BASHADA
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 513
- 148
Wiki iliyopita nilikuwa nasafiri kwa gari langu binafsi nikiwa na rafiki yangu. Njiani tukachukua abiria (Kama mjuavyo ni jambo la kawaida sana, kama namna ya kuchangia mafuta na wenye magari wengi hufanya hivyo). Tulipata abiria, ikabaki nafasi ya mtu mmoja tuu. tulipofika mji uliofuata tukaingia sheli kujaza mafuta. Wakaja vijana wapiga debe wana abiria, tukabargain bei tukaelewana. Wakamleta huyo abiria, ni kijana mmoja wa kimasai. Nilichoshukuru hakuwa mchafu chafu kwa hiyo hakuwa kero kwenye gari, la sivyo ningerudisha hela kabisa.
KITUKO:
Tukiwa tunaendelea na safari, nilikuwa naongea na huyu rafiki yangu tuliyeanza naye safari, tukipeana uzoefu wa kuendesha gari long safari. Nikawa namsimulia safari yangu ya hivi majuzi ambapo tulisafirisha msiba ambapo njiani mke wa marehemu alikuwa anazimia mara kwa mara, maana kifo kilikuwa cha ajali, kwa hiyo mfiwa alikuwa na mshtuko mkubwa. Sasa Mmasai akadakia story yetu, akasema, "sasa kama mume amekufa si mnazika, huyo mama yoyo analia na anasimia nini, au na yeye afe akamfuate mume yake....". Kusema ukweli tulishtuka, wote tukamgeukia. Tukamwuliza wewe mke wako akifa hulii? Akasema sasa nilie nini, mutu kama imekufa nazika. Tukamwuliza, wewe huogopi kufa? Akasema sipendi kufa lakini mtu akifa dawa ni moja tuu, kuzika tuu.
Sasa nimewaza sana kuhusu hawa ndugu zetu wamasai, hivi hawana roho ya huruma na ubinadamu? Au siyo binadamu by nature?