Kuna mkakati wowote wakurudisha twiga waliotoroshwa?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,887
wanajf kama kuna mtu ana habari za kinachoendelea kuhusu urejeshwaji wa wanyama waliotoroshwa maana isije kuwa makelele ya bungeni ndio mwisho! kama walitoroshwa kimagendo najua hata sheria za kimataifa zitakuwa upande wetu
 
Subutu! Walishakwenda na maji na wajanja wameshaweka vyao mifukoni.
sio wajanja mkuu sema wezi! kagasheki yuko wapi? anafukuza walinzi wa mbuga anaacha kufuatilia ishu kubwa(au sina habari kuna kitu kinaendelea) watu wa haki za wanyama hii ishu haiwezi kuwahusu? bunge liko wapi? domo tu! wabunge wa CHADEMA nahisi hili liko ndani ya uwezo wenu komaeni hadi ile ndege irudishe wanyama wetu.
 
nyinyiemu huwa wana msemo wao wa kiendacho kwa mganga hakirudi,na msemo mwingine wa kufanana na huo unaosema kuwa chatu akimeza huwa hatapiki..........kwa hiyo ndugu yangu hebu jiongeze na wewe
 
Kama hawarudishwi mbona wahusika yaani waliowauza hao wanyama mbona wanapeta tu mtaani na magari yao ya kifahari na chama tawala nacho kimefunga macho tu au ni ule msemo kuwa UKINIGUSA NAKUGUSA NA WEWE manake walioko ndani ya chama tawala asilimia kubwa ni majangili/mafsadi
 
Wewe ukowapi Tanzania hii inayoongozwa na wasanii boys 2men au? Hapa bwana ukiiba bila kukamatwa imetoka kama mzee wa kiwira. akijua sheria Hazifanyi kazi akasimama na kusema bila aibu ofisi ya ubalozi Yeye ndio anahusika mzee wa intelejensia naye akazidi pindisha sheria kutetea wazee wa Epa kuwa warudishe pesa kwanza sheria baadae mmh hapa inabidi tuuiombee CDM ije na sera mpya uwajibikaji ndio twiga warudi kama wako hair bado teh teh teh. J
wanajf kama kuna mtu ana habari za kinachoendelea kuhusu urejeshwaji wa wanyama waliotoroshwa maana isije kuwa makelele ya bungeni ndio mwisho! kama walitoroshwa kimagendo najua hata sheria za kimataifa zitakuwa upande wetu
 
Nani kakwambia twiga anaweza kutoroshwa?
Huwezi kumtorosha twiga kwa ukubwa wake ule, tena kwa kutumia ndege ya jeshi ya nchi nyingine.
 
inabidi wakati wa bajeti ya maliasili na utalii wabunge wapatikise ikiwezekana isipite bila twiga kurudi. bila shaka hao jamaa walianza long sana hizi deal ila juzi kati ndio yamewakuta. yaani inasikitisha kweli.
 
Nani kakwambia twiga anaweza kutoroshwa?
Huwezi kumtorosha twiga kwa ukubwa wake ule, tena kwa kutumia ndege ya jeshi ya nchi nyingine.
Sikuelewi, inawezekana kusafirisha mnyama yeyote kwa ndege hata tembo. Kuna sindano maalum zinapigwa kama risasi analala kisha anasafirishwa. kama ulifuatilia wale faru wa mkomazi walirudishwaje kutoka Afrika kusini? si waliletwa na ndege ya jeshi la Afrika kusini.
 
hivi mkuu waziri kivuli wa wizara ya maliasili na utalii ni nani?
huyu ni mchungaji msigwa wa jimbo la iringa mjini CHADEMA na katika moja ya hoja za zitto katika mkutano wa iringa leo hili la twiga kalizungumzia kuwa lazima twiga warudi..tatizo wako wachache sana na mambo ya ku deal nayo ni mengi mno..tuwape muda tuu
 
Hio ndo imetoka Hii ndo Tanzania ya ccm
yaani ni nchi ya walalamishi wabunge wanalalamika tu bila kutoa way forward nini kifanyike, mwizi unamuona anavinjari na mali yako uwezo wa kuichukua unao badala ya kuchukua unalalamika. hivi ni moja ya vitu vinavyochangia kushusha umri wa kuishi.
 
Sioni sababu ya msingi ya kutumia mamilioni ya walipa kodi kwa ajili ya kurudisha twiga 4 ambao tayari wamesha athirika kisaikolojia na kuacha twiga wengi wakizidi kuuawa. hizo fedha bora zitumike kzwalinda waliopo
 
huyu ni mchungaji msigwa wa jimbo la iringa mjini CHADEMA na katika moja ya hoja za zitto katika mkutano wa iringa leo hili la twiga kalizungumzia kuwa lazima twiga warudi..tatizo wako wachache sana na mambo ya ku deal nayo ni mengi mno..tuwape muda tuu
thanks kwa info, hivi maige si huwa analialia kaonewa na kujidai mzalendo sasa atusaidie kurudisha twiga wetu vinginevyo 2015 tutamnyonga na mafisadi wengine pale jangwani.
 
thanks kwa info, hivi maige si huwa analialia kaonewa na kujidai mzalendo sasa atusaidie kurudisha twiga wetu vinginevyo 2015 tutamnyonga na mafisadi wengine pale jangwani.
hii ilikua ni kutapatapa tu baada ya kunyang'anywa kitumbua..hawezi kufanya lolote kwani wizi wa kule ni mwingi mno toka enzi za magji na usafirishaji wa magogo nje ya nchi..MUKULU mwenyewe kaanza ujenzi wa hoteli moja matata sana kule mbugani na ni wakati wa huyu maige ..sasa unategemea lolote hapo??
 
kwenye mwanainchi ya leo kuna watu watatu wamefungwa miaka 20 kila mmoja kwa kosa la kuua pundamilia mbugani. TZ ni vidagaa tu ndio wanaoonewa!
 
Sioni sababu ya msingi ya kutumia mamilioni ya walipa kodi kwa ajili ya kurudisha twiga 4 ambao tayari wamesha athirika kisaikolojia na kuacha twiga wengi wakizidi kuuawa. hizo fedha bora zitumike kzwalinda waliopo
sheria ikifuatwa aliye iba ndio atahusika na gharama halaf kulikuwa na wanyama wengine pia
 
Back
Top Bottom