Kuna mikoa ina utamaduni na mwamko wa kuchangia elimu. Serikali haina haki kuwakatisha tamaa

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,402
54,878
Watanzania tuna msemo wetu: "KUTOA NI MOYO..."

Sasa ipo mikoa ambayo wenyeji wake wana UTAMADUNI wa kuchangia Elimu.

Utamaduni huo ulikuwepo tangu Elimu ilipoingia na kabla hatujapewa jina la Tanganyika na baadae Tanzania.

Suala la kuchangia elimu ktk maeneo hayo halitokani na uwezo wa kiuchumi, bali linatokana na MUAMKO wa kupenda ELIMU BORA kwa vijana wao.

Ushauri wangu ni serekali isikwamishe wananchi wa maeneo hayo kuchangia elimu, au huduma yoyote nyingine ya kijamii.
 
Na hicho ndicho wengi tunasema...

Tusiwafanye wananchi ni wapumbavu. Haiwezekani mtu anayeishi au kufanya kazi sehemu za Magogoni akawa anazifahamu vyema shule za Namtumbo kuliko Wanamtumbo wenyewe~~

Hawa wananchi wana akili ya kufahamu ni wapi panahitaji nguvu zao! Anapotokea mtu mwingine na kutoa marufuku as zimechangwa pesa za kuwapa walimu wakalewee pombe, inatia ukakasi si kidogo na matokeo yake wananchi wanafikia kuamini kwamba kumbe serikali imemaliza kero zote za shule wakati si kweli!!!

Kuna mkoa mmoja miaka nenda rudi huwa unafanya vibata sana kielimu.

Sasa kuna msimu fulani, ule mkoa ukawa hukosekani kwenye 10 Bora ya mikoa iliyofanya vizuri elimu ya msingi kwa takribani miaka 3 mfululizo!

Nikashangaa!!

Nikaenda kufanya utafiti kujua kulikoni! Kumbe wazazi kwenye moja ya majimbo walianzisha kitu ambacho walikuwa wanaita Kambi za Kusoma. So, walikuwa wanachangishana pesa kwa ajili ya kuziendeleza hizi kambi!

Ilikuwa ukifika ama darasa la 7 au la 6, watoto wakawa wanakuwa kwenye hizi kambi za kusoma/kujisomea badala ya kuwaacha nyumbani wakizurula!!

Matunda ya hizi kambi yalianza kuonekana baada ya muda mfupi sana!
 
chige,

..mimi naamini wazazi wanaochangia shule, wanakuwa pia wafuatiliaji wazuri wa maendeleo ya watoto wao, na utendaji wa waalimu, na hiyo hupelekea watoto kufanya vizuri ktk masomo.

..kwa hiyo michango kwa maoni yangu ingekuwa kama ni chachu ya wazazi kuwa involved kuhusu elimu ya watoto wao, na waalimu kuwajibika na kujituma zaidi.

..ilitakiwa serekali iwaelimishe wazazi kuhusu umuhimu wa kuchangia elimu, na siyo kufuta michango as if serekali ina uwezo wa kugharamia kila kitu.

..hata katika nchi zilizoendelea zinazotoa elimu bure wazazi wanachangia mambo mbalimbali, na kuna kamati za wazazi ktk kila shule.
 
Tena hapa umeongea jambo la msingi sana! Ni kweli, inasaidia sana kwa wazazi kuwa involved kwenye hizi gharama... Katika hali ya kawaida, lazima watataka waone matunda yake na katika kufikia hilo, watakuwa concerned na mienendo ya watoto vile vile katika suala zima la kusoma.
 
Back
Top Bottom