sawa
mpka anatoka nyerere madarakani deni lilikuwa trilion 3
mzee mwinyi alipotoka baada ya miaka 10 alikopa mpka kufikia trilioni 18 alipoingia mzee mkapa alifanikiwa kulipunguza mpka kufikia trilioni 10, mzee kikwete akakopa mpka kufikia trilion 35 kwa kipindi cha miaka 10 alipoingia Jiwe kwa miaka mitano tu liliongezeka mpka kufikia trilion 63, ndiye raisi alieongeza deni kuliko wote tena kwa mda mchache tu, ameligharimu taifa kwa kiasi kikubwa sana
 
Nawauliza watanzania, nchi hii ni maskini kweli au inakosa viongozi wenye maono?

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani Kikwete alitembeza sana bakuri ughaibuni,tulivyoambulia ni pamoja na vyandarua toka USA

Magufuli akaingia madarakani slogan yake akasema nchi hii si maskini ,ina kila aina ya utajiri ,akasisitiza watanzania tuchape kazi na ndani ya muda mfupi alifanya maajabu,shahidi ni Rais wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,mara kwa mara alikiri hadharani juu kazi nzuri ya hayati Magufuli,

Ifahamike mzee huyu ni mchamungu haswa.

Zama za MAGUFULI zimepita.

Awamu ya sita imeingia naona kama tunaanza kulemazwa na misaada uchwara tena,walewale ambao wanafahamu sisi ni matajiri kwa raslimali zetu ndio wako mstari wa mbele na vijimisaada.nasi tunashangilia kweli kweli.

Je, tunahitaji misaada ama tunahitaji viongozi wenye maono ya kuhakikisha neno maskini linafutika midomoni mwetu.

Na kwanini kiongozi anayejaribu kutufumbua macho anakuwa adui kwa hawa wanaotubatiza umaskini?

Huu unaoitwa umaskini ni wa kweli au ni ukosefu wa akili ,uzalendo na maarifa?

Jamaa badala watupe ndoano tuvue samaki kazi yao ni kutupatia samaki wa kula ,nini kilicho nyuma ya hii ajenda?

"Mtanikukumbuka "alisema kiumbe mmoja
Mpaka sasa Magufuli anashikiria rekodi ya kukopa pesa nyingi kuliko raisi yoyote katika kipindi kifupi.
Angalia mikopo serikali ya Magufuli iliyokopa world Bank.

Standard gauge ela imekopwa Kwa mabeberu Sweden na Norway kupitia standard chartered Bank.
Tanzania signs $1.46 billion loan for standard gauge railway construction

Mpaka mwaka 2020 deni la Taifa lilifika Zaid ya shilling trilioni 70 Sawa na 54% ya uchumi wetu.
Tanzania's debt surging, but government says it’s still sustainable | The East African

Wakati mtangulizi wake alikuwa deni la Taifa mwaka 2005 ni Dola bilioni 7 ndani ya miaka 10 deni la Taifa likaongezeka mpaka dola bilioni 18,2015 yaani ongezeko la Dola bilioni 11.

Wakati raisi Magufuli deni la Taifa lilifika Dola bilioni 30.63, ongezeko la bilioni 12 ndani ya miaka mitano Tu.

Tz ni nchi masikini sana na tupo ndani ya nchi 33 masikini zaidi duniani Kwa kuzingatia GNI per capita, kutembeza bakuli hakuepukiki na punguzeni propaganda hazifai.
 
inaonesha hujui kitu ngoja tuweke sawa
mpka anatoka nyerere madarakani deni lilikuwa trilion 3
mzee mwinyi alipotoka baada ya miaka 10 alikopa mpka kufikia trilioni 18 alipoingia mzee mkapa alifanikiwa kulipunguza mpka kufikia trilioni 10, mzee kikwete akakopa mpka kufikia trilion 35 kwa kipindi cha miaka 10 alipoingia Jiwe kwa miaka mitano tu liliongezeka mpka kufikia trilion 63, ndiye raisi alieongeza deni kuliko wote tena kwa mda mchache tu, ameligharimu taifa kwa kiasi kikubwa sana
Mule mule lakini deni linapaaa tu

Ova
 
Wapumbavu wa mwendakuzimu wala hamuwezi kuisha na mtaendelea kuweweseka kenge nyinyi.

Shetani wenu ndio amesababisha MCC wakawithdraw msaada wa mradi wa dola million 700 kwa sababu ya kenge nyinyi.

Umeme wa Rea ni msaada kutoka kwa mabeberu, barabara mikoani zimewekwa lami kwa hisani ya watu wa marekani, lakini kenge mmoja umevimbiwa makande unakuja kujamba JF? Hovyo kabisa. View attachment 1979962
Umetoa povu hujajibu swali,
Au unaunga mkomo kuwa wewe ni masikini na si viongozi wanaotuangusha?
 
Mkuu inaonekana unaeamini katika misaada,au nyie ni wanufaika binafsi wa hiyo misaada?,si hilo povu tutajikomboa kwa kufanya kazi na ubunifu ,sio misaada ,misaada mingine ndio maana tunaambiwa turuhusu na ndoa za jinsia moja , "wake up gay"
Ooh my Allah
Hapo mwisho duh hatariiiiiii.
 
Maajabu yaliyofanyika ndiyo yanalipwa na tozo sasa hivi. Mkitaka serikali ifanye maajabu kubalini pia kulipa tozo na mkubali mfumuko wa bei. Hii ni basic Economics ambayo haikwepeki.

