Kuna mengi yaliyojificha nyuma ya uchomaji makanisa Unguja

Heshima mbele Mkuu MMKJJ:

Kielimu tu na kimaendeleo ni vigumu kuwalinganisha watu wa Scotland na Quebec na hawa Wazanzibari. Huko majuu wanafanya mambo yao kistaarabu zaidi, au tunaaminishwa wanbafanya hivyo.

Kutumia udini ktk malengo ya siasa yamefanyika mahala mengi kama historia inavyotuambia. Miaka ya karibuni ni Iran, pale udini ulitumika kumuondoa Shah mwaka 1979. Hii ni kwa sababu Iran ni Waisilamu kwa asilimia 95%.

Halafu tusisahau Ireland ya Kaskazini. Kuna udini unatumika kudai haki au kuiminya haki ya kujitenga kwa jimbo lile la uingereza (UK). Waprotestanti ambao ndiyo wengi kule wanatumia udini kutaka kubakia chini ya utawala wa London, na Wakatoliki wanataka kujiunga na Jamhuri ya Ireland (Ireland ya Kusini) ambayo ina Wakatoliki wengi.

Hali kadhalika huko Palestina ambako udini unatunmika sana kwa malengo ya kisiasa na Kashmiri, jimbo (state) pekee la India ambalo lina Waisilamu wengi (majority). Udini unatumika ktk harakati za kujitenga.

Huko Zanzibar Waisilamu ni kama 95 % hivyo kuitumia dini ktk malengo ya kisiasa yapo na yanaeleweka hasa katrika nchi zenye dini moja au dini moja kubwa. Ila swali la kujiuliza ni kwamba jee ni haki au dhambi kufanya hivyo?

Mmh! Kuna masuala ya msingi hapa aliyoleta NSM, na hasa katika ile dhana ya kwamba ni vigumu kutenganisha dini na siasa. Hata huko nchi za magharibi, udini unatumika sana katika harakati za siasa na kudai haki ingawa mara nyingi si kwa njia za ghasia. Ghasia hutokea pale tu ambapo ukandamizaji hupitiliza kipimo.

Mfano alioutoa NSM wa Ireland na Iran ni mizuri, lakini kuhusu Ireland, mauaji mengi sana yalifanyika dhidi ya kikundi cha IRA pale majeshi ya Uingereza yalipokwenda kuzima "uasi" kuanzia miaka ya 70.
 
JAMANI HAYA MAMBO YAKO WAZI HAWA VIJANA WAMEANDAMANA SIKU TATU ,NA KANISA WAMECHOMA SIO MARA MOJA,
  • SIKU YA KUKAMATWA KWA KIONGOZI WAO WAKIWA KWENYE MAANDAMANO KWENDA KWEREKWE WAKACHOMA KARIAKOO AU KUNA UTATA?
  • SIKU YA PILI WAMEWASHA MATAIRI BARABARANI HAO UAMSHO WANAFUKUZWA NA MABOMU WANARUDI ILI KIONGOZI WAO ATOE AU HILO LA KUCHOMA MATAIRI ROAD LINA UTATA?
  • WAKICHOMA MATAIRI MITAA YA KISONGE NAKWEREKWE MCHANA KWEUPE WAKAENDA KUCHOMA KANISA LA MPENDAE TENA WAKIWA WANATOKEA KWEREKWE AU KUNA UTATA?
  • WAKIWA KISONGE WAMEWASHA MATAIRI MAGARI HAYAPITI WANASHINIKIZA KIONGOZI WAO AACHIWE WAKACHOMA MAGARI YA WATU AU KUNA UTATA?
  • MAANDAMANO YAO WALIYOKUWA WANAFANYA KUTOKEA MSIKITINI NA KUSABABISHWA BARABARA KUFUNGWA NALO LINA UTATA KUWA PENGINE WALIOKUWA WANAFUKUZWA NA MABOMU AMBAO HATA KWENYE TV NA MAGAZETI WAMEONEKANA NAO SIO UAMSHO?
  • MIKUTANO YAO WANAYOENDELEA MSIKITINI NA WANAYOENDELEA KUITANGAZA HUKU VIONGOZI WAO WAKISEMA WATAENDELEA NA MIKUTANO NAYO WAMESINGIZIWA?

hapo kuna nini kisicho wazi ndani ya siku tatu maandamano na kuchoma makanisa kila siku yote hiyo wamesingiziwa?

kama sio kikundi cha fujo hiyo kuchoma matairi na vurugu barabarani serikali imedanganya?naombeni majibu

Kama bara ungesikia wangapi wameuawa, kadhaa mahabusu, Isinge wezekana kuandamana kwa siku 3,
kutokana na kutulia kwa jeshi la polisi kwa siku hizo 3 tunahisi angenda hiyo ilipata baraka za viongozi wa Zanzibar
 
Heshima mbele Mkuu MMKJJ:

Kielimu tu na kimaendeleo ni vigumu kuwalinganisha watu wa Scotland na Quebec na hawa Wazanzibari. Huko majuu wanafanya mambo yao kistaarabu zaidi, au tunaaminishwa wanbafanya hivyo.

