thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Pointless!Wakoloni waliwajengea watz mentality za utajiri Ili wengi walipe kodi kupitia uzalishaji mashambani na viwanda na kwenye biashara. Nyerere na Sokoine wakawajengea watz mentality za umasikini kwa kuwaletea ujamaa Ili wawatawale,.Enzi ya mkoloni wapo watz wengi tu walikuwa wanamiliki utajiri kupitia kilimo, biashara nk baada ya UHURU walipigwa uhujumu uchumi wote wakafilisiwa, wajanja wakakimbilia Kenya na nchi za jirani, alichofanya mwendazake ni copy and paste ya Nyerere na Sokoine kuwafanya matajiri wawe masikini.Mkoloni hakuwa na shida na mwafrika kumiliki mali.Itikadi ya umasikini Iliingizwa nchini tokea China baada ya kucopy na paste ujamaa ambao lengo kuu la ujamaa ni kuwatawala watu kwa kuwafanya wawe masikini maana huwezi mtawala tajiri bali unamuongoza.kuongoza na kutawala ni vitu viwili. matajiri wamekuja kuanzia kuchomoza alipoingia Mwinyi madarakani huku itikadi ya umasikini ikiwa bado imetamalaki kwa wtz wengi kwa kubatizwa msamiati mpya wa unyonge.
Unyonge ndio umasikini huohuo sema lugha imeboreshwa.