High government spending = High taxes and inflation.
Ukiwambia wanakosea=umetumwa na mabeberu and they build a case on you for economic sabotage
 
nchi hii ni masikini tena wa kutupwa hata aje nani,sema atakuza tu uchumi wa kwenye makaratasi na kuboresha kidogo maisha ya wananchi,kupunguza rushwa kubwa na kuweka mfumo thabiti wa kutoa haki, lakini kusema itafika siku tusiombe misaada au tuwe kama singapore,hatuhitaji mabadiliko yetu ya ndani pekee bali mfumo wa biashara na uchumi duniani ubadilishwe,yale mamwamba hata tu china hayaturuhusu turukute tuwe nayo sawa kwenye kuhodhi uchumi wa dunia hata tu wetu,mwl Nyerere na misimamo yake mikali kwa sehemu kubwa aliangushwa na haya madubwana, mazao aliyoyategemea kuingiza pesa nyingi za kigeni yakaua sokoni, vita ya kagera yakamwambia nunua cash silaha,WB na IMF zikatutenga. itatuchukua karne nyingi sana kuanza kutengeneza mitambo yetu ya kuchimba dhahabu,kuchimba gas,n.k. mwangalie IRAN na mafuta yake lakini yamemkaba kwelikweli!!! habari ya uchumi kabisa wa kujitegemea percee siyo rahisi kihivyo
 
kujisahihisha ni pamoja na kuiondoa ccm madarakani
Tatizo upinzani hawapo serious kuongoza nchi.
Tunajikuta hatuna option.
Upinzani ulikuwa ule wa CDM 2005-2015. baada ya kuuza chama wamekuwa hawana hoja wala Sera za kuwaunganisha wananchi.
 
Nakijua Sana hamna kitu pale.Wale ni waathirika wa mawazo ya kikomunist na ujamaa.Watawala wa kiafrica baada ya kushindwa kuwaletea waafrika maendeleo baada ya mbwembe za kuwafurusha wakoloni wakawatumia watu kama kina walter rodney kuwafeed wanafunzi uongo wa kuwatupia lawama wazungu juu kushindwa kwa watawala.Ukoloni mambo leo sijui ubepari hizi filisofia ziliasisiwa Urusi kwenye chuo cha patrick lumumba enzi za vita baridi lengo kuu la Mrusi ni kupandikiza sumu ya chuki dhidi ya ulaya kwa waafrika Ili kupata sapoti ikiwemo kuwabrainwash waafrika waamini matatizo yao yameletwa na Mzungu.
Hicho kitabu kina mawazo ya kikomunist mawazo ya zamani ambayo siyo tija.Kama mwanasiasa analipwa pesa nyingi kuliko msomi kwann msomi asikimbilie ulaya kulipwa pesa nyingi?
Sasa kwanini aliuliwa?
 
Tatizo upinzani hawapo serious kuongoza nchi.
Tunajikuta hatuna option.
Upinzani ulikuwa ule wa CDM 2005-2015. baada ya kuuza chama wamekuwa hawana hoja wala Sera za kuwaunganisha wananchi.

Msema kweli tume huru ndiyo itakayo amua mbivu na mbichi, achana na hii ya ccm inayojipigia kura vichochoroni, ccm haijawahi kushinda uchaguzi na haitakuja kushinda,
 
Mkuu inaonekana unaeamini katika misaada,au nyie ni wanufaika binafsi wa hiyo misaada?,si hilo povu tutajikomboa kwa kufanya kazi na ubunifu ,sio misaada ,misaada mingine ndio maana tunaambiwa turuhusu na ndoa za jinsia moja , "wake up gay"
Ila kuna mamb ni lazima tuwe wakwel, hatujafikia levels za kujitegemea tatizo ni hii misingi ya utegemez tang enzi. Huez mlaumu mtu kwasasa eti anasapoti utegemez while ndio ukweriii na msema kweri na mpenz wa MUNGU!! Tusikatae uhalisia hautotusaidia tatizo ni mfumo!!
 
Nawauliza watanzania, nchi hii ni maskini kweli au inakosa viongozi wenye maono?

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani Kikwete alitembeza sana bakuri ughaibuni,tulivyoambulia ni pamoja na vyandarua toka USA

Magufuli akaingia madarakani slogan yake akasema nchi hii si maskini ,ina kila aina ya utajiri ,akasisitiza watanzania tuchape kazi na ndani ya muda mfupi alifanya maajabu,shahidi ni Rais wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,mara kwa mara alikiri hadharani juu kazi nzuri ya hayati Magufuli,

Ifahamike mzee huyu ni mchamungu haswa.

Zama za MAGUFULI zimepita.

Awamu ya sita imeingia naona kama tunaanza kulemazwa na misaada uchwara tena,walewale ambao wanafahamu sisi ni matajiri kwa raslimali zetu ndio wako mstari wa mbele na vijimisaada.nasi tunashangilia kweli kweli.

Je, tunahitaji misaada ama tunahitaji viongozi wenye maono ya kuhakikisha neno maskini linafutika midomoni mwetu.

Na kwanini kiongozi anayejaribu kutufumbua macho anakuwa adui kwa hawa wanaotubatiza umaskini?

Huu unaoitwa umaskini ni wa kweli au ni ukosefu wa akili ,uzalendo na maarifa?

Jamaa badala watupe ndoano tuvue samaki kazi yao ni kutupatia samaki wa kula ,nini kilicho nyuma ya hii ajenda?

"Mtanikukumbuka "alisema kiumbe mmoja
Umeongea point mkuu, tatizo hili si Tanzania tu ila Afrika nzima hatuna viongozi wa maana labda Rwanda peke yake.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom