Kuna mliofanya harusi za gharama kubwa na sasa mnajutia?

hiden

JF-Expert Member
Sep 28, 2015
376
691
Wakuu,

Nataka kufanya harusi, kinachonisikitisha ni kwamba nikipitisha mchango sitakosa 25M.

Lakini naumia kuteketeza 25M kwa siku moja.

Pia naona kero kuchanga pesa za watu, nafikiria hata nisifunge ndoa.

Naomba ushauri kwa waliofanya harusi za gharama.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unauchungu na hela zinazogharamia tukio hilo ni bora usichukue kabisa hata michango ya watu maana siku utalazmika kuilipa watoto wao wakioa au kuolewa. Na kupanga kuzitumia tofauti na malengo ya walikuchangia itakucost Mambo mengi utajuta kufanya hivyo Tena hapa duniani.
 
Umeweza vyema harusi si tukio la muhimu sana ila ndoa ndiyo tukio la muhimu sana. Unaweza ukafunga ndoa halali na ukapata baraka zote kutoka kwa Mungu, pia unaweza ukafanya harusi kubwa sana na usipate baraka zozote toka kwa Mungu.
Nachotaka kusema hapa ni kuwa ndoa ni mpango wa Mungu na harusi ni mpango wa wanadamu.


Ndoa haina gharama yeyote kufunga ila ukitaka harusi ina gharama, fanya jambo jema funga ndoa na fanya harusi iliyo ndani ya uwezo wako pasi kuwachangisha watu. Hii itakupa heshima kwa jamii inayokuzunguka ila pia utakuwa umeonyesha maana halisi ya uanaume.
 
Wakuu,

Nataka kufanya harusi, kinachonisikitisha ni kwamba nikipitisha mchango sitakosa 25M.

Lakini naumia kuteketeza 25M kwa siku moja.

Pia naona kero kuchanga pesa za watu, nafikiria hata nisifunge ndoa.

Naomba ushauri kwa waliofanya harusi za gharama.
Sent using Jamii Forums mobile app
....unaogopa kuteketeza, kwani hela zako? Mie harusi yangu iligharimu milioni 28 sijaijutia mpk leo na maisha yanaenda tu poa mpaka leo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom