Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,803
- 30,743
Heshima sana wanajamvi,
Wakati serekali ya awamu ya tano ilipoanza rasmi kazi Rais Mheshimiwa,Mtukufu Dr John Pombe Magufuli alianzisha msako wa watumishi hewa na tulipewa mrejesho zaidi ya watumishi hewa 10,000 waligunduliwa katika mikoa yote Tanzania bara au ukipenda Tanganyika.
Naipongeza sana serekali kwa kubaini chanzo cha upotevu mkubwa wa fedha za serekali.Lakini pia nashindwa kuamini kama kweli idadi hiyo ilikuwepo na ikiwa ilikuwepo ni kwanini wale wote waliosababisha au kufaidika na wafanyakazi hewa hawajafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuisababishia serekali hasara kubwa kiasi hicho.
Nikiondoka katika eneo la wafanyakazi hewa ambao tunaambiwa hawakuwepo makazini (walisahakufa,walishastaafu,walishafukuzwa kazi na nk)Lipo tatizo lingine kubwa tena kubwa kubwa kuliko wafanyakazi hewa tulioambiwa na Mheshimiwa,Mtukufu Dr Magufuli ambalo ni WAFANYAZI waliopo katika ajira za serekali na taasisi zake wasiokuwa na kazi za kufanya.Unamkuta mfanyakazi katoka nyumbani kaenda kazini kuanzia asubuhi hadi jioni hana kazi aliyofanya ?.Hili liko katika ofisi za wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,wakurugenzi wa miji na majiji.
Mfano Jiji la Arusha limeachukua kazi za kukusanya ushuru wa parking za magari,utashangaa watumishi wa Jiji kutoka idara mbali mbali (wasiokuwa na kazi) wamepelekwa katika viunga mbali mbali vya Jiji la Arusha kwaajili ya kukusanya ushuru huo.Jiulize kama walikuwa na kazi kweli wasingepelekwa kukusanya ushuru wa parking lakini kwakuwa hawana kazi ndio maana imekuwa rahisi Mkurugenzi wa Jiji kuwatupa mitaani na kufanya kazi ambazo zipo.Huu ni mfano mdogo tembelea maofisi mengi ya serekali utakuta watumishi kibao wasiokuwa na kazi kutwa nzima wanasogoa tu au wanafanyakazi ya kugonga mihuri barua ?.
Serekali ya Mheshimiwa Mtukufu Dr Magufuli yafaa baada ya kumalizika zoezi la kuhakiki wafanyakazi hewa wakaingia katika zoezi lingine la kuhakiki wafanyakazi wasikokuwa na kazi za kufanya wakawalipa stahili zao wakawabakiza wanastahili kubaki na kuwalipa vizuri.
Naomba kuwasilisha.