Kuna Mtanzania bado anaamini nchi hii ni masikini na inahitaji misaada zaidi kujikwamua?

Wakoloni waliwajengea watz mentality za utajiri Ili wengi walipe kodi kupitia uzalishaji mashambani na viwanda na kwenye biashara. Nyerere na Sokoine wakawajengea watz mentality za umasikini kwa kuwaletea ujamaa Ili wawatawale,.Enzi ya mkoloni wapo watz wengi tu walikuwa wanamiliki utajiri kupitia kilimo, biashara nk baada ya UHURU walipigwa uhujumu uchumi wote wakafilisiwa, wajanja wakakimbilia Kenya na nchi za jirani, alichofanya mwendazake ni copy and paste ya Nyerere na Sokoine kuwafanya matajiri wawe masikini.Mkoloni hakuwa na shida na mwafrika kumiliki mali.Itikadi ya umasikini Iliingizwa nchini tokea China baada ya kucopy na paste ujamaa ambao lengo kuu la ujamaa ni kuwatawala watu kwa kuwafanya wawe masikini maana huwezi mtawala tajiri bali unamuongoza.kuongoza na kutawala ni vitu viwili. matajiri wamekuja kuanzia kuchomoza alipoingia Mwinyi madarakani huku itikadi ya umasikini ikiwa bado imetamalaki kwa wtz wengi kwa kubatizwa msamiati mpya wa unyonge.
Unyonge ndio umasikini huohuo sema lugha imeboreshwa.
Pointless!
 
Kwani RAIA wanahitaji CCM au viongozi bora?
RAIA wanahitaji uongozi bora sio vingine.
Kuna faida gani kuitoa CCM 'A' nakuiweka CCM 'B'? kwa maana yako hiyo tukiichoka CCM ndio tuchague chochote kilicho mbele yetu?
Heri zimwi likujualo! Bado km nchi tunamuda wakujisahihisha

kujisahihisha ni pamoja na kuiondoa ccm madarakani
 
Pointless!
Tafuta historia halisi achana na ya darasani iliyochujwa kwa maslai ya watawala kuhalalisha kushindwa kwao kuleta maendeleo wakawatupia wakoloni lawama.
Toka lini kutawaliwa kunaifanya nchi kuwa masikini.
 
Omba omba ni tabia na ukishakuwanayo, huwezi kuiacha mpaka mtoaji aache kutoa.

Ikiwa watoaji bado wanaendelea kutoa, wavivu wa utumiaji wa ubongo wataendelea kuamini katika misaada.

Ni wajibu wa vyama vya siasa waje na siasa/maono mapya katika hili.
Well said
 
Kusema sisi ni matajiri wakati hatuna teknolojia ya kufua umeme ni kujidanganya. Kusema sisi ni matajiri wakati tunategemea pesa ya utalii ni kujipa matumaini bandia.

Kusema sisi ni matajiri wakati chanjo ni ya mzungu ni kujidanganya ni kujipa matumaini ya kuwa siku moja tutakuwa na uwezo na mamlaka juu ya kila tulichobarikiwa na Mungu.

Hayati JPM alitujaza kiburi ambacho hatua inayofuata ilitakiwa iwe ni kukuza uwezo wetu ili tuendane sambamba na kile tulichopewa na Mungu.

Unabaki kuwa ni mtazamo wako ,na ni wa kindezi kweli
 
Tatizo kubwa la Tanzania ndilo tatizo la nchi nyingi za bara la Afrika. Waafrika sisi ni wabinafsi sana. Wakati tunakuwa wabinafsi kiasi hicho pia tunaandamwa na ushamba wa madaraka. Mwafrika akishika madaraka anajua sasa wakati wa kuwa juu ya sheria umefika (na si yeye tu hata ndugu, marafiki na sisi wengine huku mtaani tunategemea jamaa asibabaishwe na polisi kwani ni mheshimiwa, akifika sehemu atetemekewe, anyeyekewe, )- na kwa kujilinda tunasema hiyo ndiyo demokrasia ya Afrika- akili zetu vituko sana.
Mpaka hapo tutakapoachana na hizi kasumba na kutambua kuwa nafasi ya kuongoza ni nafasi ya wewe kutuonyesha kipaji chako na siyo kutuibia na umwamba wako.
 
J

Je, kwa wale ambao hawakupiga kumbuka biashara nyingi zilikopa kwenye mabenki ,unadhani ninini kilitokea kwakutokulipa madeni kwa zaidi ya miaka 4 ama zaidi "many business were closed and confiscated'
Nakuhakikishia uhakiki haukusumbua kwa wafanyabiashara wakweli,unamwaga tripu 10 za mawe halafu ulipwe pesa ya tripu 30 harakaharaka,hili lilifanikiwa awamu ya nne ,mwamba alipoingia alikuwa ni mkali wa double check na ndio principle ya mwana mahesabu yoyote yule makini
 
Nawauliza watanzania, nchi hii ni maskini kweli au inakosa viongozi wenye maono?

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani Kikwete alitembeza sana bakuri ughaibuni,tulivyoambulia ni pamoja na vyandarua toka USA

Magufuli akaingia madarakani slogan yake akasema nchi hii si maskini ,ina kila aina ya utajiri ,akasisitiza watanzania tuchape kazi na ndani ya muda mfupi alifanya maajabu,shahidi ni Rais wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,mara kwa mara alikiri hadharani juu kazi nzuri ya hayati Magufuli,

Ifahamike mzee huyu ni mchamungu haswa.

Zama za MAGUFULI zimepita.

Awamu ya sita imeingia naona kama tunaanza kulemazwa na misaada uchwara tena,walewale ambao wanafahamu sisi ni matajiri kwa raslimali zetu ndio wako mstari wa mbele na vijimisaada.nasi tunashangilia kweli kweli.

Je, tunahitaji misaada ama tunahitaji viongozi wenye maono ya kuhakikisha neno maskini linafutika midomoni mwetu.

Na kwanini kiongozi anayejaribu kutufumbua macho anakuwa adui kwa hawa wanaotubatiza umaskini?

Huu unaoitwa umaskini ni wa kweli au ni ukosefu wa akili ,uzalendo na maarifa?

Jamaa badala watupe ndoano tuvue samaki kazi yao ni kutupatia samaki wa kula ,nini kilicho nyuma ya hii ajenda?

"Mtanikukumbuka "alisema kiumbe mmoja
Magufuli alikopa matrilioni na angekuwa hai leo tungakuwa kwenye deni lisilolipika. Itachukua miaka mingi kuiponya nchi na madhara ya Magufuli na genge lake.
 
Tafuta historia halisi achana na ya darasani iliyochujwa kwa maslai ya watawala kuhalalisha kushindwa kwao kuleta maendeleo wakawatupia wakoloni lawama.
Toka lini kutawaliwa kunaifanya nchi kuwa masikini.
Soma kitabu kimoja cha Walter Rodney,uamshe ubongo wako ,kinaitwa "How Europe underdeveloped Afrika ",upate madini ,huyu jamaa walim- assassinate ,baada ya kuwapa makavu
 
Magufuli alikopa matrilioni na angekuwa hai leo tungakuwa kwenye deni lisilolipika. Itachukua miaka mingi kuiponya nchi na madhara ya Magufuli na genge lake.
Kuna kukopa kwa ajili ya anasa, Magufuli alikopa kwa ajili ya ustawi wa Taifa
 
Tatizo kubwa la Tanzania ndilo tatizo la nchi nyingi za bara la Afrika. Waafrika sisi ni wabinafsi sana. Wakati tunakuwa wabinafsi kiasi hicho pia tunaandamwa na ushamba wa madaraka. Mwafrika akishika madaraka anajua sasa wakati wa kuwa juu ya sheria umefika (na si yeye tu hata ndugu, marafiki na sisi wengine huku mtaani tunategemea jamaa asibabaishwe na polisi kwani ni mheshimiwa, akifika sehemu atetemekewe, anyeyekewe, )- na kwa kujilinda tunasema hiyo ndiyo demokrasia ya Afrika- akili zetu vituko sana.
Mpaka hapo tutakapoachana na hizi kasumba na kutambua kuwa nafasi ya kuongoza ni nafasi ya wewe kutuonyesha kipaji chako na siyo kutuibia na umwamba wako.
Kujimwambafai
 
Soma kitabu kimoja cha Walter Rodney,uamshe ubongo wako ,kinaitwa "How Europe underdeveloped Afrika ",upate madini ,huyu jamaa walim- assassinate ,baada ya kuwapa makavu
Nakijua Sana hamna kitu pale.Wale ni waathirika wa mawazo ya kikomunist na ujamaa.Watawala wa kiafrica baada ya kushindwa kuwaletea waafrika maendeleo baada ya mbwembe za kuwafurusha wakoloni wakawatumia watu kama kina walter rodney kuwafeed wanafunzi uongo wa kuwatupia lawama wazungu juu kushindwa kwa watawala.Ukoloni mambo leo sijui ubepari hizi filisofia ziliasisiwa Urusi kwenye chuo cha patrick lumumba enzi za vita baridi lengo kuu la Mrusi ni kupandikiza sumu ya chuki dhidi ya ulaya kwa waafrika Ili kupata sapoti ikiwemo kuwabrainwash waafrika waamini matatizo yao yameletwa na Mzungu.
Hicho kitabu kina mawazo ya kikomunist mawazo ya zamani ambayo siyo tija.Kama mwanasiasa analipwa pesa nyingi kuliko msomi kwann msomi asikimbilie ulaya kulipwa pesa nyingi?
 
Maajabu yaliyofanyika ndiyo yanalipwa na tozo sasa hivi. Mkitaka serikali ifanye maajabu kubalini pia kulipa tozo na mkubali mfumuko wa bei. Hii ni basic Economics ambayo haikwepeki.

High government spending = High taxes and inflation.
 
Back
Top Bottom