Kuna Mkoa haujapata mafanikio ya Magufuli?

Waimba mapambio ya kusifu na kuabudu mtangaika sana , tuliwaambia huyu 2025 hafiki na maaircondition kila anapoenda , mkakazania mitano tena , niliwaambia Mia tena .
 
jingalao
Arusha kuna mradi gani mkubwa unaoweza kufananishwa na Chato?
Angalizo mradi wa maji na barabara ya Sakini iliasisiwa na Kikwete.
Ama kwa Zahanati kaangalie ule upuuzi uliojengwa Kijenge fananisha na hospital ya Kijiji Cha Chatto
 
jingalao
Arusha kuna mradi gani mkubwa unaoweza kufananishwa na Chato?
Angalizo mradi wa maji na barabara ya Sakini iliasisiwa na Kikwete.
Ama kwa Zahanati kaangalie ule upuuzi uliojengwa Kijenge fananisha na hospital ya Kijiji Cha Chatto
Arusha haikuwa na Hospitali ya wilaya...leo ipo pale njiro
Arusha ilikuwa na hospitali mbovumbovu ya mkoa pita leo Mount Meru.
Ukienda Loliondo kuna barabara inajengwa itakayofupisha safari kutoka loliondo hadi Arusha mjini
Ukuta wa mererani na soko la madini ya Tanzanite
Barabara ya Ngaramtoni hadi mianzini
Murieti kuna kituo kikubwa cha afya
Makuyuni kuna kituo cha afya
Shule ya Ilboru imekarabatiwa
Longido imepata mradi wa maji
longido imejengewa hospitali
Karatu imejengewa hospitali na vituo vya afya
Arusha -Moshi road ...
Arusha by pass road
Soko la Samunge
vyumba vya madarasa
Hospitali kubwa ya kijeshi monduli
Reli kutoka Tanga imefufuka
Mahakama ya hakimu mkazi inaboreshwa
Ikulu ya Arusha ilikarabatiwa na kuanza kutumika
Jengo la posta ya Africa linaelekea kukamilika
barabara za kati ya mji zina lami
mfumo wa majitaka unaboreshwa
Hayo ni machache
 
Hili ni swali kwa wawakilishi wa wananchi na wananchi ili tuende sawa.

1. Kuna mkoa haujajengewa hospitali au kituo cha afya?

2. Kuna mkoa hauna mradi wa maji?

3. Kuna mkoa hauna mradi wa barabara?

4. Kuna mkoa hauna mradi wa umeme vijijini?

5. Kuna mkoa haujapata mradi wa ujenzi wa shule?

6. Kuna mkoa una machinga asiyetambuliwa?

7. Kuna mkoa haujengi viwanda?

8. Kuna mkoa haujapata pembejeo za kilimo?

9. Kuna mkoa haujapata fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa?

10. Kuna mkoa hauna huduma bora za fedha?

Hayo ni maswali yangu machache kati ya mengi yenye kuhoji utekelezwaji wa Ilani ya CCM.

Tukumbuke kuwa wakati miradi kadhaa ikitekelezwa basi kuna miradi mikubwa na ya kimkakati inayoshika kasi tena kwa fedha za ndani.

1. Mradi wa SGR
2. Mradi wa kufua umeme
3. Manunuzi ya ndege
4. Mradi wa Maji
5. Ujenzi wa flyovers n.k

Rais Magufuli songa mbele wanafiki wanaombea uumwe!!
kushiney babuji
 
Back
Top Bottom