Kutumia udini ktk malengo ya siasa yamefanyika mahala mengi kama historia inavyotuambia. Miaka ya karibuni ni Iran, pale udini ulitumika kumuondoa Shah mwaka 1979. Hii ni kwa sababu Iran ni Waisilamu kwa asilimia 95%.

Halafu tusisahau Ireland ya Kaskazini. Kuna udini unatumika kudai haki au kuiminya haki ya kujitenga kwa jimbo lile la uingereza (UK). Waprotestanti ambao ndiyo wengi kule wanatumia udini kutaka kubakia chini ya utawala wa London, na Wakatoliki wanataka kujiunga na Jamhuri ya Ireland (Ireland ya Kusini) ambayo ina Wakatoliki wengi.

Hali kadhalika huko Palestina ambako udini unatunmika sana kwa malengo ya kisiasa na Kashmiri, jimbo (state) pekee la India ambalo lina Waisilamu wengi (majority). Udini unatumika ktk harakati za kujitenga.

Huko Zanzibar Waisilamu ni kama 95 % hivyo kuitumia dini ktk malengo ya kisiasa yapo na yanaeleweka hasa katrika nchi zenye dini moja au dini moja kubwa. Ila swali la kujiuliza ni kwamba jee ni haki au dhambi kufanya hivyo?

Nakubaliana nawe kabisa. Waliokuwa wakifuatilia mgogoro wa ireland ya Kaskazini kulikuwapo ripoti kuhusu shirika la ujasusi la uingereza (MI5) kupandikiza mabomu kule Belfast na Londonserry katika miaka ya 70 ili kuonyesha kuwa ni IRA ndiyo walifanya hivyo.

Hapa kwetu haya pia yanawezekana saana, msibishe jamani!
 
Acha kutetea upumbav,
Hizo stori kaongee na wajukuu zako. Hazina hata chembe ya ukweli ndani yake.
Ni nani asiyefahamu kuwa uongozi wa SMZ mzima na waz'bar kwa ujumla wanapinga muungano?
Na hicho kitu si jana wala juzi, hata mtoto mdogo anajua!
Unataka kutuaminisha nini kwa maneno yako hayo?Au nawe ni miongoni mwa hao Uamsho? Ushindwe ulegee, wajanja tumekumaizi, KAJIPANGE.
 
kuna harufu ya kutetea udhalimu hapa - thread hii mtu mahili anaweza itunga - haina ushahidi wa moja kwa moja. uzamili unahitajika katika hili
 
Hapa mnataka kuwachezea watu akili. Kama hoja ni Muungano kwanini hao wanaopinga Muungano wasijikite kwenye kuukataa Muungano pasi ya kuzungumzia chuki dhidi ya Watanganyika na Tanganyika? Kwa mfano Scotland na Britain zina matatizo ya muungano wao kwa muda mrefu sana lakini wanahusiana vizuri na watu wa Scotland watakapoanzisha taifa lao si kwa sababu wana chuki na Waingereza. Hili ni kweli pia kati ya Quebec na Canada. Hawa nao wamekuwa na mjadala mkubwa sana wa muungano wao na Quebec wanataka kujitenga kwa muda mrefu sana.

Wanaopinga Muungano Zanzibar wanachanganya mambo mengi sana kiasi kwamba kuchomwa majengo, kutishiwa watu wa bara na hata baadaye vurugu zitakazotokea haziwezi kutenganishwa na hoja za hawa jamaa. Wanaopinga Muungano wangeweza kabisa - kama wanataka - kupinga muungano kwa kutumia hoja dhidi ya Muungano na utaifa wa Zanzibar. Hoja ya kupinga Muungano ingeweza kutolewa kwa misingi miwili:

a. Muungano haukuwashirikisha watu wa Zanzibar na hivyo hauna uhalali (msimamo wa baadhi ya wasomi wengi wa Zanzibar kama kina Prof. Sharrif na wengine.

b. Muungano ulivyo sasa hauna sababu ya kuendelea kwani Zanzibar hainufaiki na inaweza kujinufaika yenyewe bila kuwa katika Muungano.

Hoja hizi mbili zinatosha kabisa kuwaunganisha Wazanzibari wote - na sisi wengine tutawaunga mkono.

Bahati mbaya hizi siyo hoja; hoja zao zimeongezwa "anti-Tanganyikans" and "anti-Christians". Sijui kama watu wamewasikliza hawa wanaozungumzia kupinga Muungano. Wanapinga kwa sababu ni wa Watanganyika. Sasa chuki wanayopandikiza dhidi ya watu wa bara inapoota mizizi wanashangaa inapochanua maua halafu wanaruka? Umwitie mtu "mwizi mwizi" halafu watu wakaja wakamtia kiberiti uruke na kusema ulikuwa unaimba tu wala hukumaanisha?


Nakuuliza tu MMKJJ: Hivi jee yule Kony anayesumbua Uganda na CAR kwa kutumia udini angekuwa ni Muisilamu?
 
Hivi kama Wazanzibari wengi hawapendi Muungano, wakidai umeundwa kinyemela na Mwalimu Nyerere akishinikiza Sheikh Abeid Karume; na sasa hata WaTz wa Bara wanafukuzwa Zanzibar, wengine wakitishiwa maisha yao na mali zao kuteketezwa kwa moto, kuna sababu gani kung'ang'ania Zanzibar isijiondoe katika Muungano?

Hivi kama Watanganyika hawakuombwa waridhie Muungano kwa kura ya maoni, na wengi wetu tunaona hii ndoa ni "nuisance", yaani bughudha, inayotufanya tusitekeleze mambo muhimu ya kuendeleza miradi itakayotumia maliasili lukuki ya nchi yetu, na kutuletea maisha bora; kwa nini tusikubali kuwa na referandum wakati huu wa kujadili Katiba ya Muungano? Tujiondoe ili tuweze ku-concetrate on development of Tanganyika.

Kwa kifupi, Wazanzibari hawatutaki; na Watanganyika tunaona Muungano hauna tija.

Tuachane!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 



Hii issue ya maandamano ya Uamsho, vurugu zilizotokea na uchomaji wa makanisa ina mengi yaliyojificha kuliko tulivyoona na kuamini (au kuaminishwa).M

Kuna wanaoona kuna mikakati ilibuniwa rasmi na kupangwa kimakusudi kwa lengo la kupindisha ajenda ya awali waliokuwa nayo Uamsho ya kuuhoji Muungano au hata kutaka uvunjwe.

Haijulikani mikakati hii ilifanywa na akina nani lakini kulikuwapo thread moja humu JF siku chache zilizopita ambayo iliondolewa iliyosema kuwa kule Visiwani wengi walikuwa wanaamini kuwa Usalama wa Taifa (UWT) ndiye walipanga mikakati hiyo kwa madhumuni hayo hayo ya kupotezesha lengo halisi la mikakati ya Uamsho.

Mikakati hii ya UWT kama kweli wao ndiyo walitekeleza itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani dhoruba kali tayari imewaangukia Uamsho kwani hatimaye wamejikuta wanabebeshwa lawama la uchomaji wa makanisa, kitu ambacho wengi katika taasisi hiyo wanaamini kuwa siyo wao waliotenda kitendo hicho, ingawa katika mazingira yalivyokuwa itakuwa vigumu kutohusishwa nayo.

Tutegemee vyombo vya dola iwapo kweli watawakamata watu wale hasa waliochoma makanisa hayo, na siyo kamata-kamata tu ya holela. Kuna usemi unaosema kwamba Uchomaji wa majengo (yaani arson) ni rahisi sana kutenda lakini ni vigumu sana kuwabaini mhusika/wahusika halisi. (It is easy to commit arson than to detect those responsible).

Kuna watu wameicheza hii kama Messi. Ni dhoruba ambayo kwa waliokusudia wanaona wamefanikiwa kuizima kabisa mikakati yote ya ajenda ya kuuhoji na/au kuuvunja Muungano kwani hakuna tena huko Unguja atakayeweza kuja na kitu hii – kwani wataambiwa ‘Nyie hamna lolote – ajenda yenu kumbe ni udini tu, na siyo Muungano!”

Ni hakika watu wa uamsho wamejinasa. Dola imepata sababu kubwa ya kupiga marufuku tena maandamano/harakati zozote kuhusu kuhojiwa Muungano kule Unguja.

Hii inatokana na ukweli kwamba suala zima la Muungano katika mchakato wa kuandika Katiba mpya limawakalia vibaya sana watawala kwani wameshasema kwamba Muungano usiguswe. Na ugumu mkubwa ulikuwa unatoka Visiwani lakini sasa inaonekana wamefanikiwa kulizima – pengine labda kwa muda tu.

Sasa hivi Tume ya Katiba inaweza kuingia Visiwani na kufanya kazi bila hofu, pamoja na kwamba kutumika kwake Zanzibar bado ni kitendawili kutokana na sheria iliyoiunda ktk Bunge la Muungano kutothibitishwa na Baraza la Wawakilishi.





Mkuu una matatzo ya kufikiri.
Mbaya zaidi ni kufikiri sisi Watanganyika hatuwaelewi Wazanzibari na mlengo wao kimawazo.
Kupinga Muungano na kuchoma makanisa haikuanza na hawa watu wa Uamsho.

Masuala ya upinzani kwa Muungano yanajirudia katika mbinu tofauti na ninahisi kuna mkono wa watu vogogo wa kisiasa nyuma yake.
Makanisa yameanza kuchomwa toka 2001 na HAKUNA aliyekamatwa au kufikishwa mahakamani.
Na hii ndiyo dalili ya kuhusika kwa SMZ katika uponzani huu na uchomaji moto makanisa.
Kwa matukio tuliyo yaona wikiendi iliyopita na toka 2001,inakuwa vigumi kuamini kama kuna dhamira njema yoyote toka visiwani.
 
bado ni vigumu kuwatenganisha uamsho na uchomaji makanisa kwa sababu zifuatazo
1. Walishatamka maneno hadharani kuonyesha chuki yao dhidi ya makanisa. Rejea kauli zao kuwa 'kanisa lisiwaingilie mambo yao'
2. Sio mara ya kwanza kuchomwa makanisa zanzibar. Ingawa kuho vyuma waliochoma inawezekana hawakuwa uamsho (kwa sababu pengine haikuwepo), inamaanisha kuwa kuna watu/makundi ya watu yana chuki dhidi ya ukristo zanzibar. Ni rahisi sana wakajipenyeza ndani ya uamsho
3. Kulikuwa na chance kubwa na nzuri kwa mtu yeyote zanzibar kuanzisha vuguvugu la kudai 'uhuru' bila kuhusisha dini. Kitendo cha uamsho kutumia vikundi nya kidini, maimamu na mihadhara ya kidini kudai zanzibar yao hakiwatenganishi na udini kamwe
4. Uamsho wanafanya pia mihadhara ya kiislamu. Kila mtu anafahamu kuwa mihadhara ya kiislamu imejaa matusi na kebehi dhidi ya ukristo. Watu wengi wanazisikia cassettes za kutoka kwenye mihadhara zinavyotunaka ukristo. Hakuna jambo jingine zaidi ya chuki za kidini linaloweza kumhamasisha mtu kutukana dini ya mwenzake


jumiki wanahusika, na hawawezi kupinga hilo kuwa hawajachoma makanisa...
which means kama ni kweli ni uwt basi ni mission well executed and 100% accomplished.
 
Sioni ni kwa vipi UWT wangetumia mbinu dhaifu hivyo kuiangamiza JUMIKI. Tumewaona kwenye vyombo vya habari waandamanaji wa JUMIKI wakichoma matairi barabarani na kuziba barabara. Why should that happen?
Wewe inaonekana ni mchanga sana wa masuala ya serikali na jinsi watu wa usalama wanavyoweza kuendesha mambo kwa siri. Hivi ulitaka wakutangazie kuwa sisi UWT tupo kazini??!! Unajua maana ya njama (conspiracy). Jitahidi usome jinsi CIA au KGB walivyoweza kufanya operesheni mbalimbali wakati wa vita baridi ndiyo utajua serikali huwa zinafanya mambo gani zikitaka mambo yaende kwa mabavu.

By the way sisemi kwamba ni UWT, hilo sina hakika nalo ila kuna uwezekano kama mleta mada alivyowakilisha.
 
Ndugu yangu, ukisoma thread No 11 hapo juu ya Counterpunch yanayoelezwa yanawezekana. UWT walichukulia hasira za vijana hao nao kufanya vitu vyao -- hata kwa siku ngapi. They are capable of doing it!
Mi mawazo ya kijinga kama haya mtu akiambiwa baba yako mdogo ndo kachoma hayo makanisa utaamini tu bila kufikiri.
 
Back
Top Bottom