Kuna mji wenye usafiri mzuri wa daladala na elimu nzuri kuliko Mbeya?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,029
Hakika sijaona mji wenye system nzuri ya daladala kama Mbeya. Stendi kubwa zipo tatu kuna ya mjini ambayo ni stendi kuu ya zamani na ni kubwa kiasi kwajili ya mabasi ya mikoani na daladala, kuna stendi kabwe hii ni kwajili ya daladala na bajaji na pia utaikuta stendi kuu ya nane nane.

Nimejaribi kufananisha na miji mingine bado sijaona, kwa mfano pale Arusha hakuna hata stendi moja inayoeleweka kwajili ya daladala yaani hata stand ya mabasi ya mkoani pale town bado sana.

Elimu -

Shule za msingi - zipo shule tatu za serikali za mtaala wa Kiingereza ada laki 3, ipo Shule ya Azimio, Mkapa na Magufuli. Shule za private nazo zipo kuna Umoja, Riverside, Saint Mary, Uwata, n.k. shule za serikali pia zipo kibao kama utitiri, Sisimba ndio kinara na kongwe

sekondari - zipo za umoja wa wazazi kuanzia Sangu, Meta, Ivumwe, Mbalizi, n.k huku niseme tu ya kwamba ufaulu upo ila na njiti zinatembezwa hasa, ukija shule za serikali nazo zipo Samora, Mbeya day, forest, n.k ukija private nazo zipo st marys, uwata, pandahill, Swilla, n.k. shule za kata ni nyingi sana.

Vyuo - M.U.S.T, Udsm - mchas, Udsm - ucc, Mzumbe, Tia, Open, utumishi, cbe, Saut, Adem, Tumaini, Teku, n.k ukija vyuo vya uuguzi na ufundi napo vimejaa si mchezo kuna Mbalizi, k's, moravian, veta, n.k ni vingi sana.

Kwa hali hii wacha niwape pongezi Mbeya
 
Songea wanazidi hukoo usemako
Pic%20Layer_2021111311215721.jpg
 
Mbeya ni jiji linalojiweza kwa mengi bila boost kubwa kutoka serikali kuu.

Mbeya wanapiga sana kazi kule na wana nidhamu sana hasa wanawake wao.

Nitaoa mke wa pili toka Mbeya Inshallah.
 
Back
Top Bottom