Kuna mrundikano wa watumishi Serikalini

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
15,078
2,000
Heshima sana wanajamvi,

Wakati serekali ya awamu ya tano ilipoanza rasmi kazi Rais Mheshimiwa,Mtukufu Dr John Pombe Magufuli alianzisha msako wa watumishi hewa na tulipewa mrejesho zaidi ya watumishi hewa 10,000 waligunduliwa katika mikoa yote Tanzania bara au ukipenda Tanganyika.

Naipongeza sana serekali kwa kubaini chanzo cha upotevu mkubwa wa fedha za serekali.Lakini pia nashindwa kuamini kama kweli idadi hiyo ilikuwepo na ikiwa ilikuwepo ni kwanini wale wote waliosababisha au kufaidika na wafanyakazi hewa hawajafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuisababishia serekali hasara kubwa kiasi hicho.

Nikiondoka katika eneo la wafanyakazi hewa ambao tunaambiwa hawakuwepo makazini (walisahakufa,walishastaafu,walishafukuzwa kazi na nk)Lipo tatizo lingine kubwa tena kubwa kubwa kuliko wafanyakazi hewa tulioambiwa na Mheshimiwa,Mtukufu Dr Magufuli ambalo ni WAFANYAZI waliopo katika ajira za serekali na taasisi zake wasiokuwa na kazi za kufanya.Unamkuta mfanyakazi katoka nyumbani kaenda kazini kuanzia asubuhi hadi jioni hana kazi aliyofanya ?.Hili liko katika ofisi za wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,wakurugenzi wa miji na majiji.

Mfano Jiji la Arusha limeachukua kazi za kukusanya ushuru wa parking za magari,utashangaa watumishi wa Jiji kutoka idara mbali mbali (wasiokuwa na kazi) wamepelekwa katika viunga mbali mbali vya Jiji la Arusha kwaajili ya kukusanya ushuru huo.Jiulize kama walikuwa na kazi kweli wasingepelekwa kukusanya ushuru wa parking lakini kwakuwa hawana kazi ndio maana imekuwa rahisi Mkurugenzi wa Jiji kuwatupa mitaani na kufanya kazi ambazo zipo.Huu ni mfano mdogo tembelea maofisi mengi ya serekali utakuta watumishi kibao wasiokuwa na kazi kutwa nzima wanasogoa tu au wanafanyakazi ya kugonga mihuri barua ?.

Serekali ya Mheshimiwa Mtukufu Dr Magufuli yafaa baada ya kumalizika zoezi la kuhakiki wafanyakazi hewa wakaingia katika zoezi lingine la kuhakiki wafanyakazi wasikokuwa na kazi za kufanya wakawalipa stahili zao wakawabakiza wanastahili kubaki na kuwalipa vizuri.

Naomba kuwasilisha.
 
Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
6,726
2,000
Umeliona hilo ila kumbuka ata hao wafanyakazi wasio na kazi wana watoto na familia zinazowategemea unategemea fagio la mkuu wa nchi likiwapitia hali zao hao watu na familia zao zitakuwaje unazani...? ila mimi nadhani mkuu wa nchi ni bingwa wa kucheza na akili zetu maana alidai sukari maelfu ya matani ameyakamata mwisho wa siku ikazimika kama taa wananchi hatukupewa kama alivyodai...
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,367
2,000
Heshima sana wanajamvi,

Wakati serekali ya awamu ya tano ilipoanza rasmi kazi Rais Mheshimiwa,Mtukufu Dr John Pombe Magufuli alianzisha msako wa watumishi hewa na tulipewa mrejesho zaidi ya watumishi hewa 10,000 waligunduliwa katika mikoa yote Tanzania bara au ukipenda Tanganyika.

Naipongeza sana serekali kwa kubaini chanzo cha upotevu mkubwa wa fedha za serekali.Lakini pia nashindwa kuamini kama kweli idadi hiyo ilikuwepo na ikiwa ilikuwepo ni kwanini wale wote waliosababisha au kufaidika na wafanyakazi hewa hawajafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuisababishia serekali hasara kubwa kiasi hicho.

Nikiondoka katika eneo la wafanyakazi hewa ambao tunaambiwa hawakuwepo makazini (walisahakufa,walishastaafu,walishafukuzwa kazi na nk)Lipo tatizo lingine kubwa tena kubwa kubwa kuliko wafanyakazi hewa tulioambiwa na Mheshimiwa,Mtukufu Dr Magufuli ambalo ni WAFANYAZI waliopo katika ajira za serekali na taasisi zake wasiokuwa na kazi za kufanya.Unamkuta mfanyakazi katoka nyumbani kaenda kazini kuanzia asubuhi hadi jioni hana kazi aliyofanya ?.Hili liko katika ofisi za wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,wakurugenzi wa miji na majiji.

Mfano Jiji la Arusha limeachukua kazi za kukusanya ushuru wa parking za magari,utashangaa watumishi wa Jiji kutoka idara mbali mbali (wasiokuwa na kazi) wamepelekwa katika viunga mbali mbali vya Jiji la Arusha kwaajili ya kukusanya ushuru huo.Jiulize kama walikuwa na kazi kweli wasingepelekwa kukusanya ushuru wa parking lakini kwakuwa hawana kazi ndio maana imekuwa rahisi Mkurugenzi wa Jiji kuwatupa mitaani na kufanya kazi ambazo zipo.Huu ni mfano mdogo tembelea maofisi mengi ya serekali utakuta watumishi kibao wasiokuwa na kazi kutwa nzima wanasogoa tu au wanafanyakazi ya kugonga mihuri barua ?.

Serekali ya Mheshimiwa Mtukufu Dr Magufuli yafaa baada ya kumalizika zoezi la kuhakiki wafanyakazi hewa wakaingia katika zoezi lingine la kuhakiki wafanyakazi wasikokuwa na kazi za kufanya wakawalipa stahili zao wakawabakiza wanastahili kubaki na kuwalipa vizuri.

Naomba kuwasilisha.
Kujikomba tu,, Mtukufu ni Mungu tu! Wengine ni wana wa damu na Eva na nyama zao kama wewe!
 
Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
15,078
2,000
umeliona hilo ila kumbuka ata hao wafanyakazi wasio na kazi wana watoto na familia zinazowategemea unategemea fagio la mkuu wa nchi likiwapitia hali zao hao watu na familia zao zitakuwaje unazani...? ila mimi nadhani mkuu wa nchi ni bingwa wa kucheza na akili zetu maana alidai sukari maelfu ya matani ameyakamata mwisho wa siku ikazimika kama taa wananchi hatukupewa kama alivyodai...

Mkuu eddy_mhando habari za familia za wafanyakazi ni jambo lingine kabisa tena tunaweza kufungua uzi mwingine namna ya kuwawezesha baada ya ajira ya serekali kukoma.Kuendelea kubeba mzigo wa watumishi ni sawa na kukubali walipa kodi kulipa kodi jambo lisilo na tija.Fedha ambazo zinatumika kuwalipa watumishi wasiokuwa na kazi zingeweza kupelekwa maeneo mengine yenye tija zaidi eg ujenzi wa miundombinu,afya na elimu.
 
ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
12,056
2,000
umeliona hilo ila kumbuka ata hao wafanyakazi wasio na kazi wana watoto na familia zinazowategemea unategemea fagio la mkuu wa nchi likiwapitia hali zao hao watu na familia zao zitakuwaje unazani...? ila mimi nadhani mkuu wa nchi ni bingwa wa kucheza na akili zetu maana alidai sukari maelfu ya matani ameyakamata mwisho wa siku ikazimika kama taa wananchi hatukupewa kama alivyodai...
wakati huo huo viwanda vya sukari vimeamza kufanya kazi ama hii huna taarifa nayo!!!?
 
harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,890
2,000
Kweli hili suala hata mm nilikua nalitazama kwa mshangao kwamba IT wa jiji kumbe anaweza kuwa kituoni anakusanya fedha mwezi mzima bila shughuli kutetereka.

Au Afisa elimu taaluma na takwimu pia Mwezi mzima barabarani.

Ila pia nasikia kuna uwezekano wa kupunguza idara hizo ili wabaki wachache wenye shughuli zenye tija kwa taifa wengine wapewe shughuli nyingine mbadala
 
Patience123

JF-Expert Member
Mar 10, 2013
5,040
2,000
Naunga mkono hoja.

Ipitishwe redundancy ya hatari, wabaki wachache wenye tija.
Baada ya hapo hilo ombwe la wasio na kazi litakwenda wapi? Watamudu vipi mahitajia yao na family zao? Au ndio mnataka kuzalisha majambazi na vibaka mwisho was Siku mrudi hapa kuilaumu serikali kwa ukosefu wa ajira?
 
Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
6,726
2,000
Nimekuelewa mzee mwenzangu ila sasa tuilaumu hiyo hiyo serikali maana mwanzo si ndio iliwaajiri...
 
Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,623
2,000
Kweli hili suala hata mm nilikua nalitazama kwa mshangao kwamba IT wa jiji kumbe anaweza kuwa kituoni anakusanya fedha mwezi mzima bila shughuli kutetereka.

Au Afisa elimu taaluma na takwimu pia Mwezi mzima barabarani.

Ila pia nasikia kuna uwezekano wa kupunguza idara hizo ili wabaki wachache wenye shughuli zenye tija kwa taifa wengine wapewe shughuli nyingine mbadala
Kuhusu hilo la kupunguza idara na kubaki na chache sidhani kama mwelekeo wake ni kupunguza wafanyakazi. Kitakachofanyika ni kuunganisha idara mbili tatu na kuwa na idara moja lakini idadi ya watumishi inabaki ile ile.
 
bagain

JF-Expert Member
Jul 21, 2011
345
250
Hapo awali waajiriwa wa serikali walikuwa wanafanya kazi za utaalamu moja kwa moja. Lakini inaonekana mabadiliko ya mambo ya manunuzi au mabadiliko mengine yamefanya kazi nyingi zinafanywa na wakandarasi (contractors) kupitia tenders.

Hivyo kuwafanya wataalamu walioajiriwa na serikali kwa sehemu kubwa kuwa wasimamizi tu. Na kama tujuavyo kazi ya usimamizi haihitaji watu wengi.
 
All TRUTH

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
4,842
2,000
Kweli hili suala hata mm nilikua nalitazama kwa mshangao kwamba IT wa jiji kumbe anaweza kuwa kituoni anakusanya fedha mwezi mzima bila shughuli kutetereka.

Au Afisa elimu taaluma na takwimu pia Mwezi mzima barabarani.

Ila pia nasikia kuna uwezekano wa kupunguza idara hizo ili wabaki wachache wenye shughuli zenye tija kwa taifa wengine wapewe shughuli nyingine mbadala
Sio kupunguza ni kuziunganisha
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,101
2,000
Heshima sana wanajamvi,

Wakati serekali ya awamu ya tano ilipoanza rasmi kazi Rais Mheshimiwa,Mtukufu Dr John Pombe Magufuli alianzisha msako wa watumishi hewa na tulipewa mrejesho zaidi ya watumishi hewa 10,000 waligunduliwa katika mikoa yote Tanzania bara au ukipenda Tanganyika.

Naipongeza sana serekali kwa kubaini chanzo cha upotevu mkubwa wa fedha za serekali.Lakini pia nashindwa kuamini kama kweli idadi hiyo ilikuwepo na ikiwa ilikuwepo ni kwanini wale wote waliosababisha au kufaidika na wafanyakazi hewa hawajafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuisababishia serekali hasara kubwa kiasi hicho.

Nikiondoka katika eneo la wafanyakazi hewa ambao tunaambiwa hawakuwepo makazini (walisahakufa,walishastaafu,walishafukuzwa kazi na nk)Lipo tatizo lingine kubwa tena kubwa kubwa kuliko wafanyakazi hewa tulioambiwa na Mheshimiwa,Mtukufu Dr Magufuli ambalo ni WAFANYAZI waliopo katika ajira za serekali na taasisi zake wasiokuwa na kazi za kufanya.Unamkuta mfanyakazi katoka nyumbani kaenda kazini kuanzia asubuhi hadi jioni hana kazi aliyofanya ?.Hili liko katika ofisi za wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,wakurugenzi wa miji na majiji.

Mfano Jiji la Arusha limeachukua kazi za kukusanya ushuru wa parking za magari,utashangaa watumishi wa Jiji kutoka idara mbali mbali (wasiokuwa na kazi) wamepelekwa katika viunga mbali mbali vya Jiji la Arusha kwaajili ya kukusanya ushuru huo.Jiulize kama walikuwa na kazi kweli wasingepelekwa kukusanya ushuru wa parking lakini kwakuwa hawana kazi ndio maana imekuwa rahisi Mkurugenzi wa Jiji kuwatupa mitaani na kufanya kazi ambazo zipo.Huu ni mfano mdogo tembelea maofisi mengi ya serekali utakuta watumishi kibao wasiokuwa na kazi kutwa nzima wanasogoa tu au wanafanyakazi ya kugonga mihuri barua ?.

Serekali ya Mheshimiwa Mtukufu Dr Magufuli yafaa baada ya kumalizika zoezi la kuhakiki wafanyakazi hewa wakaingia katika zoezi lingine la kuhakiki wafanyakazi wasikokuwa na kazi za kufanya wakawalipa stahili zao wakawabakiza wanastahili kubaki na kuwalipa vizuri.

Naomba kuwasilisha.
Mkuu, nimesikia zoezi la kujua kila mtumishi wa umma anafanya nini toka asubuhi hadi anatoka kazini linaendelea.
Ukweli mchungu sana ni kwamba kuna idadi kubwa ya watumishi wa umma hawana kazi za kutosha. Maana yake kuna uwezekano wa kupunguza wafanyakazi.
Inaweza kuonekana kama contradiction wakati inazungumzwa kutengeneza nafasi za ajira. Kuwa na wafanyakazi wasio na kazi za kutosha haiwezi kuwa ufumbuzi wa kutengeneza nafasi za ajira. Wingi wa wafanyakazi wasio na kazi au kazi za kutosha ni sawa kuwa na wafanyakazi hewa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom